Hakuna mkoa mzuri wa kuishi kama Mbeya hapa Tanzania

Hakuna mkoa mzuri wa kuishi kama Mbeya hapa Tanzania

Mkoa wenyewe imejengwa hovyo hovyo hasa Mbeya mjini kuliko mkoa mwingine wowote hapa Tanzania. Miundo Mbinu mibovu kuliko mkoa mwingine wowote.

Mbeya mjini wameharibu jiografia kwa kujenga hovyo hadi kwenye vimilima kama kile cha Ilemi, cha Simike! Skwataz everywhere.
Acha Uongo bhana
 
Mkoa wa Mbeya ni Kati ya Mikoa mitano iliyopo Nyanda za Juu Kusini sanjali na Mikoa ya Ruvuma, Iringa, Songwe, Njombe na Rukwa. Mbeya ilianzishwa mwaka 1961.

Mkoa wa Mbeya umejaaliwa kila kitu unachokijua wewe.

Kwa hapa Tanzania sijaona Mkoa Mzuri wa Kuishi kushinda Mbeya.

1. Kiuchumi
Mbeya ni ya 3 Kwa kuchangia pato la Taifa yaani GDP Tanzania.

Mbeya ni ya 3 Kwa kuwa na Watu wenye kipato kikubwa.

 2. Hali ya Hewa na Mandhari
Mbeya Ina Hali ya hewa ya majira yote yaani Bariadi na joto na mvua ni uhakika sio tia maji tia maji kama Mikoa mingine.

3. Usafiri
Uwanja wa ndege wa Songwe
Usafiri wa Barabara kutoka Mikoa yote na Nchi jirani Kupitia Barabara kuu ya Tanzam. Usafiri wa kwenye Maji via Ziwa Nyasa. Pia Kuna usafiri wa reli nzuri kabisa unakufikisha Zambia kutokea Dar.

4. Kilimo
Mbeya Ina Ardhi nzuri ya kulima Kila aina ya zao kuanzia mbogamboga, matunda, nafaka Hadi pareto na chai.

5. Madini na Nishati
Mkoa una Kila aina ya Madini kuanzia Dhahabu za Chunya Hadi Makaa ya Mawe ya Kiwira bila kusahau Madini ya gas asilia ya CO2. Umeme ni wa uhakika unaozalishwa kutoka migodi ya Kiwira na Geothermal.

6. Elimu
Mbeya ni Kati ya Mikoa ya Wasomi hapa Tanzania. Mkoa wa Mbeya una vyuo Vikuu zaidi ya 5 mfano MUST, Mzumbe, CuCoM, UDSM, Tumaini, nk.

Mkoa una mamia ya vyuo vya kati na shule za kutosha eg St.Francis hivyo ni ideal pia Kwa issues za Elimu.

7. Utalii
Hapa kwenye Utalii ndio Kuna fursa nyingi maana sehemu kubwa ni underdeveloped.

Kuna Milima ya Kawetere, bwawa la Mungu, Hifadhi ya Kitulo na pia unafika Kwa urahisi Ruaha au Katavi NP kutokea Mbeya.

8. Viwanda na Biashara
Kuna viwanda vya aina mbalimbali kama Saruji, vinywaji vikali na laini kama soda, bia, wine nk.
Kuna viwanda vya magodoro, vifaa vya ujenzi, home appliances nk.

Aisha kama unataka kujenga viwanda Kuna maeneo ya kutosha yametengwa Kwa Ajili hiyo.

Mbeya ndio Kitovu Cha Uchumi wa Mikoa ya Nyanda za Juu Kusini.

9. Makazi na Accomodations
Kuna fursa kubwa Bado ya ujenzi wa hoteli za kitalii na hoteli za kawaida maana ni Mkoa wa Biashara hivyo itakulipa.

Pia Hapa ni wewe tuu maana ujenzi wa Mbeya sio costful kama Mikoa mingine,unachagua ijengee tofauti au blocks au hata tofari mbichi udongo una nata vizuri kabisa.

10. Watu
Mbeya Ina idadi ya watu zaidi ya milioni 2.3 Kwa Mkoa mzima wanaokuhakikishia soko.

Aidha watu wake ni Wapambanaji ndio maana huwezi kusikia Mbeya ikitajwa kwenye mambo ya umaskini na shida ndogo ndogo,hawalalamiki kusubiria serikali.

11. Michezo na Burudani.

Mbeya Ina Wasanii wakubwa Toka kitambo ila icon ya Mkoa ni kina Sugu,VanBoy na Stamina.

Kwenye Michezo hapo ndio nyumbani hususani football.Mbega Ina Timu 3 Ligi kuu za Prisons,Ihefu,Mbeya City na Timu 3 Ligi daraja la kwanza za KenGold,Mbeya Kwanza na Tukuyu Stars.Na Ina Wachezaji Wakubwa wengi tuu na makocha.

Kiufupi hiyo ni summary ndogo sana Kati ya Mengi mazuri yaliyopo Mbeya,Karibuni sana Mbeya.





View attachment 2565251View attachment 2565252View attachment 2565253


1 Dar
2 Mwz
3 Mbeya
 
Jiji gani CBD haijulikani ipo wapi hamna mishe mishe hata kidogo watu wake wamekaa kilugaluga, hakuna vibes wala mipango miji, hakuna sehemu ya starehe zaidi ya vilabu vya gongo, huwez kujua kijana ni yupi mzee ni yupi wote wanavaa mibwanga tu, kilugha kila mahali, nyumba za tope adi katikati ya mji, ni tabu na kelele za mabajaji kila kona, poor city, poor mbeya.
Ni vizuri kwa CBD kutokuwa sehemu moja. Miji mingi ukitaka kwenda mjini labda benki lazima wote muende sehemu moja. Mbeya tofauti. Ukifika Uyole unapata kila kitu, benki maduka nk. Ukienda Kabwe hivyohivyo, ukienda mjini hivyohivyo, ukienda Mbalizi hivyohivyo. Hakuna ushamba wa eti naenda mjini.
 
L

Lete list ya international school mbeya mkoa tuone acha porojo
Na kukutoa ushamba. Shule za intrrnational wanasoma hasa watoto wa wageni, kama wafanyakazi wa ubalozini, makampuni ya nje nk. Na wanatumia mtaala wa kimataifa. Kama watu hao hawapo kwenye mji, shule ya kimataifa ya nini?
 
Kwani unadhani uongo?? [emoji23][emoji23][emoji23]
Mbeya tuko juu mawinguni.[emoji91]

Kitu kimoja kinachoiangusha Mbeya ni mpangilio wa majengo
Mipango miji sijui walikuwa wamelala,, nyumba zimejengwa hovyohovyo, kila mtu anajenga anavyojua bila hata kujali kuacha barabara.

Dodoma Kwa sasa wameipita Mbeya parefu sana kwenye kupangilia mji wao.


Vitu vingine vyote kuhusu Mbeya ni kweli.

Ukipita Mbeya-Kyela utaona maana halisi ya green city.

Mji wake hauonekani exactly Kwa sababu umefunikwa ma milima na miti.. ila ile milima ndio uzuri wenyewe.
 
Ni vizuri kwa CBD kutokuwa sehemu moja. Miji mingi ukitaka kwenda mjini labda benki lazima wote muende sehemu moja. Mbeya tofauti. Ukifika Uyole unapata kila kitu, benki maduka nk. Ukienda Kabwe hivyohivyo, ukienda mjini hivyohivyo, ukienda Mbalizi hivyohivyo. Hakuna ushamba wa eti naenda mjini.
Miji yote duniani ina CBD, mbeya huwez jua CBD ipo wapi? Mbona miji kama Mwanza na dar, ina cbd lakini kuna miji mingine mikubwa ndani ya jiji inayojitegemea kwa kila kitu.
 
Miji yote duniani ina CBD, mbeya huwez jua CBD ipo wapi? Mbona miji kama Mwanza na dar, ina cbd lakini kuna miji mingine mikubwa ndani ya jiji inayojitegemea kwa kila kitu.
Labda utoe Dar, miji karibu yote, maghorofa, biashara kubwa zimerundikana sehemu moja. Mfano jiji la Mwanza, ukitoka mjini kati, nje huwezi kutana na mji kama Mbalizi au Uyole. Miji iliyokamilika. Arusha, Moro mambo karibu yote ni hapo mjini. Hakuna mji wa nje ya CBD unaojielewa.
 
Labda utoe Dar, miji karibu yote, maghorofa, biashara kubwa zimerundikana sehemu moja. Mfano jiji la Mwanza, ukitoka mjini kati, nje huwezi kutana na mji kama Mbalizi au Uyole. Miji iliyokamilika. Arusha, Moro mambo karibu yote ni hapo mjini. Hakuna mji wa nje ya CBD unaojielewa.
Buzuruga, nyegezi, buhongwa na igoma hizo miji hazina huduma gani na zinawatu zaidi ya 60, 000 kila eneo hapo.
 
Back
Top Bottom