Hizo picha za barabara unazoweka humu ni za zamani nadhani 2014, sasa hivi barabara zote za mjini ni mashimo kwa mahandaki makubwa makubwa..
Mtoa mada unadanganya kwa faida ya nani?kwanini usirushe hali halisi ya barabara za sasa ili hata serikali ione aibu iliyopo Mbeya upande wa barabara?
Umefikia hatua umerusha hadi picha za msitu wa sao hill uliopo Iringa unadanganya kuwa ni Mbeya,lengo lako nini?
Unasema Mbeya ni mkoa wa pili kwa idadi ya mabasi yanayofanya safari zake kutoka Mbeya kwenda wapi sijui...sina takwimu siwezi kukupinga ila kama ni mabasi yaendayo Dar ( kama ulimaanisha hayo) ni machache sana.labda kama ulimaanisha hadi yale ya akina super rojas,mwendamseke,zanuni,fire, yote mafuso ya injini nyuma ambayo maeneo mengine ni daladala hizo wala siyo gari za route ndefu tena hizo.
Watu wamekuhisi humu kuwa una ushamba flani hivi utakuwa hujatembea maeneo mengine,nami naona ni kweli...nenda Mwanza uone basi za route fupi za Mwanza-Musoma, Mwanza-Tarime-Sirari, Musoma-Bukoba, Tabora,Kahama uone vyuma vinavyofanya safari zake huko,huwezi kuja kutuletea akina super rojas utaona aibu. Hapo hujagusa basi zinazofanya route za kutoka kote huko kwenda Dar,Dodoma,Arusha.
Ardhi imebarikiwa sana,yaweza kuwa kweli, ila kwa maoni yangu,ardhi iliyobarikiwa ni ambayo ukipanda mazao hata bila kuweka mbolea,inakupa products nzuri tu,Mbeya hata mchicha bila UREA hupati kitu,mahindi ndiyo lazima uweke DAP kupandia,UREA kukuzia, SA na CAN kunenepesha punje, baraka za hiyo Ardhi ziko wapi? Wakati kuna maeneo Nyandoto Tarime huko watu wanavuna vizuri tu bila kuweka mbolea na wanalima mara mbili kwa mwaka wakati Mbeya ni mara moja kwa mwaka.
Mbeya ni pazuri ila sisi wana Mbeya tunapakuza sanaa kuliko uhalisia wake
Sent from my Infinix X650 using
JamiiForums mobile app