Hakuna mchezaji ambaye atatokea katika hii dunia kama mnyama Pele the don(black mamba) record hazidanganyi

Tuzo hiyo alipewa Pele,afu watu wengi hawakumuona Pele,Pele ndo mpango mzima fuatilia ujue ukweli kwamba FIFA awawezi wakampa MTU ambaye ana W/C moja tena KWA goli LA mkono afu wamnyime MTU mwenye W/C tatu na magoli 1800 mfyuuuu shame on you

Unasema watu wengi hawakumuona pele...wewe ulimuona? Si umecheki video zake!! Na Diego si hivyo hivyo!! Ingawa Diego amecheza mda mfupi sana ukilinganisha na Pele. Mimi mwenyewe nimezishuhudia video zao yani Pele hagusi kwa Diego mkuu...na Kumbuka 4 years Diego hakucheza.

Swali! Pele kachukuwa world cup ngapi akiwa ndani ya uwanja? Na je Ili niamini kama nikweli kachukua world cup 3 naomba Niwekee link au video hapa ikimuonyesha ni yeye kweli ndiye kaifungia timu yake katika hizo final 3 na kubeba ndoo zote hizo ama wakina Garincha???...1958, 1962 na 1970.

Naomba jibu sahihi na usipindishe hata kidogo!
 
Kama ni hivyo,basi hao wote umeo wataja,wamecheza enzi ambazo sheria za Moira azijaimarika KWA mfano maradona mwaka wa 1980,but reality sheria zimeanza kuimprove miaka ya2000 ok


Kumbe wewe ni dogo kihivyo....Maradona alianza kuwika toka mwaka 1977 ila alitamba zaidi kuanzia mwaka 1984 mpaka 92. Maradona wa 1986 huwezi fananisha na Pele kwani alikuwa juu mno kimpira.
 
MKUU,,, takwimu ndy zinaongea kwamba PELE NDY mchezaji BORA WA KARNE hii ambaye hajapata kutokea,,, takwimu hizo hajaweka YEYE,,, majibu yote ingia GOOGLE utayapata,,, kwnz jiulize,,, PELE amecheza mpira wakati UBAGUZI wa RANGI DUNIANI umeshamiri,,, lakini WAZUNGU wamemvulia KOFIA,,,tena AMECHEZA MPIRA wakati mpira ni zaidi ya FUJO UWANJANI,,, sio wachezaji wa leo ukimgusa UNAPEWA KADI,,,, wakati huo KADI PIA HAKUNA,,, KIPA KUKURUKIA MGUU WA SHINGO ni KWENYE harakati za kufunga ni kawaida,,, BEKI kukutia DOLE,, KUKUFANYIA RAFU ukiwa hata hujashika mpira,,, au una mpira,,, pia sawa tu,,, Na hao akina MESSI,,,RONALDO,, maradona,, wote hawamfikii PELE,,,, kwahyo mkuu unataka kusema kama MCHEZAJI hajaifungia timu goal lakini AMEPIGA ASSIST PIA HAJASAIDIA timu? wewe hujamuona PELE,, wala hushughuliki na habari za PELE kuzitafuta,, unayokataa kwa PELE LEO,, kesho kuna VIZAZI vitakataa kwa MESSI NA RONALDO,,,kwamba WALIKUWA HAWANA LOLOTE,, , fuata takwimu mkuu,,,, ukiambiwa PELE alikuwa Anajuwa ELEWA ANAJUWA KWELI,,,PELE WAS A KING OF FOOTBALL, , style zote za MAGOLI,,, CHENGA zote unazoziona leo kwa akina MESSI,, NA RONALDO,,,, ni marudio tu ya PELE,,,, kuna Uzi ulishawahi kuwekwa humu kuhusu PELE,,, ungebaki mdomo wazi,,,,
 
ASANTE SANA MKUU NAONA UMEMALIZA AWEZII KUBISHA TENA,KWA HIYO FACT THANKS.
 
Badilisha kichwa cha thread yako hasa neno "atatokea." [Hakuna mchezaji ambaye atatokea katika hii dunia kama mnyama Pele the don(black mamba) record hazidanganyi]. Wewe umejuaje kama hatatokea wa mfano wa Pele au zaidi ya Pele wakati life span yako ni fupi kuliko ya dunia. Je, kama ufundi wa Pele ni genetic, hakuna uwezekano wa hiyo gene kujirudia endapo Pele ana watoto?
 
Hapana mkuu umechemka

Pele official records ana magoli zaidi ya 1000 mechi zinazotambuliwa na Fifa

World cup 3 alicheza zote alikosa tu mechi za mtoano 1962 baada ya kuumia game ya kwanza

Mchezaji bora wa karne walishare sababu maradona alishinda kura za mashabiki ambao wengi wao walikuwa watoto na walimshuhudia maradona akicheza ila pele walimsoma magazetini tu ila ilipoitwa kamati ya wataalamu na makocha wa timu za taifa ikampigia kura pele so unaweza kuona wataalam na mashabiki nani wa kuconsider

Sio hiyo tu hata UN ilimtaja kma mwanamichezo bora wa karne, pia kamati ya olympic ilimpa tuzo ya mwanamichezo bora wa karne bila kusahau shirikisho la wachezaji wa zamani nao walimpa ushindi pele kwa kura zaidi ya 90%

Kwa ufupi hakuna mchezaji ulimwenguni kama pele na hatowahi tokea tofauti hakukuwa na kiki kama sahivi na wengi wenu hamkuona akicheza ni vizuri uingie website za ESPN classic utakuta archive za mechi za dakika 90 kabisa za pele timu ya taifa na klabu ndio utaelewa nachosema hivyo viclip vya youtube hata Giroud huonekana kama mungu maana wanachukua best moments pekee

By the way pele kastaafu na miaka 29 huyo maradona kafika hadi 34 tena alistaafishwa kwa lazima huku hajafikia hata robo ya mafanikio ya pele so usiwalinganishe kabisa hawa jamaa ni matusi kwa pele
 
Individual performance maradona??? Kivipi wakati akicheza world cup ya 1982 alikuta kikosi kilichoshinda 1978 world cup bado kipo??? Yaani ni sawa na neymar aende madrid leo alafu useme ameipa kombe individually?? Seriously??

Unamuacha wapi buruchuga,kempes,valdano na grocochea???

Kuhusu Pele licha ya kuanza robo fainali ila alifanya impact alifunga throughout mpaka fainali wakabeba kombe mbona maradona husemi 1986 world cup kaja kufunga goli la kwanza robo fainali??? Ilihali alicheza tokea game ya kwanza??

Maradona anamzidi pele spidi na chenga kidogo ila mengine yote hamkuti kabisa zaidi wazungu wanampaisha sababu ya ubaguzi wa rangi and as u know maradona alicheza ulaya ila pele aligoma

Pele is pele while maradona is a soccer player!! Ndio maana hata muhammad ali alijiita pele wa boxing.......
 
Walikuwa hawajui mpira duh embu acha utani?? Timu zilivyokuwa zinajituma enzi zile unasema walikuwa hawajui mpira?? Katafute documentary ya 1954 world cup uone watu walivyokuwa wanafia uwanjani

Kuna kipa mmoja wa uruguay alikuwa anacheza namba zaidi ya 5 yaani kipa ila timu ikizidiwa anaingia kucheza kma beki baadae midfield n.k sahivi wapo wa hivyo??, kuna mechi nakumbuka brazil na poland iliisha 4-4 baada ya extra time ikaamuliwa irudiwe kesho yake asbuhi kwa vikosi vilevile vilivyocheza jana usiku na bado mechi ikapigwa na mshindi ndio akapatikana!!!

Zamani walikuwa wanajituma sana pesa kidogo ila uzalendo mbele sio siku hizi unakuta Christiano Ronaldo anahamia barcelona kisa pesa enzi hizo kosa kubwa sana unaweza kuuawa mpira ulikuwa mpira kama vile dini au itikadi sahivi ni pesa yako tu so huwezi sema zamani viwango hakuna wakati mpaka sasa rekodi nyingi za wababe wa enzi hizo hazijavunjwa

Zico
Pele
Just fontaine
Ferenc puskas
N.k

Hao rekodi zao hazivunjwagi kwa miaka zaidi ya 60 sasa alafu ndio unasema hawakuwa na viwango ilihali sahivi miaka 10 ballon dor inachukuliwa na wachezaji wawili pekee ila enzi hizo competition kubwa ukibeba ni ngumu kuipata tena
 
hata ccm huiba kura lakini wanatangazwa washindi,aliyetangazwa na mamlaka ndie mshindi.kwa sasa tukifuata sayansi kwa maana ya takwimu ronaldo wa madrid ndio zaidi.hutaki k....nya.
 
Unamzungumzia pele huyu huyu mwenye assist 10 na goli 12 katika mechi 14 za kombe la dunia, ama kwa hakika ww pele hujamfatilia vizuri, pele huyu huyu ambae nchi yake ilimmention as a national treasure ili asipate kwenda nje ya brazil

Kabla ya kumwaga data nyingi, nikuulize kidogo hiv hawa wa kina didi,vava, garincha, jarzinho na wengineo kina gerson si walikuwepo, why pele apate kurise mbele ya kundi hilo, mie najua ww hujafatilia, ulichokiandika ni umekiokota katika blogs za wasiompenda babu pele mie nawaita ant pele
 
Hhmmm... Mkuu tusiongopeane bhana, nianze kukusahihisha katika worl cup ya 58 kwanza nikwambie kabisa pele hakiwa mtu wa benchi ila alikwenda sweden hali yakiwa ni majeruhi na katika kuitwa kwale ni wachezaji ndio walipendekeza na kusimamaa kidete pele aende bila shaka hapo utajua ubora wa pele mpaka wenzie wamemganda ukizingatia alikuwa bwamdogo..

Pia pele hakuanzi katika robo huo ni uongo mechi ya kwanza pele alicheza ilikuwa mechi ya makundi brazil vs ussr(soviet union) nahisi ilikiwa ni mechi ya mwisho kwa makundi hapo alikiwa kapona majeraha yake.. The rest is history..

Robo fainali alicheza brazili vs wales nar akifunga goli pekee lililolipeleka brazil nusu fainali

Nusu fainali alicheza. Vs france na akapiga hat trick safi kabisa, akawa kijana mdogo kufanya hivyo ktk world cup akiwa na miaka 17

Fainalo akatupia 2


Haya unasemaje kuwa 58 pele alinenwa kama si yeye tena mtoto mdogo kubeba wenzie.. Fix hatupendi.
 
Labda nikurekebishe kidogo mkuu... Maradona hana chochotr cha kumzidi messi, labda kutumia midawa yake huyo maradona tu hajamzid andunje messi itakuwa pele, hapa nazungumzia si kwa speed, vyenga, ufundi, crrativity, playmaking na kufunga..
Mimi nimemfatili vizuri sana pele nimepoteza muda wangu kumtizama, pele si wa mchezo mchezo kaka, kwanza ana speed, pili ana stamina za kutosha, kajitu ka futi 5 na inchi kadhaa kalikuwa kanaenda hewan ma kupiga magoli ya kichwa bila wasi, alikiwa anaitumia miguu yake yote miwili ipasavyo kama unavyomuona roboti ronaldo


We bwana we hv unamjua pele vizur in brother k's voice
 

Brazil ingelichukua taji la 1958 na 1970 Hata kama pele asingelikuwemo. NA uthibitisho pale hakucheza mechi nyingi 1962 na timu ilkua bingwa. Mimi sipingi uwezo wa pale. Pele nikatika wachezaji bora kabisa waliowahi kutokea. Ninachopinga mimi ni kuzidisha kumuoverate katika baadhi ya mambo. Moja likiwemo hili lakuaminishwa ulimwengu kua aliipa Brazil mataji matatu ya Dunia. Garincha alikua bora zaidi ya pele kwenye 1958 world cup. na kuhusu 1962 hakuna kilichojificha linafahamika. Lakini je Dunia inamzungumza wapi Garincha? kwanini mambo aliyoyafanya kwenye ulimwengu wa soka yamefungiwa macho? Utakuta unaekewa list wachazaji bora hata 20 hukuti jina lake wakati ndani yake unakuta mpaka vibade kina CR7 ndani. Pele alifunga magoli 6 kwenye world cup. halikua jambo dogo na hasa kwa umri wake alikuanao Lakini garincha ndie aliefanya mambo makubwa zaidi kwenye pich. Na laziada nafikiri pia unafaham kama jamaa alikua ni mgonjwa wa akili kidogo. Sasa vuta picha angelikua mzima kabisa angelikuaje. na sina haja ya kuyazungumzia ya 1970. Usitizame statistic katafute record za mechi utizame. Ukitizama statistic unaweza kukuta Thomas muller ni zaidi ya Maradano. Lakini kiuhalisia je ni kweli?
Na jengine Pele magoli yake official hayakufika hata 800. Ayo elfu naa tunayoambiwa ni yapamoja na ya mechi ya vichochoroni na friend matches za vilabu ambazo kisheria hazitambuliki kwenye fifa.
 

Maradona alkua wa aina yake. Usimfananishe kabisa na kina Messi.
 

Nashukuru atleast soka unajua.. Uchawi umechanganya mambo mengi kwa wakati mmoja hvyo nitshindwa kukujibu kwa mtirirko mzur tuanze hapo na kusema pele amewapa brazili makombe matatu hapo naona shida ni kiswahili, pele hakuwapa brazili world cup 3 ila pele ni mshindi wa world cup3, mchango wake mkubwa kabisa ulikuwa ni katka 58 na 70, 62 aliumia katika game na chechzlovakia wakati akijaribu kupiga shuti, so pele ni mshindi wa makombe 3 ila mwenyewe mchango wake mkubwa ni katka mawili..
Nachelea kusema bila mchango wa pelee 58 na 70 brazil kombe yawezekana wangeisikia katika bomba kaangalie mchango wake(goals na assist katika world cup ya 58 na 70).. Kama brazil ilikiwa inajiweza bila ya pele mbona 66 ilitoka kiaibu baada ya pele kuumia..tukubaliane kwanza ushind wa timu ni mchango wa wachezaji 11 japo wapo wachache au m1 atang'ara zaidi ya wenzie..
Unajua km 66 pele ndio alikuwa mchezaji aliyechezewa rafu mbaya mnoo kiasi kasema hatcheza tena worl cup, ila 70 aliombwa ashiriki na kwa mara ya kwanza world cup kukawa na kadi nyekundu na njano.

Halafu hili suala la magoli ya pele linawaiza watu vichwa bure ubora wa pele si kufunga tu pekee, pele alikuwa zaidi ya mfungaji alikuwa ni mchezaji mtimilifu anavitu vyote, skills, creativity, stamina, power, dribling na kila kitu, hapo mdio maana nasema pele ni bora kwangu si bora sababu anafunga tu la hasha..

Sasa tuje kwenye magoli, hiv mfano barcelona wakicheza exhibition game na yanga messi akafunga goli 2 zinakuwa hazihesabiki, inakuwa hajawafungia barcelona, same to pele kuna goli 18 wameziommit toka katika idad ya magoli yake katika national team badala ya 95 iko 77, sasa swali la kujiuliza hizi goli alifunga akiwa kavaa jezi za nani yanga, au alikiwa mazoezin, jibu zilikiwa ni mechi zilizoandaliwa kabisa na kufahamika..

Ahsante mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…