Hakuna kitu kinaumiza kama unaamka Asubuhi na hujui utaenda wapi

Vitu vya kufanya, kama ni Muislam.

Amka asubuhi nenda msikitini ukasali jamaa na sala za jamaa zisikupite.

Jiunge na chama cha siasa ujumuike na wenzako na ufanye mazoea ya kwenda mara kwa mara. CCM connection nyingi.

Jiunge na vikundi vya michezo, hususan mpira, vya hapo mtaani kwako au jirani na mtaani kwako.

Jiunge na meza za vijana au wazee wanapocheza bao na draft jioni.

Vijiwe vya kahawa ni muhimu sana, ujlvijuwe hata kama vipo mbali na wewe, uwe unaenda kila siku japo mara moja baada kusali alfajiri na au jioni.

Mjuwe mwenyekiti wako wa serikali ya mtaa na wajumbe wake wote. Kuwa karibu nao, siyo kuwajuwa kwa sura tu. Uwe na mawasiliano nao ya karibu.

Mjuwe Diwani wako na uwe na mawasiliano nae ya mara kwa mara.

Wajuwe wafanya biashara wakubwa na wadogo wa mtaani kwako, jisogeze kwao uwe na ukaribu nao.

Wajuwe watu wanaojenga mtaani kwako au maeneo ya karibu na hapo, ufanye ukaribu na mafundi na ma engineer wa ujenzi.


Sasa kijana ukiwa na connection na wote hao na ukiwa na mawasiliano nao utakosa cha kifanya kweli?

Fikiri.
 
Wewe nae toa upuuzi wako hapa,kila kitu uislamu
 
Wewe nae toa upuuzi wako hapa,kila kitu uislamu
Kama si Muuslam atakwenda msikitini kuswali sala 5?

AlhamduliLlah, mimi ni Muislam na najivunia Uislam wangu.

hiyo kwenda msikitini tu, kutwa mara 5, inampa mtu connections kibao.
 
Mbona juzi Marco Rubio yule US secretary of State, alisema misaada ya USAID kwa NGO imerudishwa tena 🤔 ERoni
 
Kama si Muuslam atakwenda msikitini kuswali sala 5?

AlhamduliLlah, mimi ni Muislam na najivunia Uislam wangu.

hiyo kwenda msikitini tu, kutwa mara 5, inampa mtu connections kibao.
Mkuu nipe basi connection kama ipo
 
Nenda mjini tuu Kuna vijiwe kibao
 
Asante kwa ushauri mzuri ubarikiwe Sana
 
Tena ukiwa na njaa ndy utajuwa Kila kitu ktk maisha yako,wanao kupenda na wasio kupenda utawajuwa.
Kuanzia mke uliyenae,ndugu.

Ukiwa na njaa hata kama una AFYA mgogoro pia itajulikana.
Njaa inadhalilisha utu wa mtu.
Halafu sijui kwanini mtu ukimaliza chuo ukakaa mda mrefu sana bila ajira, maisha yakikupiga, inafika mahali mtu akikuona anaona kama dishi lako limeyumba, ila kiuhalisia una akili timamu, au kuna saa mtu akikuangalia anahisi wewe ni mlevi wa pombe, kumbe kiuhalisia hunywagi pombe hata kidogo mwandende
 
Unamaanisha tangu umemaliza degree chuo, uko home miaka 10 bila kazi😲 na bado kula yako inategema wazazi kwa asilimia 100, alooo Tayana-wog
Mkuu hiko Cha kushangaza kwani?
Ulishawahi kufanya mishe na ikagoma?
Usifanye mchezo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…