Rais William Ruto amesema hakuna Mkenya anayepaswa kupoteza maisha, uhuru au heshima yake kwa sababu tu ya kuikosoa serikali, kutoa maoni yasiyopendwa na wengi au kushiriki maandamano ya amani.
Akizungumza katika Kongamano la 16 la Katiba lililofanyika KICC, Nairobi, Agosti 27, 2026, Ruto alisema maandamano ya amani, ukosoaji na kutokubaliana na serikali ni sehemu muhimu ya demokrasia.
Akirejelea maandamano yaliyoongozwa na vijana wa Gen Z mwaka 2024, Rais alisema madai yao kuhusu uwajibikaji, utawala bora na nafasi kubwa katika kuamua mustakabali wa taifa hayapaswi kutazamwa kama shambulio dhidi ya demokrasia.
Ruto pia alikiri kuwa familia kadhaa zilipoteza wapendwa wao huku madai ya kukamatwa kinyume cha sheria, watu kupotezwa kwa lazima na matumizi kupita kiasi ya nguvu yakitolewa. Alisema madai yoyote ya kuaminika ya ukiukaji wa haki za binadamu yanapaswa kuchunguzwa kwa uhuru, kikamilifu na kwa uwazi.
Hata hivyo, alisisitiza kuwa haki ya kuandamana hailindi vitendo vya vurugu, uporaji au uharibifu wa mali.
Baada ya yaliyoshuhudiwa kwenye maandamano ya miaka ya hivi karibuni, je, kauli hii ya Rais Ruto inaashiria mabadiliko katika namna serikali itakavyoshughulikia maandamano yajayo, au Wakenya watasubiri kuona matendo?