Lucas Mwashambwa
JF-Expert Member
- Jul 28, 2022
- 28,722
- 20,610
Ndugu zangu watanzania,
Huo ndio ukweli kuwa kwa Sasa Hakuna mpinzani au mtu yeyote kutoka upinzani mwenye uwezo wa kushindani na Rais Samia Jukwaani Na hata katika sanduku la kura, kwa Sasa Rais Samia ndiye kiongozi mwenye ushawishi mkubwa Sana hapa Barani Afrika na ukanda huu wa Afrika mashariki.
Ni kiongozi ambaye Kuna nchi zinatamani angezaliwa kwao ili aweze kuwatumikia Kama ambavyo anatutumikia watanzania,wanatamani wapate kiongozi msikivu, mnyenyekevu,mchapa kazi ,mzalendo,mwana demokrasia,mwana diplomasia, mcha Mungu na mwenye hofu ya Mungu Kama Rais wetu.
Wanatamani wangekuwa na Rais Samia nchini kwao atakaye wasikiliza sauti zao na kuwatazama shida zao,lakini kwa bahati Nzuri Ni kuwa Rais Samia alizaliwa Tanzania na kuinuliwa na Mwenyezi MUNGU kwa ajili ya kuwatumikia Watanzania kutoka katika umaskini na kusonga mbele kimaendeleo na kiuchumi.
Ni kiongozi Ambaye watanzania wanatamani kumsikiliza muda wote,wanatamani kumuona akifika maeneo yao kwa kuwa wanajuwa Kuna Tumaini jipya juu ya kero na changamoto zao afikapo Rais wao, Wanajuwa kuwa watasikilizwa na kupewa majibu ya kuridhisha.
Kila anapokuwa mh Rais na kutoa hotuba yake inakuwa Ni hotuba iliyo jaa matumaini kwa watanzania wote,inakuwa Ni hotuba inayojibu maswali ya watanzania wote,anaweza akawa Dodoma lakini hotuba yake ikajibu maswali na kutoa matumaini kwa wakulima wa Mbozi mkoani Songwe au wafanyabiashara na vijana wa Tunduma mkoani Songwe.
Ni kiongozi ambaye maneno yake yanaponya wenye kuumizwa na kero mbalimbali,yanaleta faraja na matumaini kwa waliokata Tamaa,Yanaleta matumaini kwa walio poteza Dira,yanaamsha ari na nguvu ya kufanya kazi kwa walio nyong'onyea,Yanaleta ujasiri na kutia hamasa kwa walio kaa chini.
Rais Samia Amewafanya watanzania wasitamani hata kufanyika kwa uchaguzi maana wanaona Ni upotevu wa pesa kwa kuwa wameridhishwa na utendaji kazi wake na wangependa aendelee kuwatumikia kwa kuwa ameonyesha dhamira ya dhati katika kumfanya kila mtanzania awe na Tabasamu la kiuchumi na kumgusa kila mtu kiutendaji.
Kazi alizozifanya mh Rais ndani ya muda mfupi zimeikonga mioyo ya watanzania, Zimewagusa kila watu, zimeamsha matumaini katika kila secta, zimeleta amani na utulivu kwa watumishi wa umma, zimewainua na kuwaheshimisha wakulima na kilimo.
Zimeamsha matumaini kwa wanafunzi wanao pata Elimu bure,zimeleta Tabasamu kwa wafanya Biashara, zimekuwa chambo kwa wawekezaji na watalii kumiminika na kufurika nchini, zimeleta umoja na mshikamano miongoni mwa watanzania, zimeiheshimisha nchi yetu na kuifanya kuheshimika kimataifa.
Ni wapi na secta ipi ambako Rais Samia Hajafika? Ni Nani ambaye hajafikiwa na Rais Samia? Ni wapi na mkoa upi ambao haujapelekewa maendeleo na mabillioni ya pesa?
Ni mwananchi yupi ambayeAmeonewa au kuumizwa kimaneno na kimatendo na Rais Samia na serikali Yake? Ni Nani ambaye ndoto zake zinakwama kwa sababu ya serikali ya Rais Samia?
Kazi Iendeleee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na sauti.
Lucas Hebel Mwashambwa, kijana mzalendo na mpenda nchi yangu. 0742-676627