Hakuna nchi iliyotolewa kiuchumi na China, mfano ni Korea Kaskazini Vs Korea Kusini

Hakuna nchi iliyotolewa kiuchumi na China, mfano ni Korea Kaskazini Vs Korea Kusini

North korea mfumo wao ni ujamaa ambao watu wa ubepari hawawezi kutoa taarifa zao sahihi sababu hawana data kamili ila taifa maskini haliwezi miliki nuclear wala kutoboa kwa vikwazo walivyo wekewa.
Sisi acha tuwe machawa na goli la mama tyu.
Kumiliki nuclear is not hard kama uchumi wako wa nchi mwingi umeelekezea huko, hata tz mnaweza kama mkacha vipaombele vyote , na budget nzima ya nchi ikaelekea huko
 
Hajafungwa, kaachwa ashirikiane na wale anaoona wana mfaa,

Yan wew huwez ukawa unataka kunipiga halafu ufanye na mm kazi nikupe hela, USA kamuwekea vikwazo ili afanye biashara na China na Urusi ambao ni marafiki zake
Huu ni ujinga
 
Hapo kwenye vikwazo ni uongo kabisa, ina maana Marekani ndio lazima uelewane naye ndio uwe vizuri kiuchumi na kama ni hivyo basi kwa nini mtu akomae tu kuipinga Marekani wakati unafahamu vema kwamba kwa kufanya hivyo ndio unajimaliza mwenyewe.

To be rationale, why can't you join them if you can't beat them in order save your face.
Mifumo ya kiuchumi ya kidunia upo upande wao marekani na washirika wake sivyo unavyo fikiri wewe na ndio maana mpaka leo mataifa kinzani na marekani yanaanzisha mifumo ya ku challenge hii ya sasa
 
Kwa Korea Kaskazini kafungwa mikono na miguu??
Hujaelewa historia ya hiyo nchi, sisi tuliopata uhuru wa bendera huwa tunajisahau sana
Korea Kaskazini ilimwagiwa mabomu mengi na mmarekani kuliko hata Vietnam
Waliharibu miundombinu yote ya nchi, ni zezeta tu anaweza kufunika kombe mwanaharamu apite
 
sifa kubwa zaidi waliyo nayo ulimwenguni ni wizi
M
Screenshot_20230218-232333.png
Mhhh
 
Wakorea walipokubali kusitisha mapigano ya vita vya wenywe kwa wenyewe mwaka 1953 ilikuwa ni nchi moja ikagawanywa katika mataifa mawili, moja likaamua kuchukua mrengo wa ubepari na kushirikiana na US lingine likaenda njia ya Ukomunisti na kushirikiana na China.

Miaka 72 leo baada ya uamuzi huo Korea Kaskazini ni taifa fukara lenye GDP ya $bilioni 23 na GDP per capita ya $1,700, wanachojua ni kutengeneza mabomu tu, kwa upande mwingine Korea Kusini ni taifa la GDP ya $Trillion 1.8, taifa la nne kwa ukubwa wa uchumi Asia,ina wastani wa kipato $ 34,000, ni taifa linalogawa misaada kwa bara zima la Africa na lenye uwezo wa kuwaita viongozi wote wa Africa Seoul kuwapa agenda zake wajipange nazo.

Kwa uchache Korea Kusini ni nchi ya Samsung, Hyundai na LG wakati wenzao wa Kaskazini sifa kubwa zaidi waliyo nayo ulimwenguni ni wizi wa fedha wa udukuzi mtandaoni.
Kwa hiyo tunakubaliana Ubepari ni kichocheo cha maendeleo? Lakini ubebari wa Ulaya ni tofauti kidogo na wa Afrika.

Mabebari wa Ulaya wanamnyonya raia lakini kwa kupuliza, yaani huku wakiendelea kumuhudumia raia mahitaji ya msingi yenye ubora ili awe na afya njema ili waendelee kumnyonya vizuri mfano, elimu, huduma za maji, barabara.
LAKINI

Mabepari wa Kiafrika Kusini mwa Jangwa la Sahara waao wanamnyonya raia mpaka anashindwa kupumua na hawajali hata akifa sawa tu, wanachoangalia wao ni leo na siyo kesho. Hawajui uzima na furaha ya maskini ni faida kwao kuendelea kuwanyonya kuliko raia bila kushtukiwa. Raia wakiwa na maisha magumu, hawana furaha lazima wataanza kutafuta mchawi ni nani, mwisho wa siku watamgundua ndio pale tunaita machafuko!
 
Mwafrika hata Damascus na Allepo hii miji inawazid mbali sana , sio ajabu kuyasema hayo kwa NK , wenzio hawaangalii barabara 2 tatu tu bali wanaangalia vitu vingi kweny nchi
Ulitaka uwone nini ndio ujue Korea kaskazini pia ni matajili !!!!

Propaganda za western zisikumbumbaze mkuu. Korea kaskazini wapo juu sana ata mji mkuu wao ni nomaaa umejengeka kisasa!
 
Mwafrika hata Damascus na Allepo hii miji inawazid mbali sana , sio ajabu kuyasema hayo kwa NK , wenzio hawaangalii barabara 2 tatu tu bali wanaangalia vitu vingi kweny nchi
Ndio mana nikaulize mwanzo mkisema Korea ni masikini sana au China kawatupa jamaaa zake mnatumia vigezo vipi !!!!!

mana Korea kaskazini ipo Biz kuliko nchi nyingi za Afrika !!!

na ata muonekana tu wa macho jamaaa wapo mbaliii lkn ikiwa vigezo vyenu ni Propaganda za West basi sawa!!! Wakorea wanajenga nchi yao kwanguvu kubwa na hari ya Ajabu nyie mnasikiliza Media za Propaganda!!!!!!!!!
 
Ila vyombo vya habari viinaharibu sana akili za vijana wetu
Sana mkuu Propaganda zimewatatiza kuzielewa kwa undani wake.. !!!

lengo la iyo Habari usika usipowaza ivyo kujua nimeona Habari hiii lkn inalenga nn wenzetu wapo biz kutufifisha !!!

sio kutukweza apana !!!

inabidi tujikweze wenyewe,,
 
Ndio mana nikaulize mwanzo mkisema Korea ni masikini sana au China kawatupa jamaaa zake mnatumia vigezo vipi !!!!!

mana Korea kaskazini ipo Biz kuliko nchi nyingi za Afrika !!!

na ata muonekana tu wa macho jamaaa wapo mbaliii lkn ikiwa vigezo vyenu ni Propaganda za West basi sawa!!! Wakorea wanajenga nchi yao kwanguvu kubwa na hari ya Ajabu nyie mnasikiliza Media za Propaganda!!!!!!!!!
Korea Kaskazini ni nchi Masikini sana, muonekano wa maeneo machache Pyongyang yanayovutia ni kwa sababu waandishi wa habari hawaruhusiwi kupiga picha sehemu nyingine zilizochoka ambazo ni nyingi sana.

Ni sawa na hapa bongo mwandishi aje apelekwe Posta, masaki na Mbweni halafu aanze kuuliza kama Tanzania ni masikini sana. Korea Kaskazini wao wamezidi, watu masikini wachafu wachafu na wasio na kazi maalumu hawaruhusiwi kutembea katikati ya mji wa Pyongyang.
 
Back
Top Bottom