Toka karne nyingi zilizopita suala la ulipaji kodi limekuwa likikwepwa sana na raia wa mataifa mbali mbali hadi kupelekea kutungwa sheria kali za kuwabana walipa kodi.
Nchi yetu Tanzania ina nguvu kazi kubwa na hazina ya vijana ambao wengi hawashiriki kikamilifu kulipa kodi.
Mfumo wetu wa ulipaji kodi unawalenga tu wafanyabiashara wakubwa na wafanyakazi walio kwenye mfumo rasmi huku ikiwaacha mamilioni ya watanzania nje ya mfumo wa kodi.
Ukiacha VAT inayolipwa na wote kuna makundi mfano:-
Bodaboda hawalipi kodi, japo wanaingiza kipato kwa mwezi mara nyingine kuliko hata mwalimu.
Wamachinga zaidi ya mchango wa 20,000 za kipindi cha Magufuli hakuna kodi nyingine wanalipa.
Wakulima nao hali kadhalika, kodi zao ni kwa wakulima wakubwa tu ambao ni wachache mno.
Na hawa ni wengi sana. Je nchi itapigaje hatua bila kutafuta kodi itakayo wahusisha wote? Jibu ni rahisi maana asilimia kubwa ya hili kundi linatumia mitandao ya simu kufanya miamala basi tuwafuate huko huko.
Wanaopinga tozo za miamala Je mnataka nchi isonge mbele kwa kodi za nani?
Angalia toka asubuhi hadi jioni ni fedha kiasi gani umekatwa kama kodi na je zinatosha kukuletea huduma unazohitaji?
Rais Magufuli alikamua kodi mpaka mwisho lakini aliishia kupata 1.2 Trillion kwa mwezi ambazo hazitoshi kabisa.
Tutakapolipa wote kodi, uchungu wa kuzifuatilia utaongezeka na maendeleo yatapatikana. Kuliko wachache wanaumia kulipa kodi, wengine wanashinda instagram kupromote udaku.