Hakuna mtu anayependa kuishi Uswahilini. Hata sisi Waswahili tunatafuta nyumba na viwanja mbali na Uswahili

Kwangu uswahilini ni sehemu yeyote yenye makazi yasiyopimwa!! Sehemu ambayo haijapimwa imekaa hovyo hovyo unaweka dirisha lipo karibu na choo cha mtu au hakuna njia ya kuingia gari,hao wetu wenye mageti uswahili ni wale wenye kipato wamewavua watu viwanja vya pembeni yao ili kujivinjari.
 
Lakin semeni yote jamani uswahilini kuna raha yake, tukianza kuzitaja burudani zinazopatikana uswazi tutajaza nyuzi nyingi sana
 
Sky Eclat kama unaweza kuwaepusha watoto wako na maisha ya uswahilini, please fanya hivyo ndugu yangu.

Mimi nilikulia uswahilini kabla ya wazazi kuhamisha makazi mapya pahala pengine.

Asilimia 70 ya ambao nilisoma nao shule ya msingi katika mtaa ule kwa sasa ni mateja na walevi wa kutupwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…