Watanzania wanaokimbilia kuoa Kenya kukwepa gharama wabanwa
Thursday August 22 2019
Wakazi wa wilaya ya Serengeti wanaokwenda kuoa wanawake nchini Kenya kwa madai kuwa hutumia kiasi kidogo cha fedha kukamilisha sherehe wametakiwa kuwalipia vibali vya kuishi nchini Tanzania.
BY Anthony Mayunga, Mwananchi amayunga@mwananchi. co.tz
IN SUMMARY
Wakazi wa wilaya ya Serengeti wanaokwenda kuoa wanawake nchini Kenya kwa madai kuwa hutumia kiasi kidogo cha fedha kukamilisha sherehe wametakiwa kuwalipia vibali vya kuishi nchini Tanzania.
Advertisement
Serengeti. Wakazi wa wilaya ya Serengeti wanaokwenda kuoa wanawake nchini Kenya kwa madai kuwa hutumia kiasi kidogo cha fedha kukamilisha sherehe wametakiwa kuwalipia vibali vya kuishi nchini Tanzania.
Akizungumza leo Alhamisi Agosti 22, 2019 ofisa uhamiaji Wilaya ya Serengeti, Henry Kilangwa amesema wamebaini kata ya Manchira wilayani humo, wakazi wake wengi ni wa kabila la Wakisii na Wamalagori wanaotokea Kenya.
"Nimeishawaeleza walio na wanawake wa Kenya waje ofisini wawalipie Sh100,000 kwa miaka miwili sawa na Sh50,000 kwa mwaka ili waweze kuishi Tanzania,” amesema.
Amesema watakaoshindwa kufanya hivyo watasakwa popote walipo kwa maelezo kuwa kuishi nchini bila kibali ni kosa.
Amewataka raia hao wa Kenya kutojiingiza katika siasa, kutofanya juhudi za kupata kitambulisho cha uraia wala cha kupiga kura kwa maelezo kuwa hawana sifa kisheria