Vitu vya kufanya, kama ni Muislam.
Amka asubuhi nenda msikitini ukasali jamaa na sala za jamaa zisikupite.
Jiunge na chama cha siasa ujumuike na wenzako na ufanye mazoea ya kwenda mara kwa mara. CCM connection nyingi.
Jiunge na vikundi vya michezo, hususan mpira, vya hapo mtaani kwako au jirani na mtaani kwako.
Jiunge na meza za vijana au wazee wanapocheza bao na draft jioni.
Vijiwe vya kahawa ni muhimu sana, ujlvijuwe hata kama vipo mbali na wewe, uwe unaenda kila siku japo mara moja baada kusali alfajiri na au jioni.
Mjuwe mwenyekiti wako wa serikali ya mtaa na wajumbe wake wote. Kuwa karibu nao, siyo kuwajuwa kwa sura tu. Uwe na mawasiliano nao ya karibu.
Mjuwe Diwani wako na uwe na mawasiliano nae ya mara kwa mara.
Wajuwe wafanya biashara wakubwa na wadogo wa mtaani kwako, jisogeze kwao uwe na ukaribu nao.
Wajuwe watu wanaojenga mtaani kwako au maeneo ya karibu na hapo, ufanye ukaribu na mafundi na ma engineer wa ujenzi.
Sasa kijana ukiwa na connection na wote hao na ukiwa na mawasiliano nao utakosa cha kifanya kweli?
Fikiri.