Hakuna mtu asiye na Mapungufu, tusilaani Viongozi

Hakuna mtu asiye na Mapungufu, tusilaani Viongozi

BOB LUSE

JF-Expert Member
Joined
Jan 25, 2014
Posts
3,738
Reaction score
3,199
Nimeona Viongozi wa awamu mbalimbali nchini,kwenye kada tofauti,kasoro mkoloni.katika medani ya siasa na uongozi maeneo mbalimbali, wengi wao wamepata umaarufu baada ya kuondoka madarakani,walipigwa Kwa maneno magumu ya kuwalalamikiwa na kuwalaani wakiwa madarakani.

Kila mtu ni malaika akiwa Hana kazi,akipewa nafasi ya uongozi hatuangalii mazuri ya mtu,tunaangalia ubaya,Matokeo akiondoka kwenye nafasi,tunaangalia mazuri yake.

Watu wapewe maua yao mapema,sio wakifa.tukilinganisha tunaona ni wema Kuliko walioko madarakani! Usilaani,weka akina ya Maneno.
 
Kila mtu ni malaika akiwa Hana kazi,akipewa nafasi ya uongozi hatuangalii mazuri ya mtu,tunaangalia ubaya,Matokeo akiondoka kwenye nafasi,tunaangalia mazuri yake...
Mbona maua wanapewa sana mpaka inakua kero wanayakataa. Mama alisema hataki machawa maanayake ameyakataa maua. Huoni hata serikali siku hizi imekua ya mtu binafsi. Mara nyingi tumeskia serikali ya mh. fulani
 
Ndio maana watu wenye akili kama Plato alipendekeza kuwa nchi iongozwe na "mfalme Mwanafalsafa".Maana alitambua vema sio kila mtu anafaa kuwa kiongozi bali wachache.Tanzania wajinga ndio hupewa madaraka na wenye akili timamu kuwa wafuasi.
 
Ndio maana watu wenye akili kama Plato alipendekeza kuwa nchi iongozwe na "mfalme Mwanafalsafa".Maana alitambua vema sio kila mtu anafaa kuwa kiongozi bali wachache.Tanzania wajinga ndio hupewa madaraka na wenye akili timamu kuwa wafuasi.
Hakuna msomi asiyepingwa! Nyerere alikuwa mwanafalsafa,msomi,lakini wakosoaji mpaka kesho wapo wanaompinga
 
Very,ila hakuna ambaye atakosa kunyooshwa kidole,Masihi wenyewe walipingwa
Masihi hupingwa na wachache na huungwa mkono na wengi (sauti ya wengi ni sauti ya Mungu).
Ni muhimu kwa watu kufikiri kwa uoni mrefu na mpana.
Hata hivyo, ni lazima kuwa na tahadhari ya kundi la majuha wengi.
 
Back
Top Bottom