Pre GE2025 Hakuna mwana CCM yeyote zaidi ya Rais Samia atakayechukua fomu ya Urais wala kutia nia 2025 kwasababu ya utamaduni wetu

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Acha kufananisha Mlima na Vichuguu. CCM ndio Tanzania na Tanzania ndio CCM.huwezi kuitenganisha CCM na uhai wa Taifa letu.CCM ni kama ngozi ya Binadamu.huwezi ukamchuna ngozi mtu halafu abakie kuwa hai.CCM itaongoza Taifa letu kwa kadri ya uhai wake.
🚮
Watawala wote wa kiimla baada ya kujigeuza miungu watu hujisahau na kuota ndoto batili kama hizi ambazo kimsingi ni kufuru.

Hakuna chenye mwanzo kisicho na mwisho
 
🚮
Watawala wote wa kiimla baada ya kujigeuza miungu watu hujisahau na kuota ndoto batili kama hizi ambazo kimsingi ni kufuru.

Hakuna chenye mwanzo kisicho na mwisho
Japo ukweli huu ni mchungu lakini huo ndio ukweli kuwa CCM itaongoza Taifa letu kwa kadri ya uhai wake.
 
Hata mimi baona ..ila ndio utamaduni uliotudumaza sana. Anyway kwa upande wa mgombea na wapambe wake na wenye muono wake ni faida..ila kwa walio tofauti nae ni maumivu..nadhani wangeachaga ajitokeze mwana ccm mwingine ajitokeze kumchallange mara baada ya mhura wa kwanza..yani mda iwe miaka 5, mana kama hakuna mwana ccm mwingine anayeruhusiwa na hali ya vyama vingi ni mbaya na ilichagizwa na udhaifu wa katiba yetu..basi ni kama haina haja ya uchaguzi..Mh Rais aendelee mpaka wakati sahihi wa ki-mda ili wagombee wengine. Miaka 10 kwa mtu mmoja tu kuongoza nchi ni kama kusema wengine hakuna je kweli hawapo? Mimi naamini utaratibu walioweka ccm kwasasa sio mzuri..nchi ina wasomi na wenye uwezo wengi na wazalendo tofauti na zamani pale. Nitasikitika ikiwa 2025 mama yetu hapati challenge kwenye uwanja wa siasa ..najua kwa vyama pinzani bado hakuko vizuri kwa nafasi ya Urais, ila angalau ndani ya ccm wanaweza kuwepo bora zaidi ya Mama, wakafanya vema zaidi ya alipoishia mama yetu..sisemi kama hafai ila najua waliopo bench wanaweza kuwa mbadala mzuri zaidi.
 
Fany
Fanyeni mtakavyo ila Mungu Yehova muumbaji wa mbingu na nchi ameshaamua watu wake hawatateseka tena.
 
CCM na wana CCM tuna imani kubwa sana na Rais Samia na ndio maana tunasema Fomu ya Urais ni moja tu kwa ajili ya Rais Samia hapo Mwakani.
 
CCM na wana CCM tuna imani kubwa sana na Rais Samia na ndio maana tunasema Fomu ya Urais ni moja tu kwa ajili ya Rais Samia hapo Mwakani.
Najua..ila naamini kwenye ccm pia mpo ccm wawili... voting for and voting against...nawazungumzia hawa against....utaratibu unawanyima haki ya kuvote against..naamini kama wanaovote for her wakiwa wengi basi kwenye kushinda atashinda mama..ila wacha tuwaache na utaratibu wenu
 
Hakuna kitu kinachoitwa utamaduni,,,Chama kinaendeshwa na Katiba,,,ungeleta kifungu cha katiba kinachosema hivyo
 
Huna haja ya kuandika kwa mhemko kiasi hiki
Je katiba ya sisiemu inasemaje juu ya hili? Kama sivyo mnafanya kwa nidhamu ya woga'
Lakini kwa watu makini na wenye uelewa mzuri sidhani kama wanaweza kuwa na fikira kama hizi zako,fikira duni na za kimasikini na zisizo na mwanga daima.
Ushauri
Acha uoga na simamia haki
 
Hofu ya nini sasa😁
Huyu sijui leo mkuu kanywa mataputapu gani ,ccm inawenyewe , wakisema no basi ,by the way uchaguzi ukifanyika ccm itakua ile ya kusema machawa walikupenda sana ila Mungu kakupenda sana sana
 
Acha kufananisha Mlima na Vichuguu. CCM ndio Tanzania na Tanzania ndio CCM.huwezi kuitenganisha CCM na uhai wa Taifa letu.CCM ni kama ngozi ya Binadamu.huwezi ukamchuna ngozi mtu halafu abakie kuwa hai.CCM itaongoza Taifa letu kwa kadri ya uhai wake.

Ulianza mwaka gani kuijua CCM au unausikia kwenye corridor na kwenye kitenfo cha propaganda???
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…