Hakuna nyongeza ya mishahara, hakuna ajira mpya, tozo kama kawaida na mikopo ipo pale pale. Je, kunakipi kinaendelea Tanzania?

Nani kasema hakuna ajira mpya?,nani kasema hakuna nyongeza ya mishahara? we ni mtanzania kweli?
Mara nyingi sipendi kujibishana na wapotoshaji kama wewe,viongozi wetu wenyewe wanatofautia kwenye kutoa takwimu za wanawo ajiliwa mara Rais anasema hatoajiri, hukija huku waziri mkuu anasema zimetoka ajira laki moja ( mfano) alafu waziri wa fedha anakwambia ajira zimetoka mia moja (Kwa mfano), alafu ukija mtaani Kuna wimbi kubwa walikosa ajira Baada ya kumaliza masomo. Je,unataka tumuamini nani?

Ukisema tujiajiri,je mitaala ya elimu ya nchi yetu imeweka elimu ya kujiajili? Je,vipi kuhusu mitaji,taasisi zenu zinazohusika na mikopo inamtambuaje kijana ambaye amemaliza shule na anahitaji mtaji wa kujiajili?

Msipende kuongea vitu ambavyo hamvitambui Kwa uwalisiwake upoje Kwa nje
 
Tuanze kuyachukulia hatua haya majizi ya kura na Mali za umma tumeyachekea miaka mingi tunavuna mabua
 
Si mlisema anaupiga mwingi imekuwaje tena?

Maana niliskia oh kaleta nyongeza ya mshahara...madaraja yameanza kupandishwa anafungua nchi😅😅😅 tumuache mama afanye kazi nyie Sukuma Gang kubalini mwendakuzimu harudi tena😅

Vipi ngapi ngapi huko Kojani FC?
 
Sijui anapotoshwa ama sisi huku nje hatuoni anayopitia
 
ajila gani unataka radio karibu zote nchini zinachezesha kamali makampuni ya kubeti pia yapo kila mtaa na kamali za wachina mtaani zimejaa bodaboda zinakopeshwa kila mtaa jiajili sio lazima uajiliw

Funguka,kwangu hicho unachokiita Amaleki ni ccm yenyewe.
Hilo tiba yake ni Katiba ya wananchi.
 
Funguka,kwangu hicho unachokiita Amaleki ni ccm yenyewe.
Hilo tiba yake ni Katiba ya wananchi.
Kiukweli #KATIBA MPYA haikwepeki..... ! Katiba ya sasa Haina majibu katika mfumo wa kidemokrasia Kwa wote.
 
Sasa awamu ya 6 unaiongeleaje wakati ndiyo kwanza inamiezi tu!Awamu ya 6 ni sawa mtoto aliyezaliwa hata kusimama bado.Ajabu awamu hii ya 6 imeweza kuwapandisha madaraja watumishi,wakulima waliokuwa wamekata tamaa kwa uduni wa soko sasa wanaanza kula matunda ya jasho lao tena kama awamu ya 4.Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni.Mama anapambana na mambo yanaonekana kwetu sisi washika jembe na watumishi.
 
Wengine wamejificha kwenye chuki za udini tu hawana sababu nyingine ya kumchukia mama.
 
Kwahiyo leo ndio akili zinawajia kwamba tatizo siyo mama?

Mbona mlisema magufuli ndio chanzo cha matatizo yenu yote na kwamba baada ya kufa ndio matatizo yenu yameisha?
 
Inshu katiba mpya yenye kutatua changamoto zote hizi. Unaposema watu wamepandishwa madaraja alafu figure inasoma vilevile,Mimi sioni mantiki yeyote ya kufanya hivyo
 
Noma... Ngoja tusubiri.
 
Hiz tasilimali wameshagawana wenyw bwashee
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…