Mkoa wa Mbeya ni Kati ya Mikoa 5. iliyopo Nyanda za Juu Kusini sanjali na Mikoa ya Ruvuma,Iringa,Songwe,Njombe na Rukwa.Mbeya ilianzishwa mwaka 1961.
Mkoa wa Mbeya umejaaliwa kila kitu unachokijua wewe..
Kwa hapa Tanzania sijaona Mkoa Mzuri wa Kuishi kushinda Mbeya..
1.Kiuchumi.
Mbeya ni ya 3 Kwa kuchangia pato la Taifa yaani GDP Tanzania.
Mbeya ni ya 3 Kwa kuwa na Watu wenye kipato kikubwa.
2.Hali ya Hewa na Mandhari.
Mbeya Ina Hali ya hewa ya majira yote yaani Bariadi na joto na mvua ni uhakika sio tia maji tia maji kama Mikoa mingine.
3.Usafiri
Uwanja wa ndege wa Songwe
Usafiri wa Barabara kutoka Mikoa yote na Nchi jirani Kupitia Barabara kuu ya Tanzam.
Usafiri wa kwenye Maji via Ziwa Nyasa.
Pia Kuna usafiri wa reli nzuri kabisa unakufikisha Zambia kutokea Dar.
4.Kilimo.
Mbeya Ina Ardhi nzuri ya kulima Kila aina ya zao kuanzia mbogamboga,matunda,nafaka Hadi pareto na chai.
5.Madini na Nishati.
Mkoa una Kila aina ya Madini kuanzia Dhahabu za Chunya Hadi Makaa ya Mawe ya Kiwira bila kusahau Madini ya gas asilia ya CO2.
Umeme ni WA uhakika unaozalishwa kutoka migodi ya Kiwira na Geothermal.
6.Elimu.
Mbeya ni Kati ya Mikoa ya Wasomi hapa Tanzania.Mkoa wa Mbeya una vyuo Vikuu zaidi ya 5 mfano MUST,Mzumbe,CuCoM,Udsm,Tumaini,nk.
Mkoa una mamia ya vyuo vya kati na shule za kutosha eg St.Francis hivyo ni ideal pia Kwa issues za Elimu.
7.Utalii
Hapa kwenye Utalii ndio Kuna fursa nyingi maana sehemu kubwa ni underdeveloped.
Kuna Milima ya kawetere,bwawa la Mungu,Hifadhi ya Kitulo na pia unafika Kwa urahusi Ruaha au Katavi NP kutokea Mbeya.
8.Viwanda na Biashara.
Kuna viwanda vya aina mbalimbali kama Saruji,vinywaji vikali na laini kama soda,bia,wine nk.
Kuna viwanda vya magodoro,vifaa vya ujenzi,home appliances nk.
Aisha kama unataka kujenga viwanda Kuna maeneo ya kutosha yametengwa Kwa Ajili hiyo.
Mbeya ndio Kitovu Cha Uchumi wa Mikoa ya Nyanda za Juu Kusini.
9.Makazi na Accomodations.
Kuna fursa kubwa Bado ya ujenzi wa hoteli za kitalii na hoteli za kawaida maana ni Mkoa wa Biashara hivyo itakulipa.
Pia Hapa ni wewe tuu maana ujenzi wa Mbeya sio costful kama Mikoa mingine,unachagua ijengee tofauti au blocks au hata tofari mbichi udongo una nata vizuri kabisa..
10. Watu .
Mbeya Ina idadi ya watu zaidi ya mil.2.3 Kwa Mkoa mzima wanaokuhakikishia soko.
Aisha watu wake ni Wapambanaji ndio maana huwezi kusikia Mbeya ikitajwa kwenye mambo ya umaskini na shida ndogo ndogo,hawalalamiki kusubiria serikali.
Kiufupi hiyo ni summary ndogo sana Kati ya Mengi mazuri yaliyopo Mbeya,Karibuni sana Mbeya.
View attachment 2565116View attachment 2565117