Hakuna mkoa mzuri wa kuishi kama Mbeya hapa Tanzania

Hakuna mkoa mzuri wa kuishi kama Mbeya hapa Tanzania

Unakuta mtu akipiga picha za kwao hapafai maendeleo ziro alafu anakuja kuponda vitu Ambavyo haviendani kabisa mbeya pazuri na sehemu nyingi bongo ni nzuri basi tu hatuna mipango mizuri ya miji ila sio kupondea kama ndio jalalani vile na chunguza wanaoponda sana ukihoji katokea singida vijijini unamuonea hadi huruma
Haters hao Wana wivu achana nao.

Mbeya
that_mbeya_guy_1680353128961733.jpg
that_mbeya_guy_1680353066234609.jpg
20230404_190657.jpg
20230404_190701.jpg
20230404_190556.jpg
 
Acha chuki wapi pamejengwa vizuri tz nzima ni yale yale ila mbeya wnaajitahidi hata mazingira yanavutia
Siyo kama Mbeya. Wala sina chuki kwa sababu mwenyewe imebidi niwepo Mbeya. Hali ya hewa na tabia ya nchi ya Mbeya ni nzuri. Hilo liko wazi. Lakini watu wa Mbeya mnaharibu kwa kujenga vibaya kila kona.
 
Acha chuki wapi pamejengwa vizuri tz nzima ni yale yale ila mbeya wnaajitahidi hata mazingira yanavutia
Miji kama Dodoma, Singida, Babati, Sumbawanga, Mpanda, Vwawa, Iringa, Morogoro inazidi Mbeya pakubwa sana kwenye mipangilio ya mji na miundo mbinu. Hata majengo. Mbeya mnajenga kwa matofali ya matope(mabichi). Mji hauna majengo ya maana kama miji mingine mikubwa.

Hata Arusha iko beautiful kwa majengo na hata kwa mandhari kuliko Mbeya. Na kama umewahi kufika Tengeru, Njiro, Sakina, Sanawari, Moshono, huwezi kusema Mbeya imeizidi Arusha hata kwa tabia ya nchi.
 
Ya nini kujidanganya hali ya mji kama Mbeya? Inahitajika kupangwa upya. Hatupaswi kutegemea uzuri wa asilo wa hali ya hewa. Miji yetu inahitaji uzuri wa kutengenezwa kwa kuweka miundo mbinu ya maana ili iweze kuvutia uwekezaji wa biashara kubwa kubwa.

Imagine mji mnauona mkubwa kama Mbeya lkn haina Supermarket hata moja.
 
Mji mzima una kile minisumarket vipodozi ya SH Amon pale mataa ya junction ya Mafiat.
 
Miji kama Dodoma, Singida, Babati, Sumbawanga, Mpanda, Vwawa, Iringa, Morogoro inazidi Mbeya pakubwa sana kwenye mipangilio ya mji na miundo mbinu. Hata majengo. Mbeya mnajenga kwa matofali ya matope(mabichi). Mji hauna majengo ya maana kama miji mingine mikubwa.
Hata Arusha iko beautiful kwa majengo na hata kwa mandhari kuliko Mbeya.
Na kama umewahi kufika Tengeru, Njiro, Sakina, Sanawari, Moshono, huwezi kusema Mbeya imeizidi Arusha hata kwa tabia ya nchi.
Natokea kaskazini miji yetu inajulikana bhana Mbeya sio mbaya, Arusha kupata barabara juzi tu leo mji mzuri miji yote tia maji tia maji hakuna miji tunachoshana tu na sikusema Mbeya nzuri kuzidi sehemu fulani ila Mbeya sio pakuponda hata Dar jiji kuna nyumba za tope mpaka leo Arusha zipo za tope kibao mjini lazima mabadiliko yawepo ila tofautisha jiji na miji.
 
Siyo kama Mbeya. Wala sina chuki kwa sababu mwenyewe imebidi niwepo Mbeya. Hali ya hewa na tabia ya nchi ya Mbeya ni nzuri. Hilo liko wazi. Lakini watu wa Mbeya mnaharibu kwa kujenga vibaya kila kona.
Usilaumu watu kwani hakuna wanaopanga miji mifumo yetu kibongo bongo hakuna jipya kuchoshana tu
 
Siyo kama Mbeya. Wala sina chuki kwa sababu mwenyewe imebidi niwepo Mbeya. Hali ya hewa na tabia ya nchi ya Mbeya ni nzuri. Hilo liko wazi. Lakini watu wa Mbeya mnaharibu kwa kujenga vibaya kila kona.
Ni kama wapi? Wapi mnakojenga vizuri?
 
Mkoa wa Mbeya ni Kati ya Mikoa mitano iliyopo Nyanda za Juu Kusini sanjali na Mikoa ya Ruvuma, Iringa, Songwe, Njombe na Rukwa. Mbeya ilianzishwa mwaka 1961.

Mkoa wa Mbeya umejaaliwa kila kitu unachokijua wewe.

Kwa hapa Tanzania sijaona Mkoa Mzuri wa Kuishi kushinda Mbeya.

1. Kiuchumi
Mbeya ni ya 3 Kwa kuchangia pato la Taifa yaani GDP Tanzania.

Mbeya ni ya 3 Kwa kuwa na Watu wenye kipato kikubwa.

 2. Hali ya Hewa na Mandhari
Mbeya Ina Hali ya hewa ya majira yote yaani Bariadi na joto na mvua ni uhakika sio tia maji tia maji kama Mikoa mingine.

3. Usafiri
Uwanja wa ndege wa Songwe
Usafiri wa Barabara kutoka Mikoa yote na Nchi jirani Kupitia Barabara kuu ya Tanzam. Usafiri wa kwenye Maji via Ziwa Nyasa. Pia Kuna usafiri wa reli nzuri kabisa unakufikisha Zambia kutokea Dar.

4. Kilimo
Mbeya Ina Ardhi nzuri ya kulima Kila aina ya zao kuanzia mbogamboga, matunda, nafaka Hadi pareto na chai.

5. Madini na Nishati
Mkoa una Kila aina ya Madini kuanzia Dhahabu za Chunya Hadi Makaa ya Mawe ya Kiwira bila kusahau Madini ya gas asilia ya CO2. Umeme ni wa uhakika unaozalishwa kutoka migodi ya Kiwira na Geothermal.

6. Elimu
Mbeya ni Kati ya Mikoa ya Wasomi hapa Tanzania. Mkoa wa Mbeya una vyuo Vikuu zaidi ya 5 mfano MUST, Mzumbe, CuCoM, UDSM, Tumaini, nk.

Mkoa una mamia ya vyuo vya kati na shule za kutosha eg St.Francis hivyo ni ideal pia Kwa issues za Elimu.

7. Utalii
Hapa kwenye Utalii ndio Kuna fursa nyingi maana sehemu kubwa ni underdeveloped.

Kuna Milima ya Kawetere, bwawa la Mungu, Hifadhi ya Kitulo na pia unafika Kwa urahisi Ruaha au Katavi NP kutokea Mbeya.

8. Viwanda na Biashara
Kuna viwanda vya aina mbalimbali kama Saruji, vinywaji vikali na laini kama soda, bia, wine nk.
Kuna viwanda vya magodoro, vifaa vya ujenzi, home appliances nk.

Aisha kama unataka kujenga viwanda Kuna maeneo ya kutosha yametengwa Kwa Ajili hiyo.

Mbeya ndio Kitovu Cha Uchumi wa Mikoa ya Nyanda za Juu Kusini.

9. Makazi na Accomodations
Kuna fursa kubwa Bado ya ujenzi wa hoteli za kitalii na hoteli za kawaida maana ni Mkoa wa Biashara hivyo itakulipa.

Pia Hapa ni wewe tuu maana ujenzi wa Mbeya sio costful kama Mikoa mingine,unachagua ijengee tofauti au blocks au hata tofari mbichi udongo una nata vizuri kabisa.

10. Watu
Mbeya Ina idadi ya watu zaidi ya milioni 2.3 Kwa Mkoa mzima wanaokuhakikishia soko.

Aidha watu wake ni Wapambanaji ndio maana huwezi kusikia Mbeya ikitajwa kwenye mambo ya umaskini na shida ndogo ndogo,hawalalamiki kusubiria serikali.

11. Michezo na Burudani.

Mbeya Ina Wasanii wakubwa Toka kitambo ila icon ya Mkoa ni kina Sugu,VanBoy na Stamina.

Kwenye Michezo hapo ndio nyumbani hususani football.Mbega Ina Timu 3 Ligi kuu za Prisons,Ihefu,Mbeya City na Timu 3 Ligi daraja la kwanza za KenGold,Mbeya Kwanza na Tukuyu Stars.Na Ina Wachezaji Wakubwa wengi tuu na makocha.

Kiufupi hiyo ni summary ndogo sana Kati ya Mengi mazuri yaliyopo Mbeya,Karibuni sana Mbeya.







Na vipi kuhusu vumbi lote hilo?
 
Pakis*nge niko hapa chuo cha MUST napakumbuka sana nyumbani Arusha.....
Kwani nani anahitaji kuona makanyagio Yako na meno yaliyooza? Uliitwa au kulazimishwa ?

Mbona mna kachuo kenu Kwa nini hukuenda kusoma huko?

Mbeya hatuvuti Bangi na Wala hakuna maisha magumu kama kwenu..

This is Mbeya
that_mbeya_guy_1680354519150294.jpg
that_mbeya_guy_1680354232894234.jpg
that_mbeya_guy_1680354176001634.jpg
that_mbeya_guy_168035300451845.jpg
that_mbeya_guy_1680353090037760.jpg
that_mbeya_guy_1680353491889397.jpg
that_mbeya_guy_1680352863324249.jpg
 
Tafuta hela Yani we tafuta hela usilale tafuta hela hata jangwani ukiwa na hela kuzurii mfano dubai ni jangwa tupu leo ndio mji mzuri kushinda Tz kwenye Kila kitu nasemea ten na ten tafuta hela ukiwa na hela hamna sehemu mbaya
 
Back
Top Bottom