Hakuna marefu yasiyo na ncha. Ni kitu gani kinaweza kuja kuitoa CCM madarakani?

Hakuna marefu yasiyo na ncha. Ni kitu gani kinaweza kuja kuitoa CCM madarakani?

Mpasuko wa ccm ndio likely kuja kuitoa ccm not otherwise na hili litatokea pale wale wanaojiona chama ni mali yao wakija kubaguliwa na mtu mgeni kwenye chama ambaye wataona hastahili kuwatenga, civil unrest kwa tanzania bado sana maana polisi wetu kwakweli tuwape hongera wamekuwa makini kwa viashiria vyovyote vya kuvuruga amani
Kukiwa kuna kina Luhaga Mpina kama 20 hivi inawezekana

Kuhusu polisi ni rahisi kucontroll civil unrest sababu watanzania wachache sana wana uthubutu wa kuwa face field force, Mnaweza kuandamana wengi ila defender moja tu ikionekana kila moja anatawanyika wanaobaki wanahesabika.
 
Kizazi kijacho (new generation) kitaleta mabadiliko,kwa sasa wanaopaswa kutenda haki wamekariri (mapokeo ya zamani).

Ni bora watawala waanze kuzoea kukubali mabadiliko,wakikubali watazoea kuwa inawezekana kubadilisha uongozi bila kuangalia aina ya chama anakotokea mgombea.

Marehemu,awamu ya 5,alilazimisha matokeo ya uchaguzi hadi aibu.(tena akalazimisha kuwatafuta wabunge upinzani bila hata kuzingatia utaratibu).
Ni aibu ambayo kwa watawala na watawaliwa hawatakaa wasahau.

Tukumbuke kizazi kijacho kitatudharau sana,kwa kukwepa ukweli na huhadaa wananchi kuwa yote yaliyofanyika na yanayofanyika yanakubalika.Ndipo watakapo anzia kuweka utaratibu wenye kulinda haki na nafasi ya mtanzania yoyote kuchaguliwa na kupewa ridhaa ya kushika madaraka bila kuangalia chama anachotekea.
 
Umejuaje kuwa wanajeshi wakipindua hawataitisha uchaguzi tena na ccm ikashinda?

Jeshi likipindua na lisiitishe uchaguzi, utatamani ni bora ungekuwa unatawaliwa na CCM.

Kwa kifupi kabisa, ni uwendawazimu kutamani utawala wa kijeshi.

Njia sahihi na bora zaidi, ni tume huru ya uchaguzi, tume ambayo haichaguliwi na viongozi walio madarakani.
Tume ambayo haichaguliwi na viongozi walioko madarakani hilo limeshashindikana. Bora liingie jeshi ilo wote tujute, baada ya hapo wote tutatii sheria. Ccm haina uwezo wa kupata 50% kwenye uchaguzi huru maana ni chama cha wazee.
 
Watu wa nyikani Ngorongoro, Manyara n.k wameonesha dalili kuwa wafugaji, wavuvi na wakulima vijijini wameamka. Na ndiyo watafanikishwa kukiondoa chama dola kongwe CCM

Watu wa mjini pamoja na tambo zao za kuwa wajanja wameshindwa kuandamana kushindikiza chochote kilicho haki yao.

Watu wa nyikani huko vijijini wameweza kuibana serikali isiyo na masikio ya usikivu hadi imewasikiliza.

HISTORIA YA WATU WA NYIKANI WAKULIMA NA WAFUGAJI KUONGOZA MAPINDUZI

Maasi ya Jacquerie ya mwaka 1358 ni moja ya maasi maarufu na ya kustaajabisha ya wakulima wa karne ya Zama za Kati.

Yakianzia katika kijiji kidogo lakini hatimaye kuteka sehemu kubwa ya kaskazini mwa Ufaransa, waasi wa Jacquerie waliharibu majumba ya kifahari na kuua makumi ya wakuu kabla ya kuwekwa chini katika wimbi la umwagaji damu la ukandamizaji.

Uasi huo ulitokea baada ya Kifo Cheusi na wakati wa Vita vya Miaka Mia, na ulihusishwa kwa karibu na uasi wa Paris dhidi ya utawala wa kifalme wa Ufaransa.

Maasi ya Jacquerie ya 1358 inasuluhisha mizozo ya muda mrefu kuhusu ikiwa uasi huo ulikuwa mlipuko usio na mantiki wa hasira ya wakulima kuchochea pia upanuzi wa uasi wa watu wa mjini Paris Udaransa.

Inaonyesha kuwa mahitimisho haya yanayopingana yanatokana na dhana potofu kwamba uasi ulikuwa harakati ya umoja yenye malengo yanayoshabiana. La hasha bali kila kundi likikuwa na vipaumbele vyake mfano watu wa Nyikani (vijijini) kuna vitu waliona vinawagusa moja kwa moja, huku pia watu wa mjini walilkuwa na masuala yao yenye mguso wa kipekee kwa mazingira ya mijini

Kwa kweli, maasi ya Jacquerie inabidi ieleweke kama moja ya matukio mengi ambayo yaliibuka kwa wakati mmoja.

Ilihusisha maelfu ya watu, ambao walielewa walichokuwa wakifanya kwa njia tofauti na kubadilisha.

Hadithi ya maasi ya Jacquerie ni kuhusu jinsi watu binafsi na jumuiya zilivyopitia matatizo yao mahususi ya kisiasa, kijamii, na kijeshi, jinsi walivyoitikia matukio yalipokuwa yakitokea, na jinsi walivyochagua kukumbuka (au kusahau) katika matokeo yake.

Jacquerie Revolt ya 1358 inaandika upya masimulizi ya kipindi hiki cha msukosuko na inatoa tahadhari maalum jinsi vurugu na mahusiano ya kijamii yalivyotumiwa kuhamasisha uasi maarufu.
 
Hakuna ajuae labda ni miaka 50 ijayo, lakini its certain.

Najua humu JF kuna wachambuzi wazuri wa haya mambo ya politics za nchi,

Ni kitu gani kinachoweza kuchangia ccm itolewe madarakani.

  • Vyuma vikikaza sana
  • Mapinduzi ya jeshi
  • Mpasuko mkubwa ndani ya ccm utaotengeneza chama kipya
  • Civil war watu kuanza kujiorganize misituni kupindua nchi
  • Muungano kuvunjika
  • Civil Unrest nchi nzima - Maandamano, migomo, kufunga barabara, n.k.
  • au ?
Watakuja kutolewa na reila odinga
 
Hakuna ajuae labda ni miaka 50 ijayo, lakini its certain.

Najua humu JF kuna wachambuzi wazuri wa haya mambo ya politics za nchi,

Ni kitu gani kinachoweza kuchangia ccm itolewe madarakani.

  • Vyuma vikikaza sana
  • Jeshi kuingilia kati
  • Mpasuko mkubwa ndani ya ccm utaotengeneza chama kipya
  • Civil war watu kuanza kujiorganize misituni kupindua nchi
  • Muungano kuvunjika
  • Civil Unrest nchi nzima - Maandamano, migomo, kufunga barabara, n.k.
  • au ?
Hujaweka Kurudi Kwa Masii (Yesu kristo)
 
Wamaasai wakikaa vizuri huo uhuni wanaofanyiwa utakitoa chama
 
Vyeo vitatu tu
Mkuu wamajeshi
DGs TISs
IGP
Upinzani kupigiwa kura nyingi mpaka

-bilahayo hapo juu ccm haing'atuliwi
 
Ok lakini tunajaribu ku analyse sababu sababu ambazo zipo likely
Muda wakufa ukifika ata kama utafanya nini lazima ufe.Sasa sababu za hicho kifo zitasababishwa na muda kufika.Tunaweza tukajadili sababu nyingi sana na zisitimie ila muda ndio sababu sahihi kwasababu wenyewe unakuja na full parckage.
 
Machafuko ama mapinduzi ya kijeshi ndio yataitoa ccm madarakani. Lakini kwa njia ya kura ni kupoteza muda, maana wahesabu kura na watangaza matokeo ni chawa wa ccm.
Na mhesabuji na mtangazaji kura ni two independent separate entities.
 
Eradicate all Tanzanians aged 15-100yrs, then ccm will be wiped off. Otherwise we still have a long way before this swine is terminated.
 
Mimi Imhotep sikubaliani na njia ya Machafuko au Civil War haifai mifano iko mingi mimi naamini katika Migomo na Maandamano ya AMANI ili tupate KATIBA MPYA na TUME HURU YA UCHAGUZI after that ni sawa sawa na Mwali keshalala kitandani na kanga moja inakuwa kazi ni kwetu WANANCHI kuchagua TUNAYEMTAKA.
 
Hakuna ajuae labda ni miaka 50 ijayo, lakini its certain.

Najua humu JF kuna wachambuzi wazuri wa haya mambo ya politics za nchi,

Ni kitu gani kinachoweza kuchangia ccm itolewe madarakani.

  • Vyuma vikikaza sana
  • Jeshi kuingilia kati
  • Mpasuko mkubwa ndani ya ccm utaotengeneza chama kipya
  • Civil war watu kuanza kujiorganize misituni kupindua nchi
  • Muungano kuvunjika
  • Civil Unrest nchi nzima - Maandamano, migomo, kufunga barabara, n.k.
  • au ?
Hayo ni maoni yako ila mimi naona vitakavyoitoa CCM madarakani ni:
1.Udini
2.Ukabila
3.Ukanda
4.Wizi uliyopindukia
5.Ufisadi
6.Uchawa
7.Kusahau maana ya Siasa ya Ujamaa na Kujitegemea
8.Madeni yasiyolipika
9.Mikataba mibovu
10.Wageni.
 
Machafuko ama mapinduzi ya kijeshi ndio yataitoa ccm madarakani. Lakini kwa njia ya kura ni kupoteza muda, maana wahesabu kura na watangaza matokeo ni chawa wa ccm.
Mapinduzi ya kimachafuko either ya Jeshi navyo ni unluckily kutokea maana Jeshi let la TZ ni Ccm C.

1)ndani ya Jeshi Kuna watu wanatafuta vyeo kwa kujituma kabla hata hawajatumwa.
Mara nyingi habari za JW kufanya Usafi kila Chadema wanapotaka kufanya maandamano utoka kwa wakuu wa JW hata kabla simu ya Magogoni.

2) ni nadra sana watu kufanya machafuko endapo JESHI,MAHAKAMA,SERIKALI NA BUNGE VINASHIRIKIANA KUMKANDAMIZA RAIA.
kinachotokea Tanzania ndiyo kinachokea Urusi,N/korea na Nchi zingine za Africa.
TIME NDIYO ITAFANYA RESET YENYEWE.
 
Hakuna ajuae labda ni miaka 50 ijayo, lakini its certain.

Najua humu JF kuna wachambuzi wazuri wa haya mambo ya politics za nchi,

Ni kitu gani kinachoweza kuchangia ccm itolewe madarakani.

  • Vyuma vikikaza sana
  • Jeshi kuingilia kati
  • Mpasuko mkubwa ndani ya ccm utaotengeneza chama kipya
  • Civil war watu kuanza kujiorganize misituni kupindua nchi
  • Muungano kuvunjika
  • Civil Unrest nchi nzima - Maandamano, migomo, kufunga barabara, n.k.
  • au ?
1.Wakianzaa kufarakana wenyeweee, humo ndani na siku sii nyingii hilo linaenda kutokeaa.

2.Siku mfumo ukianza kuwakataa maana ccm na mfumo ni pete na kiddle na wengi wa Ccm ni wa mfumoo na Vitengo.

3. Atokee kiongozi wa bara aanze kuinanga Zanzibar wanzibar wakinukishe
 
Back
Top Bottom