Hakuna mkoa mzuri wa kuishi kama Mbeya hapa Tanzania

Hakuna mkoa mzuri wa kuishi kama Mbeya hapa Tanzania

Mkoa wenyewe imejengwa hovyo hovyo hasa Mbeya mjini kuliko mkoa mwingine wowote hapa Tanzania.
Miundo Mbinu mibovu kuliko mkoa mwingine wowote.
Mbeya mjini wameharibu jiografia kwa kujenga hovyo hadi kwenye vimilima kama kile cha Ilemi, cha Simike! Skwataz everywhere.
Kumbe sie tunajua hii tuu
 
Mbeya haina mzunguko wa hela. Watu wengi wanalima na kuwa na chakula kupelekea mzunguko mdogo wa hela. Mbeya wanajenga holela kupelekea mji kuwa kama kijiji kikubwa. Mbeya imeshindwa hata na shinyanyanfa kwa moango mji.

Wasafa kama wazaramu wanauza mpaka barabara. Zaidi ya misosi Mbeya hakuna la maana. Naishi Mbeya si mzaliwa. Hela za madini sijui zinaendaga wapi hazionekani tofauti na Mwanza., unaona kabisa jinsi pesa za madini zinavyochangamsha mji.

Mbalali along the main road zaidi ya miaka 15+ pako vilevile hakuna mabadriko ya maana kama Njombe along the main road. Rungwe imejitaijidi sana.

Siongei ushabiki nimetembea zaidi ya mikoa 10. Dodoma sasa hivi kiujenzi opo vizuri ila sijajua mzunguko wa pesa.
Kinachoiangusha Mbeya wakulima wanauza mazao bei chini sana na kuishia kuwanufaisha wafanyabiashara wa mikoani.
 
Mkoa wa Mbeya umejaaliwa kila kitu unachokijua wewe..

Kwa hapa Tanzania sijaona Mkoa Mzuri wa Kuishi kushinda Mbeya..

1.Kiuchumi.

Mbeya ni ya 3 Kwa kuchangia pato la Taifa yaani GDP Tanzania.

Mbeya ni ya 3 Kwa kuwa na Watu wenye kipato kikubwa.

 2.Hali ya Hewa na Mandhari.

Mbeya Ina Hali ya hewa ya majira yote yaani Bariadi na joto na mvua ni uhakika sio tia maji tia maji kama Mikoa mingine.

3.Usafiri

Uwanja wa ndege wa Songwe
Usafiri wa Barabara kutoka Mikoa yote na Nchi jirani Kupitia Barabara kuu ya Tanzam.
Usafiri wa kwenye Maji via Ziwa Nyasa.
Pia Kuna usafiri wa reli nzuri kabisa unakufikisha Zambia kutokea Dar.

4.Kilimo.

Mbeya Ina Ardhi nzuri ya kulima Kila aina ya zao kuanzia mbogamboga,matunda,nafaka Hadi pareto na chai.

5.Madini

Mkoa una Kila aina ya Madini kuanzia Dhahabu za Chunya Hadi Makaa ya Mawe ya Kiwira bila kusahau Madini ya gas asilia ya CO2.

6.Nishati.,

Umeme ni WA uhakika unaozalishwa kutoka migodi ya Kiwira na Geothermal.

7.Utalii

Hapa kwenye Utalii ndio Kuna fursa nyingi maana sehemu kubwa ni underdeveloped.

Kuna Milima ya kawetere,bwawa la Mungu,Hifadhi ya Kitulo na pia unafika Kwa urahusi Ruaha au Katavi NP kutokea Mbeya.

8.Viwanda.
Kuna viwanda vya aina mbalimbali kama Saruji,vinywaji vikali na laini kama soda,bia,wine nk.
Kuna viwanda vya magodoro,vifaa vya ujenzi,home appliances nk.

Aisha kama unataka kujenga viwanda Kuna maeneo ya kutosha yametengwa Kwa Ajili hiyo.

9.Makazi na Accomodations.

Kuna fursa kubwa Bado ya ujenzi wa hoteli za kitalii na hoteli za kawaida maana ni Mkoa wa Biashara hivyo itakulipa.

Pia Hapa ni wewe tuu maana ujenzi wa Mbeya sio costful kama Mikoa mingine,unachagua ijengee tofauti au blocks au hata tofari mbichi udongo una nata vizuri kabisa..

10. Watu .

Mbeya Ina idadi ya watu zaidi ya mil.2.3 Kwa Mkoa mzima wanaokuhakikishia soko.

Aisha watu wake ni Wapambanaji ndio maana huwezi kusikia Mbeya ikitajwa kwenye mambo ya umaskini na shida ndogo ndogo,hawalalamiki kusubiria serikali.

Kiufupi hiyo ni summary ndogo sana Kati ya Mengi mazuri yaliyopo Mbeya,Karibuni sana Mbeya.



View attachment 2565116View attachment 2565117

We umeishi mikoa mingapi na hizo data zako za uongo. Unafahamu hata Tanzania ina mikoa mingapi, na waweza kuitaja? We ni wale hamjatoka nje ya mkoa.
 
Mkoa wenyewe imejengwa hovyo hovyo hasa Mbeya mjini kuliko mkoa mwingine wowote hapa Tanzania.
Miundo Mbinu mibovu kuliko mkoa mwingine wowote.
Mbeya mjini wameharibu jiografia kwa kujenga hovyo hadi kwenye vimilima kama kile cha Ilemi, cha Simike! Skwataz everywhere.
Not that bad,Tanzania Iko hovyo ukitoka Dodoma.

 
Back
Top Bottom