View attachment 2971213
MAGUFULI: HAKUNA KUZUIA WATU KUTOKA NDANI (LOCKDOWN) DAR WALA SEHEMU YOYOTE TANZANIA KWA SABABU YA CORONA
1. “Wapo wengine wanatoa mawazo ya kuifunga Dar es Salamaam hilo haliwezekani kwasababu karibu asilimia 80 ya ukusanyaji wa kodi kwa nchi yetu inapatikana Dar es salaam, tuendelee kuchukua hatua lakini kuifungia Dar hiyo ‘never’ na tunatakiwa tujue kuwa idadi ya watu wake ni karibu milioni sita (6) kwa hiyo uwezekano wa kuwa na wagonjwa wengi ni mkubwa ikilinganishwa na mikoa mingine. Hakuna 'lockdown' itakayifanyika sehemu yoyote ya nchi".
2. "Nawapongeza viongozi wa dini na watanzania kwa ujumla kwa kuitikia wito wa kuliombea taifa kwa siku 3 dhidi ya Covid19."
3. "Tuwe wakweli kwenye kutoa taarifa, tusiwafiche. Mfano kwa taarifa za leo tuna wagonjwa 284 lakini waliopona ni 11, lakini mimi taarifa niliyopewa hapa waliopona ni 100, tusiwajengee hofu Watanzania".
4. "Hakuna virusi wanaokufa kwa fumigation. Kilichofanyika Dar es Salaam kupuliza dawa yenye kemikali ni upuuzi. Wanaokufa kwenye fumigation ni mende na si virusi ikiwemo virusi vya Corona. Suala la kupuliza dawa ni upumbavu mtupu. Hakuna kirusi cha Corona kinachoweza kufa kwa Chlorine. Naomba IGP na Vyombo ulinzi mkachunguze walikuwa na lengo gani na nani alitoa hizo dawa”
5. “Tunajua kuwa 'fumigation' inauwa wadudu kama viroboto, chawa na si Virusi sasa sijui ni nani aliyesema mkoa wa Dar es Salaam ufanyiwe hivyo naomba hili suala lichunguzwe siyo kila kitu kinachotoka nje lazima tukifanye tutakuta tunasaidia kusambaza Corona,”
6. "Hii fumigation iliyokuwa inafanyika Dar es Salaam ni upuuzi mtupu, kwa sababu virus wa corona huwezi ukamuua kwa chlorine, virus yule ni mafuta, na lile linapasuka pasuka kwa kutumia sabuni au pombe".
7. “Dar na Mwanza niliona mabasi yanapulizwa dawa na hasa Dar, hakuna upuliziaji dawa unaoweza kuua corona, ingekuwa pakipulizwa corona wanakufa, nchi zilizoendelea wangemwagia nchi zao kwa ndege na wasingekuwa wanakufa, kule kupuliza dawa ni upuuzi tu”.
•
8. “Huwezi kuua corona kwa kupuliza dawa kwenye mabasi na mitaani ile unaua mende na wadudu wengine, ila hatujiulizi kwamba labda kupuliza ndio tunaongeza corona, maana Dar imepulizwa dawa tu na kasi ya wagonjwa imeongezeka, vyombo vya ulinzi mkachunguze nani alitoa hizo dawa”
9. "Hakuna sababu ya kuweka watu karantini kwa siku 14. Kama mtu umempima ukaona hana tatizo mruhusu aende nyumbani. Tubaki kushughulika na wagonjwa."
10. "Tutumie njia za asili kujikinga. Ukijifukiza kwa nyuzi joto zinazozidi 100 kama una kirusi cha korona kitapasukapasuka. Wanaotumia mwarobaini na vitunguu waendelee kutumia."
11. "Barakoa zinazotoka nje inawezekana zimebeba virusi vya corona. Kuna baadhi ya nchi wamechunguza misaada hii inaweza kuleta Corona zaidi. Tujihadhari na barakoa hasa za kupewa msaada kutoka nje. Kama mtu anaweza kujishonea barakoa yake shona vaa. Viwanda vya ndani pia vianze kutengeneza barakoa kwa usalama wetu."
12. “Ugonjwa huu umekumba dunia nzima na kama tunavyofahamu uwezo wa nchi za Afrika kiuchumi hauwezi ukalingana na nchi zilizoendelea, tunaziomba nchi hizi hasa benki ya dunia badala ya kukopesha watusamehe wanayotudai."
13. “Kwa sisi Tanzania huwa tunalipa karibu bilioni 700 kila mwezi sasa ni wakati muafaka wa benki ya dunia ambayo imeguswa na janga hili itusamehe madeni hayo ili fedha hizo zikatumike katika kupambana na janga hili la corona,”
14. “Niziombe taasisi za Fedha Duniani kwa sisi nchi maskini badala ya kutoa unafuu wa Mikopo kwa ajili ya kupambana na Corona watufutie baadhi ya madeni au kupunguza riba katika mikopo tunayolipa kusudi mapato tunayopata yakapambane na corona na si kulipa madeni”
-
15. "Ni wakati muafaka wa Benki ya Dunia ambayo imeguswa na ugonjwa huu na wana nia nzuri ya kutusaidia katika ugonjwa huu watusamehe madeni hata by percentage, ili kusudi hizi fedha tunazolipa na interest katika fedha tulizokopa zikatumike katika kupambana na Corona".
John Pombe Magufuli
Rais wa Tanzania
________________________________
NOTE: Binafsi kuna baadhi ya mambo nimemuelewa Rais katika hotuba ya leo akilihutubia Taifa kuhusu hali ya Corona na baadhi sikubaliani nayo au tuseme pengine sijamuelewa kwa sasa na pengine nikaelewa baadae sana au nisielewe kabisa.
Nitaeleza baadae ni yapi ninakubaliana na yapi sikubaliani nayo katika hotuba hii ya Rais Magufuli. Wacha niendelee kutafakari.
Je wewe ni kipengele kipi hapo juu umekielewa/unakubaliana nacho zaidi na kipi hujakielewa/hukubaliani nacho?
Nini maoni yako? (Chonde chonde, Maoni yawe ya staha jamani hii ni hotuba ya Rais sio ya Mwenyekiti wa Kitongoji)
Remmy Cameroon
Sauti ya wasio na sauti