Hakuna mtu anayependa kuishi Uswahilini. Hata sisi Waswahili tunatafuta nyumba na viwanja mbali na Uswahili

Hakuna mtu anayependa kuishi Uswahilini. Hata sisi Waswahili tunatafuta nyumba na viwanja mbali na Uswahili

Sky Eclat

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2012
Posts
57,761
Reaction score
216,011
Uswahilini mnakokukimbia ni wapi? Inawezekekana mnakimbia kushirikiana jiko, choo na bafu kwanye nyumba ya kupanga lakini hata Manzese, Mbagala, Mwananyamala kwa Kopa Kinondoni Shamba kuna nyumba self contained na gate kabisa mlangoni, ukiingia na gari yako hakuna mtu anaejua maisha yako.

Nifundisheni huu uzungu unaofanya mkimbie Uswahilini. Huko Uzunguni kuna nini cha ziada? Au oxygen wanauovuta ni tofauti na hii ya kwetu?

Uzungu na Uswahili unaubeba mwenyewe na jifunze jinsi ya kuishi na watu wanaokuzunguka
 
Maisha ya uswazi yanachangamoto sana hasa kufatiliana, hii kero ndo ilinifanya niishi mitaa ya kishua japo kipato changu ni cha kati, aise mitaa ya ushuani ina raha sana mda wote upo huru na maisha yako, huku hakuna majungu yakifala kama uswaz.
 
maisha ya uswazi yanachangamoto sana hasa kufatiliana, hii kero ndo ilinifanya niishi mitaa ya kishua japo kipato changu ni cha kati, aise mitaa ya ushuani ina raha sana mda wote upo huru na maisha yako, huku hakuna majungu yakifala kama uswaz.
Kwahiyo sisi tunaokaa huku kwa mtogole itakuwaje sasa
 
Naturally Kuna watu wanapenda kukaa uswazi, Mwamnyange aliyekuwa msemaji was polisi alikataa kukaa Oyster Bay ushuani, sio kituo cha polisi akataka akae Buruguni, eti uzunguni atakuwa mpweke.
Hata town planners watoa viwanja vya low density na high density. Huku Uswazi tunaambukizana kila kitu hadi umbea.
 
Back
Top Bottom