Hakuna Mwanajeshi pekee yake anaweza kutoka hadharani na kutoa kauli Hii, akiwa Pekee yake

Hamatan

JF-Expert Member
Joined
Nov 10, 2020
Posts
7,840
Reaction score
18,115
Leo kila mmoja ameshuhudia kauli ya wazi toka kwa captain Tesha ikieleza hali mbaya ya nchi, na kulitaka jeshi lichukue uongozi ili kuinusuru nchi. Kwa wale waliopitia mafunzo ya kijeshi, kama mimi, tunajua kabisa, hakuna askari hata mmoja anayeweza kutoka hadharani na kutoa kauli kama hiyo akiwa pekee yake.

Binafsi, pamoja na kupitia JKT ile ya mwaka mmoja, na kisha kujiunga na JWTZ, na kisha kuachana na Jeshi, lakini kabla yake niliwahi kupata mafunzo kadhaa nje ya nchi ya masuala ya uongozi jeshini. Kwa uzoefu wangu huo, kwa vyovyote hii itakuwa ni sauti ya kundi la wanajeshi wasiokubaliana na mambo yanavyoenda, na bila shaka wamejiandaa kwa matokeo.

Na kauli hii hainishangazi, ninachoshamgaa ni ujasiri wa huyu ofisa wa jeshi kuyatamka haya hadharani. Inavyoelekea kuna chuki kubwa na kutokukubaliana na maduala ya udhulumaji haki yanayoendelea nchini, ndani ya jeshi. Kuna siku mmoja tukiwa kwenye shughuli za kijamii, afisa mwingine wa jeshi pua alitamka jeshi wanavyoudhiwa na hali inavyoendelea nchi hasa udhulumaji haki.

Na akasema wazi kuwa ukiwa askari halafu unaona watu wanatekwa, wanauawa, wanakamatwa hovyo, wanabambikiwa kesi za uwongo, unapata hasira ya ajabu, kwa sababu unaona kabisa una nafasi ya kuweza kuyazuia haya.

Kwa aiana ya watawala wetu wengi walivyokosa hekima, wataanza kuhangaika kumkamata huyu au hata kutaka kumteka, kama walivyozoe, na hapo watakuwa wamewasha moto.

Ikumbukwe Serikali hii imekwishakuwa adui wa:
1. Viongozi wa dini
2. Chama cha upinzani
3. Wasomi wenye fikra huru
4. Vijana wengi waliopuuzwa
5. Wananchi wengi walioachwa kwenye umaskini wa kuoindukia, huku mafisafi wakiiba bila kubughufhiwa

Sasa wakikosea wakajiingiza kwenye uadui na jeshi kwa ama kumkamata au kumteka huyu bwana, wajue wamewasha moto wa kuwaunguza wenyewe.

Kama kutakuwepo na mwenye hekima kwenye uongozi, kwa hapa tulipofikia, ni kusimamisha huo uchaguzi bandia, na kisha kuanzisha mazungumzo yanayolenga mwafaka wa kitaifa. Nje ya hapo yale ambayo yamekuwa yakitokea kungine, na sisi tukiwaona hao ni watu wa ajabu, yatatufika, tena huenda kwa nguvu kubwa kuliko huko kungineko.

Tuzidi kumwomba Mungu, amjalie hekima Rais, afuate njia ya kutuepusha na historia mbaya, aachane na ukiziwi, awatafute wenye hekima ajadiliane nao kupata mwongozo mzuri, aachane kabisa na machawa na wanamtandao.

Watawala watambue kuwa kwa hali ilivyo sasa, wanajeshi wakifanya lolote la kuonekana kutetea haki za wanaodhulumiwa, mamilioni ya watanzania watawaunga mkono wanajeshi, japo wanajua kuwa chini ya utawala wa kijeshi, mifumo ya kidemokrasia itasimama kwa muda.

Soma Pia: Mwanajeshi, Kapteni Tesha ajitoa muhanga kuongea hatari ya Taifa linapoelekea

Nimetimiza wajibu wangu wa kuonya. Watawala wana nafasi ya kuitafuta hekima, kama wana upendo hata mdogo sana kwa taifa hili.
 
Leo kila mmoja ameshuhudia kauli ya wazi toka kwa captain Tesha ikieleza hali mbaya ya nchi, na kulitaka jeshi lichukue uongozi ili kuinusuru nchi. Kwa wale waliopitia mafunzo ya kijeshi, kama mimi, tunajua kabisa, hakuna askari hata mmoja anayeweza kutoka hadharani na kutoa kauli kama hiyo akiwa pekee yake.

Binafsi, pamoja na kupitia JKT ile ya mwaka mmoja, na kisha kujiunga na JWTZ, na kisha kuachana na Jeshi, lakini kabla yake niliwahi kupata mafunzo kadhaa nje ya nchi ya masuala ya uongozi jeshini. Kwa uzoefu wangu huo, kwa vyovyote hii itakuwa ni sauti ya kundi la wanajeshi wasiokubaliana na mambo yanavyoenda, na bila shaka wamejiandaa kwa matokeo.

Na kauli hii hainishangazi, ninachoshamgaa ni ujasiri wa huyu ogisa wa jeshi kuyatamka haya hadharani. Inavyoelekea kuna chuki kubwa na kutokukubaliana na maduala ya udhulumaji haki yanayoendelea nchini, ndani ya jeshi. Kuna siku mmoja tukiwa kwenye shughuli za kijamii, afisa mwingine wa jeshi pua alitamka jeshi wanavyoudhiwa na hali inavyoendelea nchi hasa udhulumaji haki.

Na akasema wazi kuwa ukiwa askari halafu unaona watu wanatekwa, wanauawa, wanakamatwa hovyo, wanabambikiwa kesi za uwongo, unapata hasira ya ajabu, kwa sababu unaona kabisa una nafasi ya kuweza kuyazuia haya.

Kwa aiana ya watawala wetu wengi walivyokosa hekima, wataanza kuhangaika kumkamata huyu au hata kutaka kumteka, kama walivyozoe, na hapo watakuwa wamewasha moto.

Ikumbukwe Serikali hii imekwishakuwa adui wa:
1. Viongozi wa dini
2. Chama cha upinzani
3. Wasomi wenye fikra huru
4. Vijana wengi waliopuuzwa
5. Wananchi wengi walioachwa kwenye umaskini wa kuoindukia, huku mafisafi wakiiba bila kubughufhiwa

Sasa wakikosea wakajiingiza kwenye uadui na jeshi kwa ama kumkamata au kumteka huyu bwana, wajue wamewasha moto wa kuwaunguza wenyewe.

Kama kutakuwepo na mwenye hekima kwenye uongozi, kwa hapa tulipofikia, ni kusimamisha huo uchaguzi bandia, na kisha kuanzisha mazungumzo yanayolenga mwafaka wa kitaifa. Nje ya hapo yale ambayo yamekuwa yakitokea kungine, na sisi tukiwaona hao ni watu wa ajabu, yatatufika, tena huenda kwa nguvu kubwa kuliko huko kungineko.

Tuzidi kumwomba Mungu, amjalie hekima Rais, afuate njia ya kutuepusha na historia mbaya, aachane na ukiziwi, awatafute wenye hekima ajadiliane nao kupata mwongozo mzuri, aachane kabisa na machawa na wanamtandao.

Watawala watambue kuwa kwa hali ilivyo sasa, wanajeshi wakifanya lolote la kuonekana kutetea haki za wanaodhulumiwa, mamilioni ya watanzania watawaunga mkono wanajeshi, japo wanajua kuwa chini ya utawala wa kijeshi, mifumo ya kidemokrasia itasimama kwa muda.

Soma Pia: Mwanajeshi, Kapteni Tesha ajitoa muhanga kuongea hatari ya Taifa linapoelekea

Nimetimiza wajibu wangu wa kuonya. Watawala wana nafasi ya kuitafuta hekima, kama wana upendo hata mdogo sana kwa taifa hili.
Screenshot_20251004_171638_WhatsApp.jpg
 
Huyo atakuwa mwanajeshi fake au ana matatizo ya afya ya akili. Unataka kupindua nchi uende kwenye media!!! 🤣🤣🤣
Hakuna mwanajeshi fala. Hadi kafanya hivyo jua tu kila kitu kiko sawa
 
Waache wazibe masikio watakuja kupoteza uhuru wao, mali zao,na pengine baadhi yao uhai wao.
"There is a natural mystic blowing through the air.
If you listen carefully now you will hear.
This could be first trumpet, might as well be the last.
Many more will have to suffer, many more will have to die.
Don't ask me why" - Bob Marley
 
Back
Top Bottom