Elections 2015 Hakuna kifungu cha sheria kinachomruhusu mpiga kura kukaa nje ya mita 200 toka kituoni akilinda kura

Elections 2015 Hakuna kifungu cha sheria kinachomruhusu mpiga kura kukaa nje ya mita 200 toka kituoni akilinda kura

Sawa wametumia sheria ipi kuzuwia mikusanyiko? Kwa maana ya wapiga kura.

Ukituwekea vifungu halisi tutakuelewa.

Ipo sheria ya nchi inayozuia watu kukusanyika bila ya kibali, yaani kilichokatazwa ni baada ya kupiga kura kukaa kikundi mahali kwa maana ya kukusanyika hili haliruhusiwi na hiyo sheria ipo ya kuzuia kukusanyika kama huwa mnakusanyika kundi kubwa la watu mahali pamoja na hakuna kinachotokea ni kwamba wameamua kutowafwatilia tu rejea zamani wazururaji hovyo walivyokuwa wanakamatwa au watu wasiokuwa na kazi maalumu!

Na hii ni Dunia nzima kila nchi ina hizi sheria za kuzuia mikusanyiko ya watu bila ya kibali maalumu kutoka kwa wahusika, hivyo siyo jambo geni!
 
".......mtu akikuambia upige kura na ulinde kura ..mwambie mzee njoo tulinde wote..."
Kanali kinana

Jioni njema kwa hisani ya raisi wa awamu ya tano
Dkt john pombe magufuli.
 
Nadhani sasa hii lialia ya Chadema waachiwe waangalizi wa uchaguzi ili kuona kama ni sahihi kwa tume kuwaachia wapiga kura 'walinde' kura?

Hapa namaanisha tutakaomchagua Magufuli tulinde kura na watakaomchagua Anna walinde kura.

Na wale warakaomchagua Lowassa walinde kura.

Na wapiga kura wa Hashim rungwe walinde kura n.k n.k

Yaani polisi wakae nyumbani wasubiri kama timbwili la kukinda kura likianza na damu kumwagika ndio waende vituoni.

Hii ina maana lowassa baada ya kupiga kura asimame mita 200 kwenye kituo chake pale monduli.

Magufuli akalindie kura Chato.

Mbowe naye vile vile.

Na vikongwe kama kina kingunge wakae juani na kulinda kura...

Kina mama wajawazito,vilema,mashekhe na mapadri walinde kura.

waandishi wa habari wasinyanyue miguu kwenye vituo vyao vya kupigia kura.

Tume iandae miundombinu ya kuwezesha watu kulinda kura.

Na kwa kawaida huwezi kulinda ukiwa mikono mitupu ni lazima kila mpiga kura abebe silaha ya kulindia kura...mwenye panga,bastola,mkuki na rungu abebe kabisa kwa kulinda kura.

Hiki ndicho kinachohamasishwa na UKAWA.

Hili linakuingia akilini kama mtanzania?
 
Wasomi Wetu Wananishangaza Sana, Unakutwa Mtu Anajiita Mwanasheria Wakati Hata Baadh Ya Sheria Hazijui, Nina Mashaka Sana Kama Waafrika Tutaacha Uzembe Wa Kujisomea Maandiko Mbalimbali,
Sheria INARUHUSU MTU KUENDELEA NA SHUGHULI ZAKE ZA KAWAIDA KWA UMBALI WA MITA 200 KUTOKEA KITUO CHA KUPGA KURA ,NA SI KUKUSANYIKA PALE KULINDA KURA, ANAYERUHUSIWA KUKAA PALE KITUON KULINDA NA KUHAKIKI KURA NI WAKALA WA CHAMA HUSIKA,;

MAON; natoa wito TAKUKURU wasambaze maafisa wao kila kituo cha kupgia kura na wakae ndani, maana hata mkikaa kundi nje eti mnalinda kura haisaidii kama wakala wenu ana matatizo chungu nzima, ada ya watoto ,kodi, madeni, alafu apatiwe milion 10, kubadili matokeo, tena anahamishiwa kwa mpesa hapo chumbani sijui kama anaweza kukataa, na mtakaokuwa mita 200 ndo nashangaa mtajuaje hyo, nakushauri mbowe tumia akili hyo,

Milioni 10 kwa m-pesa? ku'anyoko!! Ulinzi unawekwa ili kuzuia watu wasiohusika kuingia ndani ya chumba cha kuhesabia kura! Akionekana mtu wa hivyo "AMA ZAKE, AMA ZETU" Hivyo ulinzi wa kura ni muhimu!!
 
hakuna kifungu cha sheria kinachomruhusu mpga kura kukaa nje ya mita 200 toka kituon akilinda kura,

Swali
kunakifungu cha sheria kinachomzuia mpiga kura kukaa nje ya mita 200?

Kama kipo mleta hoja kiweke hapa

Kama hakipo basi hii mada/thread ni upuuzi wa kupuuzwa.

Raisi wa tz kwa mamlaka aliyonayo akisema kitu inakuwa ni sheria mzee
 
Tutapiga na kulinda kura.... Ni hayo tu

Angalia usije ukakosa hata hiyo nafasi ya kupiga kura!!! Rais akishasema ni kama sheria. Unamwona yule kijana aliyetoa uzushi wake wa General sasa anapata taabu Segerea hata kura hatapiga!!
 
Angalia usije ukakosa hata hiyo nafasi ya kupiga kura!!! Rais akishasema ni kama sheria. Unamwona yule kijana aliyetoa uzushi wake wa General sasa anapata taabu Segerea hata kura hatapiga!!

Hv Yericko Nyerere Mbna Kimya Sana?
 
Hivi ile tume ya uchaguzi iliyosimamia uchaguzi kule Arumeru kwa Nasari iko wapi siku hizi?

Tume ya uchaguzi ya kipindi kile iliruhusa wananchi kusubiri matokeo kwenye vituo,mshindi alitangwazwa asubui kupitia TBC,na wananchi walikuwepo,wananchi walikuwa watulivu kabisa wenye amani na furaha,ndio maana nauliza ile tume ya wakati ule iko wapi? au ile tume mwenyekiti wake alikuwa ni mzee wetu marehemu jaji------- ?

Tume tupeni majibu
uchaguzi wa ingunga wananchi walitangaziwa mayokeo vituo
arumeru
chalinze
vipi uchaguzi wa mwaka huu,au kwa kuwa mwenyekiti wa tume wa kipindi cha uchaguzi uliopita ashafariki na huyu ni mwenyekiti mpya?
 
Wasomi Wetu Wananishangaza Sana, Unakutwa Mtu Anajiita Mwanasheria Wakati Hata Baadh Ya Sheria Hazijui, Nina Mashaka Sana Kama Waafrika Tutaacha Uzembe Wa Kujisomea Maandiko Mbalimbali,
Sheria INARUHUSU MTU KUENDELEA NA SHUGHULI ZAKE ZA KAWAIDA KWA UMBALI WA MITA 200 KUTOKEA KITUO CHA KUPGA KURA ,NA SI KUKUSANYIKA PALE KULINDA KURA, ANAYERUHUSIWA KUKAA PALE KITUON KULINDA NA KUHAKIKI KURA NI WAKALA WA CHAMA HUSIKA,;

MAON; natoa wito TAKUKURU wasambaze maafisa wao kila kituo cha kupgia kura na wakae ndani, maana hata mkikaa kundi nje eti mnalinda kura haisaidii kama wakala wenu ana matatizo chungu nzima, ada ya watoto ,kodi, madeni, alafu apatiwe milion 10, kubadili matokeo, tena anahamishiwa kwa mpesa hapo chumbani sijui kama anaweza kukataa, na mtakaokuwa mita 200 ndo nashangaa mtajuaje hyo, nakushauri mbowe tumia akili hyo,

Ndugu yangu tatizo letu humu ndani watu wana mihemko lakini tatizo kubwa ni kujifanya wajuaji wakati hatujui kitu
 
Hivi ccm kuna mtu mwenye ufahamu wa mambo hata mmoja aliyebaki huko.?! Maana ukisoma uzi kama huu unaona kuna tatizo ccm. Na bahati mbaya kuanzia mpambe kama huyu mpaka mwenyekiti wa taifa wanafikiria kwa uwezo ule ule.!
 
Ipo sheria ya nchi inayozuia watu kukusanyika bila ya kibali, yaani kilichokatazwa ni baada ya kupiga kura kukaa kikundi mahali kwa maana ya kukusanyika hili haliruhusiwi na hiyo sheria ipo ya kuzuia kukusanyika kama huwa mnakusanyika kundi kubwa la watu mahali pamoja na hakuna kinachotokea ni kwamba wameamua kutowafwatilia tu rejea zamani wazururaji hovyo walivyokuwa wanakamatwa au watu wasiokuwa na kazi maalumu!

Na hii ni Dunia nzima kila nchi ina hizi sheria za kuzuia mikusanyiko ya watu bila ya kibali maalumu kutoka kwa wahusika, hivyo siyo jambo geni!

Tunahitaji vijana Kama wewe mnaojua kuchambua mambo!! Siyo hao wanajifanya kujua sheria kumbe zero!! Kuna sheria nyingi tu ambazo polisi wanaweza kuzitumia kuthibiti mkusanyiko.
 
Haiwahusu waangalizi hao na wala haihusu silaha! Bila ulinzi wa kura uchaguzi uliopita Sio Lema wala Mnyika wala Wenje wala Sugu wala Mdee wala Msigwa na wengine ambao wangalikuwa wabunge. Kwa uwepo wa watu walio mita mia moja wizi ulishindikana na utangazaji ukaahirishwa hadi muda wa majeruhi! Ikawa haiwezekani kuchakachua na kutangaza! Mradi CCM walisema kuwa hata kwa goli la mkono watashinda, ni jukumu letu kufanya kila tuliwezalo kuzuia hilo pasipo kuvunja sheria. Tutakaa umbali ambao sheria inaruhusu. Hatukubali.
 
Raisi wa tz kwa mamlaka aliyonayo akisema kitu inakuwa ni sheria mzee

Hawaelewi mkuu ila nahisi wanaleta utani kwasababu ile sheria ya kuzuia mikusanyiko zaidi ya watu 3 ipo na inafanya kazi ..mdogo mdogo wataelewa tu.
 
MAWAKALA WANAKUWEPO pia takukuru wawepo, itakuwa si rahis sana kuhonga pande zote mbili

Jumla ya vituo 65,000 hivyo maafisa wa Takukuru wa idadi hiyo watatoka labda nchi zote za Afrika mashariki.
 
".......mtu akikuambia upige kura na ulinde kura ..mwambie mzee njoo tulinde wote..."
Kanali kinana

Jioni njema kwa hisani ya raisi wa awamu ya tano
Dkt john pombe magufuli.

Umetisha mkuu!
 
Back
Top Bottom