Elections 2015 Hakuna kifungu cha sheria kinachomruhusu mpiga kura kukaa nje ya mita 200 toka kituoni akilinda kura

Elections 2015 Hakuna kifungu cha sheria kinachomruhusu mpiga kura kukaa nje ya mita 200 toka kituoni akilinda kura

Hivi kama chama tawala nacho kikiwahamasisha wapiga kura wao nao wakae umbali wa mita mia mbili ili kulinda kura zao itakuweje? Nyinyi Ukawa acheni uhuni wenu. Ni dhahiri kwamba baada ya kuona hamtashinda huu uchaguzi sasa mnatafuta njia za kuvunja amani. Hebu jaribuni kufanya hivyo na tuone.
 
sheria ya uchaguzi inaruhusu kukaa mita mia kutoka kituoni kusubiri matokeo nitafata sheria tume ya uchaguzi sijui nani huyo akitoa agizo liwe kwa mujibu wa sheria kama kinyume siwasikilizi nawapuuza tu
 
Hii itajibu mawasli mengi ya UKAWA kuhusu hizo mita 100 au 200 au 300.

Kiongozi safi sana.
 
CCM mna shida ya uwelewa. Mmekula maharage ya wapi sijui
 
kama fujo litaanzia hapo hakuna kurudi nyuma na likianzia hapo tunasimamia ikulu kuwanyofoa CCM.
 
CCM mna shida ya uwelewa. Mmekula maharage ya wapi sijui
Tatizo lenu UKAWA kama wewe ni mmoja wao, mnafuta mkumbo, huku wewe na akili yako unaweza kuthibitisha maneno yanayo semwa na viongozi wenu kama ni Uongo au ni maneno ya ulaghai.
 
Hivi kama chama tawala nacho kikiwahamasisha wapiga kura wao nao wakae umbali wa mita mia mbili ili kulinda kura zao itakuweje? Nyinyi Ukawa acheni uhuni wenu. Ni dhahiri kwamba baada ya kuona hamtashinda huu uchaguzi sasa mnatafuta njia za kuvunja amani. Hebu jaribuni kufanya hivyo na tuone.

Kwanini hawawahamasishi? Ni rahisi. Hawana wananchi wanaowatii zaidi ya dola. Meza hiyo kwanza
 
kama fujo litaanzia hapo hakuna kurudi nyuma na likianzia hapo tunasimamia ikulu kuwanyofoa CCM.
Ukifanya fujo utakua umevunja sheria za nchi ambazo Polisi ambao ndio wanao hakikisha na au enforce USALAMA WA RAIA watakushughulikia na kukuweka mahali pema Keko. Don't worry, wewe anzisha fujo tu na subiri uone mkono wa Serikali utakavyo kufunza adabu huku Lowassa akiwa amejituliza nyumbani kwake.
 
Amani mtaivunja nyie ccm, usiseme ukawa ati wanavunja amani
 
Kwanini hawawahamasishi? Ni rahisi. Hawana wananchi wanaowatii zaidi ya dola. Meza hiyo kwanza
Umekosea, kwasababu hakuna sheria inayo kuruhusu wewe UKAWA kukaa mita 100. Jaribu uone nini kitakutoke siku hiyo.
 
Hivi kama chama tawala nacho kikiwahamasisha wapiga kura wao nao wakae umbali wa mita mia mbili ili kulinda kura zao itakuweje? Nyinyi Ukawa acheni uhuni wenu. Ni dhahiri kwamba baada ya kuona hamtashinda huu uchaguzi sasa mnatafuta njia za kuvunja amani. Hebu jaribuni kufanya hivyo na tuone.

Mkuu haya yote dawa ilikua katiba mpya iliyotaka tume huru ya uchaguzi ipatikane kabla ya uchaguzi huu. Baada ya kuiona hatari hiyo waliamua kuikataa ile rasimu na kuitengeneza katiba pendekezwa, hatima yake hiyo pendekezwa mimi na wewe hatujui. CCM ina wenyewe mkuu.
 
msimizi anapaswa kutangaza matokeo je atamtangazia nani? Sheria inakataza ndani ya mita mia mbili kutojihusisha na shughuli yeyote ya siasa bali sio kuwepo eneo hilo. mfalme juha anasema asiyoyajua
 
Ndiyo kuna Sheria inayozuia watu kukusanyika bila ya sababu, Serikali ndiyo yenye jukumu la kuamua ni ipi sababu inayoruhusiwa kukusanyika na wapi ni sawa kukusanyika na wapi siyo sawa, kama yalivyo mambo mengi tu!

Baada ya matokeo kubandikwa watu wanaruhusiwa kwenda kuyasoma kinachokatazwa ni kukusanyika kukaa na kusubiri!

Mwisho hii ni Amri kutoka kwa Raisi wa JMTZ ambayo kwa kawaida haipaswi kupingwa na binadamu yoyote yule ndani ya TanZania na wewe unapaswa kutii tu bila shurti, ni rahisi kihivyo tu!

Mnajitekenya nyie, subiri tar 25 Oct mtausikia mziki wa malofa
 
wazo lako ni zuri..
lakini pia naomba nikujuze ya kwamba miongoni mwa idara zinazoongoza kwa kula RUSHWA ni pamoja na TAKUKURU yenyewe..
hili la kukaa mita mia mbili pia linalenga kuzuia misafara isiyoeleweka kuelekea kwenye vituo wakati wa kuhesabu kura..
amini usiamini eti majina ya pikipiki na migahawa nayo ndani ya daftari..i mean nayo ni wapiga kura...
ndio maana tume ilikataa mawakala kwenye majumuisho ya daftari..
 
Mkuu haya yote dawa ilikua katiba mpya iliyotaka tume huru ya uchaguzi ipatikane kabla ya uchaguzi huu. Baada ya kuiona hatari hiyo waliamua kuikataa ile rasimu na kuitengeneza katiba pendekezwa, hatima yake hiyo pendekezwa mimi na wewe hatujui. CCM ina wenyewe mkuu.
Hebu angalia hao Ukawa waliotakiwa kuwa watetezi wa katiba ya wananchi wanavyofanya sasa hivi. Unawaamini kweli hawa jamaa, wakati wao wenyewe ndio vinara wa kuvunja katiba zao?
 
Back
Top Bottom