Hakuna marefu yasiyo na ncha. Ni kitu gani kinaweza kuja kuitoa CCM madarakani?

Mungu.
 
Option 1: Mdororo mkali wa kiuchumi , kupanda bei mahitaji ya msingi, ukosefu wa ajira wa kiwango cha juu .

Option 2: Tume huru ya uchaguzi, uwepo wa marekebisho makubwa kwenye nguvu za rais kikatiba, vyombo huru vya kufuatilia mienendo ya ya vyombo vya usalama hasa polisi, utengano wa chama [shughuli za chama] na serikali.

Option 3: Hii ni ngumu kidogo japo inaweza kutokea ambayo ni makundi ya waasi katika jeshi .
 
03 September 2024
Mahakama Kuu
Kanda ya DSM
Kivukoni Front


View: https://m.youtube.com/watch?v=vw8cwCWupss

Toka mktaba,:

28 Juni 2021

RAIS SAMIA Kuhusu KATIBA MPYA na MIKUTANO ya KISIASA: "NIPENI MUDA NIJENGE NCHI KIUCHUMI"



View: https://m.youtube.com/watch?v=WBHiCf-WOboGlobal TV Online

Rais Samia ameeleza msimamo wake jana alipozungumza na wahariri wa vyombo vya habari katika kuhitimisha siku 100 za utawala wake, Ikulu mkoani Dar es Salaam.

Amesema kuwa hivi sasa amejikita katika kuimarisha uchumi wa nchi kwani umeshuka kutokana na sababu mbalimbali ikiwa ni pamoja na athari za ugonjwa wa corona zinazoikabili dunia. Hivyo, amewataka watanzania kuwa na subira kwani baada ya jitihada hizo atashughulikia madai hayo.

“Kama inavyosemwa nimeanza vizuri naomba nipeni muda nisimamishe nchi kwanza kiuchumi. Tuite wawekezaji wawekeze ajira zipatikane uchumi ufunguke halafu tutashughulikia Katiba, tutashughulikia mikutano ya hadhara wakati ukifika,” alisema Rais Sam
 
TOKA MAKTABA :

Mwezi Machi 2018 : Rais adhibitiwe




PROF LWAITAMA, AMVAA MAGUFULI ATAKA MAGUFULI ADHIBITIWE

Watu hawataki kuwa mateka wa kikundi cha watu kwa kuwatisha kupitia chama dola. Chama dola siyo chama cha kweli cha kisiasa maana hakina ushawishi bali kinatumia dola kutisha watu...


View: https://m.youtube.com/watch?v=RiOTQa88chQ
Watanzania wanataka Maendeleo ndani ya uhuru, demokrasia ndani ya uhuru, uchaguzi huru na wa haki ... chama cha ukombozi kujigeuza chama tawala wakati tumetoka kutoka ukoloni ni dhana potofu, chama kinatakiwa kinachoongoza siyo kutawala maana hatupo ndani ya ukoloni ...
 
Hadi hapo jamii itaporudishiwa akili, (kumbukumbu), binadamu akipata changamoto, (uncertainty), huamsha ubongo na kutatua changamoto, (adaptbility skills), ama kubuni mbinu zitakazo tatua changamoto, kwa ufupi tu binadamu ana akili sana lakini binadamu huyo huyo ni mvivu wa kufikiri
 
Time
 
CCM kutoka madarakani ni rahisi sana!
Tukumbuke wako madarakani kwa sababu za wizi wakisaidiwa na vyombo vya dola!
 
Vyama kama ccm vyenye mizizi kama mbuyu huwa vinaondoka kwa aina mbili au tatu tu..

Kwanza mkuu wa nchi akiamua kuachia ngazi ccm au kujivua uanachama basi imeisha hiyo yaani leo hii samiha akisema yeye sio mwana ccm ujue ccm kwisha sasa acha waendelee kumkeraa..

Pili kupitia viongozi Mapandikizi yaani vibaraka na wakapata nafasi na ushawisho mkubwa ndani cha ccm basiii imeisha hiyo mfano ni lowasa hakuwa pandikizi ila alikuwa na ushawishi imagine kuhama kwake ukawa kuliondoka na wenyeviti wa mikoa wa ccm kibao walimfuata. Kilichotokea kipindi kile 2015 ni haukuwa wakati sahihi kwa tukio kama lile tukio lile lingetokea 2050 ccm ingeng'ookaa..

Kingine ni mashinikizo yankimataifa kuna muda wenye dunia yao wakiamua jambo hakuna namna wewe dagaa utabisha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…