Hakuna mkoa mzuri wa kuishi kama Mbeya hapa Tanzania

Hakuna mkoa mzuri wa kuishi kama Mbeya hapa Tanzania

Niliaminigi maneno ya Wanyakyusa nikaenda huko 2009 nilikutana vumbi kama poda kipindi hiki watu wanakula nondo za utosi, saa moja jioni wote ndani ukitaka kwenda hata dukani inabidi uvae helmet kulinda fuvu.
Wapiga nondo, sijui sababu ilikuwa nini
 
Msipende sana mikoa yenye chakula kingi, hsina nxunguko wa hela. Mbeya, Songea, Rukwa, Kigoma, Kagera,Kilimanjaro.

Hio mikoa utashiba ila hela za maana hutashika. Mkoa unaopta ndizi 4 kwa mia mbili utatoboa hapo. Ili utoboe hio mikia inakubidi ulime usafirishe mikoa mingine.

Napingana na ushauri wako. Maisha sio chakuka bali ni hela, ukiwa na hela utanunua chochote.. Ili upate elfu 10 itabifi uuze sahani ngapi za chips au chane ngapi za nduzi!
Bila kusahau Morogoro
 
Mbeya ni namba 3 Kwa uchumi mkubwa Tanzania nzima sijui wewe unaongea nini..

Kagera ni Kati ya Mikoa inaingiza pesa nyingi za Kodi hapa Tanzania
 
Nimeishi ubaruku nikawa naenda mbeya kufuata spear za trakta lkn inasikitisha baadhi ya vifaa tulikuwa tunaagiza kutoka Arusha.nikaenda mpanda Katavi ukienda mbeya hivyo vifaa hamna ukiagiza Arusha kinakuja hivyo nikajua Mbeya agiza vyakula tu hapo utapata muda wowote lkn si vya viwandani nikaenda kuishi Arusha ndio nikaona Arusha ndio Mji wa kuishi kw kuwa kila kitu kipo ispokuwa gharama za mji huo ni ghali ikabidi nihamie Mbulu huko ni pazuri san ila baridi lake hatari utadhani upo ncha za kasikazini za Dunia likanikimbiza hata miezi 3 haikuisha kwa sasa karibuni Katesh Hanang hapa mazingira ni kati kw kati na mji upo katikati popote unaagiza bidhaa inafika iwe Dom.Arusha.Singida au Mwanza karibuni san muone mlima Hanang
 
Mbeya ni namba 3 Kwa uchumi mkubwa Tanzania nzima sijui wewe unaongea nini..

Kagera ni Kati ya Mikoa inaingiza pesa nyingi za Kodi hapa Tanzania
Soma vizuri uelewe. Kila mtu akiwa mkulima unategemea mzunguko wa hela uwepo ? Watu wanapenda kuishi Mbeya kwa sababu vyakula vipo bei chini. Inapelekea mzunguko wa hela uwe chini. Mbeya kila mkazi anawaza ajenge na gharama za kujenga zipo chini uategemea sekta ya nyumba itakuwa na faida na mzunguko wa hela ? Mbalizi unafyatua tofali mbichi unajengea bila hata kuzichoma wakati miji mengine utanunua kila kitu mpaka maji ya kujengea na bei ya kupanga au kuuza nyumba inakuwa juu.
 
Kwa nini mzunguko usiwepo? Haya mabilioni yanaenda wapi? 👇👇

View: https://www.instagram.com/p/DBlv10Kt_rE/?igsh=N21laGM4Y2RseTZy
 
Mkoa wa Mbeya ni Kati ya Mikoa mitano iliyopo Nyanda za Juu Kusini sanjali na Mikoa ya Ruvuma, Iringa, Songwe, Njombe na Rukwa. Mbeya ilianzishwa mwaka 1961.

Mkoa wa Mbeya umejaaliwa kila kitu unachokijua wewe.

Kwa hapa Tanzania sijaona Mkoa Mzuri wa Kuishi kushinda Mbeya.

1. Kiuchumi
Mbeya ni ya 3 Kwa kuchangia pato la Taifa yaani GDP Tanzania.

Mbeya ni ya 3 Kwa kuwa na Watu wenye kipato kikubwa.

 2. Hali ya Hewa na Mandhari
Mbeya Ina Hali ya hewa ya majira yote yaani Bariadi na joto na mvua ni uhakika sio tia maji tia maji kama Mikoa mingine.

3. Usafiri
Uwanja wa ndege wa Songwe
Usafiri wa Barabara kutoka Mikoa yote na Nchi jirani Kupitia Barabara kuu ya Tanzam. Usafiri wa kwenye Maji via Ziwa Nyasa. Pia Kuna usafiri wa reli nzuri kabisa unakufikisha Zambia kutokea Dar.

4. Kilimo
Mbeya Ina Ardhi nzuri ya kulima Kila aina ya zao kuanzia mbogamboga, matunda, nafaka Hadi pareto na chai.

5. Madini na Nishati
Mkoa una Kila aina ya Madini kuanzia Dhahabu za Chunya Hadi Makaa ya Mawe ya Kiwira bila kusahau Madini ya gas asilia ya CO2. Umeme ni wa uhakika unaozalishwa kutoka migodi ya Kiwira na Geothermal.

6. Elimu
Mbeya ni Kati ya Mikoa ya Wasomi hapa Tanzania. Mkoa wa Mbeya una vyuo Vikuu zaidi ya 5 mfano MUST, Mzumbe, CuCoM, UDSM, Tumaini, nk.

Mkoa una mamia ya vyuo vya kati na shule za kutosha eg St.Francis hivyo ni ideal pia Kwa issues za Elimu.

7. Utalii
Hapa kwenye Utalii ndio Kuna fursa nyingi maana sehemu kubwa ni underdeveloped.

Kuna Milima ya Kawetere, bwawa la Mungu, Hifadhi ya Kitulo na pia unafika Kwa urahisi Ruaha au Katavi NP kutokea Mbeya.

8. Viwanda na Biashara
Kuna viwanda vya aina mbalimbali kama Saruji, vinywaji vikali na laini kama soda, bia, wine nk.
Kuna viwanda vya magodoro, vifaa vya ujenzi, home appliances nk.

Aisha kama unataka kujenga viwanda Kuna maeneo ya kutosha yametengwa Kwa Ajili hiyo.

Mbeya ndio Kitovu Cha Uchumi wa Mikoa ya Nyanda za Juu Kusini.

9. Makazi na Accomodations
Kuna fursa kubwa Bado ya ujenzi wa hoteli za kitalii na hoteli za kawaida maana ni Mkoa wa Biashara hivyo itakulipa.

Pia Hapa ni wewe tuu maana ujenzi wa Mbeya sio costful kama Mikoa mingine,unachagua ijengee tofauti au blocks au hata tofari mbichi udongo una nata vizuri kabisa.

10. Watu
Mbeya Ina idadi ya watu zaidi ya milioni 2.3 Kwa Mkoa mzima wanaokuhakikishia soko.

Aidha watu wake ni Wapambanaji ndio maana huwezi kusikia Mbeya ikitajwa kwenye mambo ya umaskini na shida ndogo ndogo,hawalalamiki kusubiria serikali.

11. Michezo na Burudani.

Mbeya Ina Wasanii wakubwa Toka kitambo ila icon ya Mkoa ni kina Sugu,VanBoy na Stamina.

Kwenye Michezo hapo ndio nyumbani hususani football.Mbega Ina Timu 3 Ligi kuu za Prisons,Ihefu,Mbeya City na Timu 3 Ligi daraja la kwanza za KenGold,Mbeya Kwanza na Tukuyu Stars.Na Ina Wachezaji Wakubwa wengi tuu na makocha.

Kiufupi hiyo ni summary ndogo sana Kati ya Mengi mazuri yaliyopo Mbeya,Karibuni sana Mbeya.

Pia Soma Tukuyu, Rungwe Mbeya wilaya ya kipekee sijaona Tanzania

Hii ya mwisho ni wapi hapo mkuu
 
Niliaminigi maneno ya Wanyakyusa nikaenda huko 2009 nilikutana vumbi kama poda kipindi hiki watu wanakula nondo za utosi, saa moja jioni wote ndani ukitaka kwenda hata dukani inabidi uvae helmet kulinda fuvu.
Hilo vumbi ndo rutuba ya ardhi,mambo ya nondo yashapita kitambo
 
Back
Top Bottom