Hakuna mtu anayeweza ku-hack WhatsApp yako

Hakuna mtu anayeweza ku-hack WhatsApp yako

Kuna taarifa nyingi za uongo mitandaoni, sijui meseji za WhatsApp zitasomwa na watu, sijui nini na nini!

Ngoja niwaambie jambo moja. Zuckerberg sio fala, hakuna mtu anayeweza kuingilia mawasiliano ya mtu mwingine. Hii mitandao ipo imara sana labda uhack, na mara nyingi kuhack hutumika Facebook, Instagram kwa kuwa tunatumia email ambapo hakupo very steong kiulinzi, ila huwezi kusikia mtu anasema WhatsApp yangu imehakiwa. Ukiona mtu anatumia Whatsapp yako basi jua kuna mahali ulijisahau, akaiunganisha na Whatsapp Web ama kuscan code.

Halafu ndio maana daily watu wanalizwa. Eti ukitaka kusoma meseji za mpenzi wako Whatsapp njoo tukusaidie... Ndugu zangu, mtaliwa sana pesa zenu.

BBM watu walidanganya kuingilia mawasiliano ya kimtandao tu Blackberry alikaa tumbo joto.

Jaribu kutafuta ile documentary ya Zuckerberg: King of the Metaverse usafishe kichwa.

Hakuna mtu yeyote ataweza kuingilia WhatsApp yako, ukiona kaweza, jua aliichukua simu yako kinyemela.

Zuckerberg sio fala.
sure,
Nakumbuka 2021-2022 pale Kenya baada ya Rais Uhuru kenyata na Naibu wake Ruto kutofautiana na bifu likawa so hot,.

Kutokuaminiana, kudukuana na kufuatiliana na kuchunguzana mawasiliono kukawa kwingi.
Ruto na camp yake waliamua kutumia WhatsApp, hususani video call zaidi. Huenda walibaini mtandaoni huu si rahisi mtu kuungilia na kudukua 🐒

Nadhani walifanikiwa na mpaka wakashinda uchaguzi na leo wameunda na kuongoza Serikali 🐒
 
Jidanganye!
Wataalamu wapo sana tena hata humu humu wamo!
Narudia tena, jidanganye!

Zingatia
Udukuzi na uhalifu kwa ujumla unahitaji gharama kubwa kwahiyo muda mwingine ukiona haiwezekani basi ujue cash imepungua!
Wapo mahackers wanaofanya hizo kazi,
Sema vifurushi vyao gharama ni kubwa.
 
Niunge kwenye kundi kisha nitoe....uone masaa mawili mengi narudi na nawaondoa ADMIN....kuna dogo wangu hata sijui anafanyaje fanyaje ila hiii michezo ni hatari kwa TCRA
Anatumia ile barcode au link
 
Mkuu inawezekana mimi mwaka huu january nilipiteza akaunti yangu ya whatsapp na ilichukulia na mgeni yaani alikua akipost na kuweka profile anavyotaka nikawa siwezi kufanya chochote nikaamua kuwaandikia whatsapp wenyewe ndo ikarudi kwangu.
 
sure,
Nakumbuka 2021-2022 pale Kenya baada ya Rais Uhuru kenyata na Naibu wake Ruto kutofautiana na bifu likawa so hot,.

Kutokuaminiana, kudukuana na kufuatiliana na kuchunguzana mawasiliono kukawa kwingi.
Ruto na camp yake waliamua kutumia WhatsApp, hususani video call zaidi. Huenda walibaini mtandaoni huu si rahisi mtu kuungilia na kudukua 🐒

Nadhani walifanikiwa na mpaka wakashinda uchaguzi na leo wameunda na kuongoza Serikali 🐒
Hata hapa kwetu viongozi wa upinzani wanatumia njia hiyo.
 
Kwa experience yangu ndogo,watu hua wanatumia features za whatsapp ambazzo wengine hawajazifatilia,mfano unaaweza kuweka namba yako kwa whatsapp kwa device zaidi ya moja....
Hapa wadau hutumia njia kadhaa kuiipata ile code ya kuingilia,
Pia kuna feature ya mtu kuipoteza namba yaani namba yangu ya whatsapp haipatikani nataka kuingia whatsapp....hizi ni njia za kawaida kabisa tuseme ni features za kawaida ambazo whatsapp na mitandao mingine wameweka ili kukusaidia mtumiaji...
KUHACK Ni jambo lingine kabisa,yaani kuhack akaunti ya mtu whatsapp ni jambo gumu kuliko ugumu...
ile wanasema end to end encryption....
Ni kitu ya msingi ambayo pia wanazitumia apps kama za tigopesa,m-pesa,crdb.....
Conclusion
unaweza kuhack whatsapp ila ni ugumu wake ni karibia impossible.
Naruhusu kusahihishwa🙏🏽
 
Sasa mie waki hack acc angu ya tsup watagundua nn cha maana? Zaidi watakuta text zisizofaa nazochat na Ba tamu, pia umbea na udaku naochat na mashogaree akee.

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
ila group wanahaki sana, wakikutoa unaweza to hack na kuwaondoa hata hao ADMIN
Tunaongelea Whatsapp account.... Sio group za Whatsapp, yani mtu adukue Account yako ya Whatsapp na kufanya atakacho au kukufatilia meseji zako bila kuwai kushika simu yako
 
Back
Top Bottom