Hakuna marefu yasiyo na ncha. Ni kitu gani kinaweza kuja kuitoa CCM madarakani?

Hakuna marefu yasiyo na ncha. Ni kitu gani kinaweza kuja kuitoa CCM madarakani?

G Tank

JF-Expert Member
Joined
Feb 9, 2023
Posts
2,297
Reaction score
8,760
Hakuna ajuae labda ni miaka 50 ijayo au zaidi, lakini hili halikwepeki.

Najua humu JF kuna wachambuzi wazuri wa haya mambo ya politics za nchi,

Ni kitu gani kinachoweza kuchangia ccm itolewe madarakani.
  • Vyuma vikikaza sana
  • Mpasuko mkubwa ndani ya CCM utaotengeneza chama kipya
  • Muungano kuvunjika
  • Civil Unrest nchi nzima - Maandamano, migomo, kufunga barabara, n.k.
  • au?
 
Hakuna ajuae labda ni miaka 50 ijayo, lakini its certain.

Ni kitu gani kinachoweza kuchangia ccm itolewe madarakani.

  • Mapiduzi ya vita
  • Mapinduzi ya diplomasia
  • Baadhi ya wana ccm kutengeneza chama kingine
  • Muungano kuvunjika
  • au ?
Machafuko ama mapinduzi ya kijeshi ndio yataitoa ccm madarakani. Lakini kwa njia ya kura ni kupoteza muda, maana wahesabu kura na watangaza matokeo ni chawa wa ccm.
 
Mapinduzi ya kijeshi ndio yatawatoa ccm madarakani, kwa uhakika. Yaweza kuwa mapinduzi ya moto(risasi, mabomu, makombora na mizinga ikatumika) au mapinduzi baridi yaani kimya kimya vyombo vya ulinzi na usalama vinakataa kutumika kutesa watu na kukataa kutumika kuiba kura.

Ila yatafanywa na kizazi kipya cha ma askari, hawa ma genZ wakipanda vyeo vya kijeshi na vyuma Vikiwabana na wakiona watoto wao hawana ajira na watoto wa ndugu, jamaa, marafiki zao hawana ajira, ccm itakuwa byebye.
 
Machafuko ama mapinduzi ya kijeshi ndio yataitoa ccm madarakani. Lakini kwa njia ya kura ni kupoteza muda, maana wahesabu kura na watangaza matokeo ni chawa wa ccm.
Umejuaje kuwa wanajeshi wakipindua hawataitisha uchaguzi tena na ccm ikashinda?

Jeshi likipindua na lisiitishe uchaguzi, utatamani ni bora ungekuwa unatawaliwa na CCM.

Kwa kifupi kabisa, ni uwendawazimu kutamani utawala wa kijeshi.

Njia sahihi na bora zaidi, ni tume huru ya uchaguzi, tume ambayo haichaguliwi na viongozi walio madarakani.
 
Maandamano ya gen z ndio yatawaondoa haya maccm madarakani
Haiwezekani mtu ana shahada na anaendesha bodaboda mtaani.
 
Kama kuna nyakati ambapo upinzani wana nafasi ya kuiondoa ccm madarakani basi uchaguzi 2025 ni nafasi nzuri .

Kama sio 2025 ; Pia Civil war itaiondoa ccm madarakani huko mbeleni kutokana matendo mengi ya kijinga yanayofanywa na serikali ya ccm .
 
Kama kuna nyakati ambapo upinzani wana nafasi ya kuiondoa ccm madarakani basi uchaguzi 2025 ni nafasi nzuri .
hio 2025 cha mtoto, Kulikuwa na chaguzi za 1995, 2010, 2015.
 
Hangaya atakitoa madarakani.
Keshafanikiwa mpaka sasa.
 
Hakuna ajuae labda ni miaka 50 ijayo, lakini its certain.

Najua humu JF kuna wachambuzi wazuri wa haya mambo ya politics za nchi,

Ni kitu gani kinachoweza kuchangia ccm itolewe madarakani.

  • Vyuma vikikaza sana
  • Mapinduzi ya jeshi
  • Mpasuko mkubwa ndani ya ccm utaotengeneza chama kipya
  • Civil war watu kuanza kujiorganize misituni kupindua nchi
  • Muungano kuvunjika
  • Civil Unrest nchi nzima - Maandamano, migomo, kufunga barabara, n.k.
  • au ?
Mpasuko wa ccm ndio likely kuja kuitoa ccm not otherwise na hili litatokea pale wale wanaojiona chama ni mali yao wakija kubaguliwa na mtu mgeni kwenye chama ambaye wataona hastahili kuwatenga, civil unrest kwa tanzania bado sana maana polisi wetu kwakweli tuwape hongera wamekuwa makini kwa viashiria vyovyote vya kuvuruga amani
 
Back
Top Bottom