Balozi Diria alikuwa waziri kamili wa mambo ya nje, hajawahi kuwa naibu waziri; balozi amina ali ni sahihi, alikuwa naibu waziri;
Kwa kuongezea tu, Dr Abdurahaman Babu ilikuwa ateuliwe uwaziri wa mambo ya nje lakini akapewa uwaziri wa fedha baada ya mapinduzi ya zanzibar. Dr. Babu ndiye mtu pekee aliyewahi kushika wadhifa wa waziri wa mambo ya nje wa zanzibar baada ya mapinduzin kabla ya wizara hiyo kufanywa kuwa ni ya muungano na kupewa mtu wa Tanganyika.
Tunatarajia zanzibar kujipatia waziri wake wa mambo ya nje wa pili baada ya miaka 50, kufuatia ujio wa Tanganyika.
Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
Kwa matarajio yako hayo, lakini kwa matarajio ya wazanzibari hailo haliko kwa sababu rasimu ya katiba haeleza kwa kina mgao wa madaraka pamoja na mgawawanyo wa office kuu za muungano, kama ilivyo sasa kwamba eti muungano uko balance, headquarter zote zipo tanganyika za muungano.
Kurudi kwa Tanganyika sio kupata kile wanacho kihitaji wazanzibari, bali ni kwa faida ya watanganyika wenyewe, kwa sasa wanategemea kuwa na serikali mbili za uwendeshaji na kuiburuza zanzibar.
Kama tumeamua kuwa na shirikisho basi kila upande ujitegemee, mambo saba ya muungano kila mtu abebe yake, mnahofia nini Tanganyika kuwa na mambo yenu ya nje na uraia wenu pamoja na ulinzi ?
Mmekuwa mukisema sana kuwa wazanzibari hawajui nini wanacho kitaka lakini kawathibishia Warioba siku ya uzinduzi kwamba asilimia 60 zanzibar wanataka mkataba, na asilimia 61 Tanganyika wanataka serikali tatu, akauuuza maoni ya wazanzibari na kuyachukua ya watanganyika na kuwapa 3.
Juzi alipohojiwa Warioba alisema kwamba katiba ya tanganyika inawezekana kuandikwa ndani ya miezi mitatu kwani maoni mengi ambayo waliopendekeza katika katiba ya muungano yamo mule ina mana ya wazanzibari hayamo.
Jengine zaidi munasema kwamba wazanzibari munawabeba kwa kutumia muungano, sasa jee kwanini munang'ang'ania kuwalazimisha katika huu mungano, si mutawache tupumue , mutapungunguza gharama kubwa za kuendesha muungano kama vile munavyo sema, kwa nini kunazidi kuilazimisha zanzibar kubaki katika muungano.
:sad::sad::sad::sad: