Hakuna marefu yasiyo na ncha. Ni kitu gani kinaweza kuja kuitoa CCM madarakani?

The time for factory reset, is right on the door.
 
Mungu.
 
muda ukifika umefika, hakuna cha polisi Wala nini. umma ukiamka umeamka.

Jesus is Lord
 
Inashangaza sana, Wazanzibar wanaonyesha wazi wazi kuwa na nchi yao tena kwa vitendo lakini huku wabara wameng'ang'ania muungano kiasi cha kuwa tayari kumpoteza mwenye maoni tofauti. Kuendelea na uchaguzi wa 2024/25 kwa hali ilivyo sasa ni kukosa busara au kuhalalisha upigaji. 😡
 
28 Agosti 2024
Mahakama Kuu ya Tanzania
Kanda ya DSM
Kivukoni Front

Wakili msomi Jebra Kambole anatupa mrejesho wa kesi hii muhimu kwa umma iliyofunguliwa na raia kupinga TAMISEMI kusimamia uchaguzi 2024


View: https://m.youtube.com/watch?v=qXWaGxLc2GYSerikali yaleta mapingamizi manne ambayo yakiwemo :
Kiapo cha waombaji
Nafuu mbadala
shauri la kikatiba

Hivyo kutokana na mapingamizi yaliyoletwa na serikali, Mahakama imesogeza mbele siku ya kusikiliza kesi hadi tarehe 02 September 2024
 
Ni ukweli usiopingika kuwa chama cha kijani kimejizatiti kubaki madarakani milele lakini kanuni ya asili inakataa kuwa hilo haliwezekani, wakati ukifika sababu ya kifo itapatikana tuu. Lakini katika hizi zilizotajwa hapo yaweza kuwepo au isiwepo cha msingi kifo kimefika. Kwangu mimi nakiona hiki kuwa chama kilichojengwa katika misingi ya uchawa, uongo na unafiki. Mnafiki ni mtu ambaye anachosema sicho anachomaanisha Moyoni, hapo ndipo penye anguko la chama na serikali yake. Uchawa na unafiki wa kupindukia ukikithiri, ndipo penye anguko la chama na serikali yake
 
Pascal brother, tunaomba uwashauri Jf staffs, waache kupiga watu ban za muda mrefu.

Kitendo hicho kimefanya watumiaji walio wengi kuachana na Jf.

Ni ushauri tu.
 
Ccm yenyewe inabadilika badilika mno. Ccm ya jpm na ya kikwete utadhani ni vyama viwili tofauti.
 
Si kwa sanduku la kura sababu jamaa hao ni vibaka wazoefu na dola inakuwa nyuma yao.

Ni wananchi itafika point wataamua liwalo na liwe. Mfano mzuri ni majuzi huko shy watu wakaamua iwe bwai na kweli ikawa mbwai.
 
Kupasuka CCM ni ngumu sababu kabla hata vikao vya kuipasua havijaamza wahusika WANAPASUKA wote.
Recall CCJ ya kina Mzee Sita na kina Nape chama kikafika kwenye briefcase pale Mlimancity.
 
Mpaka matrix wawe hawafaidiki na CCM.
 
03 September 2024

Mahakama Kuu ya
Tanzania,
Masijala (Registry) Ndogo DSM
Br. Kivukoni Front

SERIKALI YAWASILISHA HOJA ZAKE ZA MAPINGAMIZI, YANGANGANIA TAMISEMI ISIMAMIE CHAGUZI 2024

Serikali ya CCM kupitia wanasheria wa serikali wamewasilisha mapingamizi manne, wakidai hii ni kesi ya kikatiba kuwa nafuu inaweza ....

KESI YA KUPINGA TAMISEMI KUSIMAMIA UCHAGUZI, JEBRA KAMBOLE mahakamani.....

View: https://m.youtube.com/watch?v=RBKZ-DKOFIY
 
Maadam inaongoza vizuri wananchi wataendelea kuipenda. Wapinzani wenyewe wananunulika nani atawaamini?
 
Shida yetu watanzania sio CCM,

Watanzania tunahitaji Amani, Haki na ustawi wa jamii

Anayekwamisha haya yote sio CCM, bali ni viongoji na raia wa Tanzania

Viongozi hawajali siasa Safi na utawala Bora
Raia hawataki kuchukua hatua za kuwabana viongozi wao

CCM Haina kosa!
Kuinyooshea CCM kidole juu ya ustawi duni wa Taifa ni kuikosea Sana!
 
CCM ndiyo kikwazo cha yote hayo kutokuwa na sera moja ya Chama inayoeleweka.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…