Hakuna mkoa mzuri wa kuishi kama Mbeya hapa Tanzania

Haku mipango mji wanajenga hovyo saaana
 
Tulia uandike vizuri
 
Kwa hili uko sahihi kabisa. Baada ya Mjerumani kupanga mji Sokomatola, Nonde, Ghana na Uhindini, serikali ikaja kupanga kidogo Block T, Q na X. Baada ya hapo wakazembea mpaka mji ikaharibikia Makunguru, Ilemi, Simike, Ilolo na Isanga. Wamekuja kushituka hapa majuzi na kuanza kupima Isyesye, Iwambi na Nsalaga. Kwenye mipango miji mbeya wamekwama sana. Waliojitahidi kupanga miji Nyanda za juu Kusini ni ji wa Vwawa na Sumbawanga mjini. Tunduma ni mji takataka kama ilivyo Ilemi.
 
Haya uliyoyasema ndo yalinikuta nilipofika mbeya.
..
 
Mbeya haifai kuitwa hata manispaa
Jiji gani CBD haijulikani ipo wapi hamna mishe mishe hata kidogo watu wake wamekaa kilugaluga, hakuna vibes wala mipango miji, hakuna sehemu ya starehe zaidi ya vilabu vya gongo, huwez kujua kijana ni yupi mzee ni yupi wote wanavaa mibwanga tu, kilugha kila mahali, nyumba za tope adi katikati ya mji, ni tabu na kelele za mabajaji kila kona, poor city, poor mbeya.
 
πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€
 
Mbeya raha ,Mbeya Ina Suburban 4

Uyole, Mwanjelwa, uhindini na Mbalizi zote ni πŸ”₯πŸ”₯πŸ”₯
 
Mbeya haifai kuitwa hata manispaa
Naona haters mnafarijiana ila Cha kufanya hamna 😁😁
 
Mbeya ingepata planning za maana, kwa kweli kwa hali yake ya hewa na productivity, ingekuwa kweli haishikiki. Halafu mbali na mipango miji lkn hata wananchi wenyewe hawaachiani space za mawasiliano ardhini. Sijui wanategemea tutembee kwa nyungo?
 
Mahindi 27000 kwa sasa mbeya, viazi 12 ndio, Mchele hadi 60 kwa ndoo maisha ni magumu mbeya kwa sasa
 
Shule za international zipo nyingi nyingi kwa sasa na zinafanya vizuri sana tu, ukiachana na za hapa mjini za wilaya nyingine pia
 
Mbeya ni mkoa wa tatu ukitoka iringa, njombe inafuata mbeya kwa kuwa na watoto na watu wenye udumavu na unyafuzi na viribatumbo na kwarshiokor.
Takwimu hizo umezitoa wapi? Yaani Mbeya kuna unyafuzi watoto. Ficha chuki zako dada
 
Umefafanua vizuri sana mkuu mpaka nimetamani kuhamishia huko hii biashara yangu ya majeneza
Vipi mzunguko huko utakuwa vizuri ?
Isije ikanitokea kama kipindi kile nilipoenda kujaribu hii biashara Zanzibar ikawa misiba mingi ni ya waislamu tu mpaka mtaji wangu ukayumba na kahela kenyewe ka mkopo[emoji848]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…