Hakuna mwanasiasa/Rais aliweza kupambana na Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) na akashinda!

Hahaaa brother kasome tena vizuri kwanza tuna natural harbour na built harbour! Na Kwa Mujibu wa Sheria yetu ya mwaka 2017, ni sehemu ya waters, na continental shelf, and land at large katika sehemu hizo ndio Bandari huwepo, ndio maana ukisoma Sheria hii, ukija ukiangalia mkataba na DP inataka hayo maeneo hasa inapotafsiri neno territory (inataja, anga, ardhi na Maji ya Tanzania)
Bandari ya dar ilijengwa,bila kujenga ni ufuo na si bandari,Kuna bandari gani ya serikali haikujengwa!?..Leo fezza Akitaka kujenga shule Dodoma hiyo sheria ya maliasili itamkumba!?
 
Mkataba hauna masilahi. Lakini hoja kuwa TEC inaweza kuichachafya serikali ?, hilo linawezekana tu kama TEC iko upande wa haki na serikali iko upande wa dhulma, Ila kama serikali iko upande wa haki, TEC haina nguvu hizo. Mfano Mzuri, Vatican nzima wakishirikiana na mkatoliki Nyerere walishindwa vita huko BIAFRA Nigeria, sioni ni kwa namna gani unaweza kudhani Taasisi ya Katoliki ni invincible!.

Kwenye hili la bandari TEC ipo upande wa haki,kwa hiyo ni bora serikali iwasikilize!
 
Nikukumbushe tu unapojadili isues jaribu kupanua WiGo wako wa ufahamu wa mambo yanavuoelezwa na kuoambanuliwa.

Hukuona malalamiko kwamba DP walitaka haki za ardhi contrary na Sheria zetu za ardhi na uwekezaji?

Unapizungumzia maji huepuki kuitaka bahari, ndio maana mkataba huu ilienda bungeni ili kuendana na matakwa ya sheria hii Hapa
 
Attachments

  • Screenshot_20230906-193959_1.jpg
    Screenshot_20230906-193959_1.jpg
    49.8 KB · Views: 2
Mkataba hauna masilahi. Lakini hoja kuwa TEC inaweza kuichachafya serikali ?, hilo linawezekana tu kama TEC iko upande wa haki na serikali iko upande wa dhulma, Ila kama serikali iko upande wa haki, TEC haina nguvu hizo. Mfano Mzuri, Vatican nzima wakishirikiana na mkatoliki Nyerere walishindwa vita huko BIAFRA Nigeria, sioni ni kwa namna gani unaweza kudhani Taasisi ya Katoliki ni invincible!.

Kwenye hili la bandari TEC ipo upande wa haki,kwa hiyo ni bora serikali iwasikilize!
Imeshasikiliza ndio mana wamewaita DP mezani mkuu kulikua hakuna namna,
Wamewasikia. Ndio mana wamesitisha mabadiliko ya Sheria ya uwekezaji na Ile ya Maliasili ya mwaka 2017
 
Wanafadhiliwa na katoloki nyuma ya pazia
Haiwezekani.
Yaani watu wanasema "Allahu Akbar", wanashambulia makanisa ya Wakatoliki na kuwaua , useme wanafadhiliwa na Wakatoliki?
Kama wangefadhiliwa na Wakatoliki, wasingeshambulia makanisa Katoliki, wangeshambulia makanisa mengine.

Fanya utafiti kwanza kabla hujaandika chochote.
 
Kwa wajuzi wa historia ya Tanzania wameishajua kuwa Tamko la Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) la kuhusu mkataba baina ya serikali ya Tanganyika AKA Tanzania na DP World ni kaa la moto mkali ambao unazidi kumchoma vikali muhusika mkuu na chama chake mpaka watakapokufa kisiasa mapema kama wataendelea kushupaza shingo.

Katika historia ya Tanzania hakuna mwanasiasa au Rais aliwahi kupambana na Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) halafu akashinda. Haijawahi kutokea na haitawahi kutokea katika miaka hii ya karibuni. Kufanya hivyo ni kujiangamiza kisiasa(political suicide).

Unaweza kuukataa huu ukweli lakini kuukataa kwako hakuwezi kuubadilisha kuwa uongo.

Mwl. Nyerere pamoja na nguvu zote za kikatiba alizokuwa nazo katika utawala wake lakini hakuwahi kutumia nguvu katika kupitisha ajenda zake za kisiasa pale ambapo maaskofu walikuwa na shaka au kumpinga. Alitumia nguvu ya ushawishi wa hoja kwa kujadiliana nao mpaka wakamwelewa na kukubali.

Nguvu za Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) zimeendelea hivyo katika tawala zote nchini. Hakuna mwanasiasa mwenye uelewa wa Tanzania na akili timamu aliweza kupuuza sauti ya Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC).

Muhusika mkuu wa mkataba wa DP World hakutegemea kama TEC wanaweza kutoa waraka mkali kama waliotoa kwa sababu sehemu ya 17 ya waraka imepigilia msumari wa mwisho wa jeneza la mkataba.

TEC IMEITAKA SERIKALI IACHANE NA MKATABA HUU.

Sehemu ya 17 ya waraka wa TEC inasema, “Hivyo tukiwajibika kimaadili, tunaona ni jukumu la serikali kusikiliza wananchi wanaotaka mkataba huu ufutwe. Kwa kuwa tumeonesha kuwa Tanzania tumeshawekeza na kuendeleza bandari, reli na bandari za nchi kavu; niwajibu miradi hii tuiendeshe Watanzania wenyewe huku tukikaribisha ubia tunaoudhibiti wenyewe. Hiki ndicho wananchi wanachokililia kusudi tujenge uwezo wetu wenyewe. Kwa vile tumegundua mapungufu yetu ya uendeshaji wa bandari, tunaweza kujizatiti kurekebisha mapungufu hayo wakati njia za kiuchumi zikibaki mikononi mwetu. Kwa sababu hizo na maelezo yote ya hapo juu, sisi Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania hatuungi mkono Mkataba huu”.

Baada ta waraka kutolewa, muhusika mkuu na genge lake akaanza kuhaha akitafuta jinsi ya kukabiliana nao. Amemtuma kiongozi mkuu wa nchi mstaafu ili ajibu hoja lakini hakufanikiwa kuzima moto, amejaribu kutumia mbinu za kidini kwa kuwatuma baadhi ya mashekhe ili wawajibu TEC katika misingi ya kidini lakini pamoja na juhudi zote, moto wa waraka wa TEC ndio unashika kasi ya kumchoma kisiasa. Ametuma “wajinga” fulani washambulie haiba ya maaskofu badala ya kujibu hoja hawajafanikiwa.

Alichofanya kwa sasa ni kuwatuma baadhi ya viongozi ndani ya serikali kwenda Dubai ili kuwaeleza wenye DP World kuhusu moto unavyowaka nchini ili waangalie namna ya kufanya ili kuondokana na moto mkali kisiasa ili kuepuka maafa ya kisiasa. Kwa hivi karibuni ndege ya Rais imekuwa na safari nyingi za kwenda Uarabuni na kurudi.

Katika hali hiyo ya kutapatapa ametangaza eti tenda ya kukaribisha wawekezaji kwenye bandari Terminal 2 ili ionekane hakutaka kugawa bandari zote kwa DP World wakati mkataba(IGA) unabainisha ni bandari zote na maziwa yote ya Tanganyika AKA Tanzania bara. Mjinga gani atakuja kuwekeza kwenye terminal 2 wakati kuna IGA inasema uwekezaji wowote katika bandari na maziwa nchini lazima kwanza uridhiwe na DP World.
Tumeona pia amemuondoa waziri wa katiba na sheria ili eti ionekane kama ndiye aliyesababisha hili sakata la DP World wakati kwenye IGA kuna saini ya Rais! Huku ni kutapatapa.

Kama isingekuwa waraka wa TEC, mchakato wa kuzifuta Sheria ya Mamlaka ya Nchi kuhusiana na Umiliki wa Rasilimali na Maliasili na Sheria ya Mapitio na Majadiliano kuhusu Masharti Hasi katika Mikataba inayohousu Rasilimali na Maliasili za Nchi za mwaka 2017 ungefanyika bungeni na hili tangazo lingine la tenda ya kukaribisha wawekezaji lisingetolewa! Hii yote ni imefanyika katika hali ya kutapatapa!

Nje ya mada, kile chama ulisema kitaanzishwa kabla ya uchaguzi mkuu wa 2025 ni lini kitaanza?
 
Nikukumbushe tu unapojadili isues jaribu kupanua WiGo wako wa ufahamu wa mambo yanavuoelezwa na kuoambanuliwa. Up

Hukuona malalamiko kwamba DP walitaka haki za ardhi contrary na Sheria zetu za ardhi na uwekezaji?

Unapizungumzia maji huepuki kuitaka bahari, ndio maana mkataba huu ilienda bungeni ili kuendana na matakwa ya sheria hii Hapa
Bandari siyo maliasili,we mbona unapenda kuzungukazunguka
 
Unazungukazunguka tu
We ndio unaona nazungukia au unahisi, watu wa Facebook kwaza sana hawataki, kufuatilia mambo hawataki, kutafuta taarifa na maarifa hawataki, kujadili mambo hawataki wanataka majibu short na hoja za kishabiki! Sidhani na sitaki kuamini kama wewe ni Moja wapo! Ila Kwa namna unavyowasilisha sentensi zako itoshe kusema wewe ni Moja
 
Bandari siyo maliasili,we mbona unapenda kuzungukazunguka
Ni Mali asili jipe Muda, kasome vyema sana sehemu anuwai. Sasa hivi ndio tumeongeza bandari kavu na artificial habours .... Na ukisoma sheria ya Maliasili inaiconfine bandari humo humo! Kiwango chako Cha elimu na uelewa wa mambo kinatia mashaka!
 
Niwekee sheria ya bandari
 
We ndio unaona nazungukia au unahisi, watu wa Facebook kwaza sana hawataki, kufuatilia mambo hawataki, kutafuta taarifa na maarifa hawataki, kujadili mambo hawataki wanataka majibu short na hoja za kishabiki! Sidhani na sitaki kuamini kama wewe ni Moja wapo! Ila Kwa namna unavyowasilisha sentensi zako itoshe kusema wewe ni Moja
Hahahaha,wewe unanizidi Mimi kutafuta na kufuatilia taarifa/mambo!?..unajaza insha ziso msingi,intellectuals tunaongea msitari mmoja sababu huwa tunajua wote tuliopo hapa tuna uelewa,siyo insha babu
 
Ni Mali asili jipe Muda, kasome vyema sana sehemu anuwai. Sasa hivi ndio tumeongeza bandari kavu na artificial habours .... Na ukisoma sheria ya Maliasili inaiconfine bandari humo humo! Kiwango chako Cha elimu na uelewa wa mambo kinatia mashaka!
Unajua tofauti ya port na harbour!?
 
Mkuu, nani alikuambia CCM ni mama au Baba yangu?

Kama CCM na viongozi wake wanakengeuka lazima nipambane nao ili kulinda maslahi ya taifa.

Kuna ahadi namba 8 ya mwana CCM ndani ya katiba ya CCM inasema; "Nitasema kweli daima, fitina kwangu mwiko"
wamissionari au TEC ni kweli wana nguvu pitia historia yao ndiyo chimbuko la ukoloni Afrika, kukomesha biashara ya utumwa,nchi nyingi kupata uhuru etc they are very influencial
 
Wewe ndiyo muongo. TEC Walimtandika Magufuli nyaraka mbili .
1. Utawala bora
2. Wakatoa msimamo wa kanisa kuhusu corona tukaacha kupeana mikono makanisani.

Juzi juzi ndo wameruhusu tena kupitia raisi wao wa TEC
Magufuli akukinzana na TEC wala taasisi yeyote ya dini,msimchafue.Magufuli alilazimisha watu kushikana mikono?
Uo utawala bora uliboreshwa mpaka tuone kweli TEC walisikilizwa?
 
Kwa wajuzi wa historia ya Tanzania wameishajua kuwa Tamko la Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) la kuhusu mkataba baina ya serikali ya Tanganyika AKA Tanzania na DP World ni kaa la moto mkali ambao unazidi kumchoma vikali muhusika mkuu na chama chake mpaka watakapokufa kisiasa mapema kama wataendelea kushupaza shingo.

Katika historia ya Tanzania hakuna mwanasiasa au Rais aliwahi kupambana na Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) halafu akashinda. Haijawahi kutokea na haitawahi kutokea katika miaka hii ya karibuni. Kufanya hivyo ni kujiangamiza kisiasa(political suicide).

Unaweza kuukataa huu ukweli lakini kuukataa kwako hakuwezi kuubadilisha kuwa uongo.

Mwl. Nyerere pamoja na nguvu zote za kikatiba alizokuwa nazo katika utawala wake lakini hakuwahi kutumia nguvu katika kupitisha ajenda zake za kisiasa pale ambapo maaskofu walikuwa na shaka au kumpinga. Alitumia nguvu ya ushawishi wa hoja kwa kujadiliana nao mpaka wakamwelewa na kukubali.

Nguvu za Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) zimeendelea hivyo katika tawala zote nchini. Hakuna mwanasiasa mwenye uelewa wa Tanzania na akili timamu aliweza kupuuza sauti ya Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC).

Muhusika mkuu wa mkataba wa DP World hakutegemea kama TEC wanaweza kutoa waraka mkali kama waliotoa kwa sababu sehemu ya 17 ya waraka imepigilia msumari wa mwisho wa jeneza la mkataba.

TEC IMEITAKA SERIKALI IACHANE NA MKATABA HUU.

Sehemu ya 17 ya waraka wa TEC inasema, “Hivyo tukiwajibika kimaadili, tunaona ni jukumu la serikali kusikiliza wananchi wanaotaka mkataba huu ufutwe. Kwa kuwa tumeonesha kuwa Tanzania tumeshawekeza na kuendeleza bandari, reli na bandari za nchi kavu; niwajibu miradi hii tuiendeshe Watanzania wenyewe huku tukikaribisha ubia tunaoudhibiti wenyewe. Hiki ndicho wananchi wanachokililia kusudi tujenge uwezo wetu wenyewe. Kwa vile tumegundua mapungufu yetu ya uendeshaji wa bandari, tunaweza kujizatiti kurekebisha mapungufu hayo wakati njia za kiuchumi zikibaki mikononi mwetu. Kwa sababu hizo na maelezo yote ya hapo juu, sisi Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania hatuungi mkono Mkataba huu”.

Baada ta waraka kutolewa, muhusika mkuu na genge lake akaanza kuhaha akitafuta jinsi ya kukabiliana nao. Amemtuma kiongozi mkuu wa nchi mstaafu ili ajibu hoja lakini hakufanikiwa kuzima moto, amejaribu kutumia mbinu za kidini kwa kuwatuma baadhi ya mashekhe ili wawajibu TEC katika misingi ya kidini lakini pamoja na juhudi zote, moto wa waraka wa TEC ndio unashika kasi ya kumchoma kisiasa. Ametuma “wajinga” fulani washambulie haiba ya maaskofu badala ya kujibu hoja hawajafanikiwa.

Alichofanya kwa sasa ni kuwatuma baadhi ya viongozi ndani ya serikali kwenda Dubai ili kuwaeleza wenye DP World kuhusu moto unavyowaka nchini ili waangalie namna ya kufanya ili kuondokana na moto mkali kisiasa ili kuepuka maafa ya kisiasa. Kwa hivi karibuni ndege ya Rais imekuwa na safari nyingi za kwenda Uarabuni na kurudi.

Katika hali hiyo ya kutapatapa ametangaza eti tenda ya kukaribisha wawekezaji kwenye bandari Terminal 2 ili ionekane hakutaka kugawa bandari zote kwa DP World wakati mkataba(IGA) unabainisha ni bandari zote na maziwa yote ya Tanganyika AKA Tanzania bara. Mjinga gani atakuja kuwekeza kwenye terminal 2 wakati kuna IGA inasema uwekezaji wowote katika bandari na maziwa nchini lazima kwanza uridhiwe na DP World.
Tumeona pia amemuondoa waziri wa katiba na sheria ili eti ionekane kama ndiye aliyesababisha hili sakata la DP World wakati kwenye IGA kuna saini ya Rais! Huku ni kutapatapa.

Kama isingekuwa waraka wa TEC, mchakato wa kuzifuta Sheria ya Mamlaka ya Nchi kuhusiana na Umiliki wa Rasilimali na Maliasili na Sheria ya Mapitio na Majadiliano kuhusu Masharti Hasi katika Mikataba inayohousu Rasilimali na Maliasili za Nchi za mwaka 2017 ungefanyika bungeni na hili tangazo lingine la tenda ya kukaribisha wawekezaji lisingetolewa! Hii yote ni imefanyika katika hali ya kutapatapa!
Samahani mtoe mada, nikumbushe jambo moja tu ambalo Nyerere alilitaka akshindwa kwa sababu kanisa lilimgomea...
 
Usahihi kamili wa hoja yako ni huu:

"Hakuna serikali yoyote ya kidunia (ikiwemo ya Tanzania) inaweza kupambana na kupingana na KANISA LA MUNGU na serikali hiyo ikaendelea kuwepo na kusimama..!"

TEC ni sehemu (kipande tu cha kanisa la Mungu). Lakini ukweli mkuu ni kuwa wapo watu wengi (jeshi la Mungu aliye hai hapa Tanzania) kote nchini (ukiacha TEC ambao wametoa official statement ya kukataa mpango huu wa Rais samia) ambao wanafunga na kuomba mchana na usiku kuhakikisha kuwa Mungu anaiponya nchi hii toka Kwa hayawani hawa..

Na mfano ulio dhahiri wa kuwa KANISA LA MUNGU liko kazini ni Mch. Mbarikiwa Mwakipesile na wafuasi wake huko Mbeya wanaomba usiku na mchana wakisema kwa uwazi bila kificho wala kumung'unya maneno kuwa Mungu aiangushe na kuipoteza CCM na serikali yake huku matangazo ya ibada zake yakirushwa live katika channel yake YouTube...

But all in all, huu ulioandika kwa ujumla wake ndiyo ukweli na wote wanaopingana na KANISA LA MUNGU wanajisumbua na kujipaka kinyesi tu...

Na ni kweli hii [emoji116][emoji116][emoji116] statement ya TEC ndiyo iliyomaliza na kuua kila kitu kabisa..!!

".....Hivyo tukiwajibika kimaadili, tunaona ni jukumu la serikali kusikiliza wananchi wanaotaka mkataba huu ufutwe. Kwa kuwa tumeonesha kuwa Tanzania tumeshawekeza na kuendeleza bandari, reli na bandari za nchi kavu; niwajibu miradi hii tuiendeshe Watanzania wenyewe huku tukikaribisha ubia tunaoudhibiti wenyewe. Hiki ndicho wananchi wanachokililia kusudi tujenge uwezo wetu wenyewe. Kwa vile tumegundua mapungufu yetu ya uendeshaji wa bandari, tunaweza kujizatiti kurekebisha mapungufu hayo wakati njia za kiuchumi zikibaki mikononi mwetu. Kwa sababu hizo na maelezo yote ya hapo juu, sisi Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania hatuungi mkono Mkataba huu”.

This is bold and most importantly authoritative statement. No any other authority will surpass this!!
Uharo mtupu huu...
 
Back
Top Bottom