Hakuna nyongeza ya mishahara, hakuna ajira mpya, tozo kama kawaida na mikopo ipo pale pale. Je, kunakipi kinaendelea Tanzania?

Hakuna nyongeza ya mishahara, hakuna ajira mpya, tozo kama kawaida na mikopo ipo pale pale. Je, kunakipi kinaendelea Tanzania?

Nani kasema hakuna ajira mpya?,nani kasema hakuna nyongeza ya mishahara? we ni mtanzania kweli?
Mara nyingi sipendi kujibishana na wapotoshaji kama wewe,viongozi wetu wenyewe wanatofautia kwenye kutoa takwimu za wanawo ajiliwa mara Rais anasema hatoajiri, hukija huku waziri mkuu anasema zimetoka ajira laki moja ( mfano) alafu waziri wa fedha anakwambia ajira zimetoka mia moja (Kwa mfano), alafu ukija mtaani Kuna wimbi kubwa walikosa ajira Baada ya kumaliza masomo. Je,unataka tumuamini nani?

Ukisema tujiajiri,je mitaala ya elimu ya nchi yetu imeweka elimu ya kujiajili? Je,vipi kuhusu mitaji,taasisi zenu zinazohusika na mikopo inamtambuaje kijana ambaye amemaliza shule na anahitaji mtaji wa kujiajili?

Msipende kuongea vitu ambavyo hamvitambui Kwa uwalisiwake upoje Kwa nje
 
Adui wetu sio Mama, NI katiba ya 1977 na CCM.
Rais AMBAYE pia NI mwenyekiti was CCM amekuwa na madaraka makubwa mno.

Nchi Ina rasiliimali za kila aina, ikiwemo madini ya thamani kubwa, LAKINI serikali inategemea kwa kiasi kikubwa pato lake kutoka kwenye bia. Nchi inaendeshwa na pombe
Tuanze kuyachukulia hatua haya majizi ya kura na Mali za umma tumeyachekea miaka mingi tunavuna mabua
 
Wanajukwaa nawasalimia Kwa jina la Jamhuri.

Wanandugu kunajambo naomba niwashirikishe tujadiliane.

Kama hakuna nyongeza ya mishahara,hakuna ajira mpya,tozo kama kawaida na mikopo ipo pale pale. Je,kunakipi kinaendelea Tanganyika? Au Kuna mchezo tunachezewa sisi watanganyika Kwa manufaa ya Wanzanzibari?
Si mlisema anaupiga mwingi imekuwaje tena?

Maana niliskia oh kaleta nyongeza ya mshahara...madaraja yameanza kupandishwa anafungua nchi😅😅😅 tumuache mama afanye kazi nyie Sukuma Gang kubalini mwendakuzimu harudi tena😅

Vipi ngapi ngapi huko Kojani FC?
 
Si mlisema anaupiga mwingi imekuwaje tena?

Maana niliskia oh kaleta nyongeza ya mshahara...madaraja yameanza kupandishwa anafungua nchi😅😅😅 tumuache mama afanye kazi nyie Sukuma Gang kubalini mwendakuzimu harudi tena😅

Vipi ngapi ngapi huko Hangaya FC?
Sijui anapotoshwa ama sisi huku nje hatuoni anayopitia
 
ajila gani unataka radio karibu zote nchini zinachezesha kamali makampuni ya kubeti pia yapo kila mtaa na kamali za wachina mtaani zimejaa bodaboda zinakopeshwa kila mtaa jiajili sio lazima uajiliw

Katiba ya mwaka 77 ni muendeleze wa Yale makubaliano ya wazee.
Hirizi ya ccm ipo kwenye katiba ccm haitaki katiba mpya, means itakufa.
Mwenge ndo ubani wenyewe ukicheza na mwenge unaondoka aliyeusitisha sababu ya corona yakamkuta.
So ni lazima viongozi wa dini waungane kumuondoa amaleki ,Ili tuwe na akili ya maendeleo.
Amaleki anakula akili za watz jiulize why wenyeji wa lindi, bagamoyo uwezo wao wa kufikiri upo chini Kazi ya amaleki hiyo.
Funguka,kwangu hicho unachokiita Amaleki ni ccm yenyewe.
Hilo tiba yake ni Katiba ya wananchi.
 
Funguka,kwangu hicho unachokiita Amaleki ni ccm yenyewe.
Hilo tiba yake ni Katiba ya wananchi.
Kiukweli #KATIBA MPYA haikwepeki..... ! Katiba ya sasa Haina majibu katika mfumo wa kidemokrasia Kwa wote.
 
Lete takwimu zako sahihi Kisha tutofautishe na Awamu tangulizi kama upo sahihi na hicho unacho kiunga mkono.

Tukiangalia Awamu tangulizi Kabla ya Awamu ya 5 na 6 zote zilikuwa zinaongeza mishahara Kwa watumishi wote pia Madara wanapandishwa Kwa wakati na hakukuwa na umati wa wahitimu wa vyuo uraiani kama ilivyo Awamu ya 5 na 6
Sasa awamu ya 6 unaiongeleaje wakati ndiyo kwanza inamiezi tu!Awamu ya 6 ni sawa mtoto aliyezaliwa hata kusimama bado.Ajabu awamu hii ya 6 imeweza kuwapandisha madaraja watumishi,wakulima waliokuwa wamekata tamaa kwa uduni wa soko sasa wanaanza kula matunda ya jasho lao tena kama awamu ya 4.Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni.Mama anapambana na mambo yanaonekana kwetu sisi washika jembe na watumishi.
 
Ajira gani tena mkuu siku chache zilizopita walimu wa kutosha wameajiriwa, idara ya afya wamelamba ajira, askari magereza, uhamiaji, zimamoto na police wamelamba ajira na wengineo wengi,pia watumishi wamelipwa madai yao na kupandishwa madaraja ikiwemo kubadilishiwa mishahara yao wewe upo dunia gani mkuu. kuhusu kuongezeka kwa mishahara watumishi wamehaidiwa may mosi inayokuja mkuu wa nchi atakuja na viwango vipwa sasa muda haujafika lawama za nini.
Wengine wamejificha kwenye chuki za udini tu hawana sababu nyingine ya kumchukia mama.
 
Adui wetu sio Mama, NI katiba ya 1977 na CCM.
Rais AMBAYE pia NI mwenyekiti was CCM amekuwa na madaraka makubwa mno.

Nchi Ina rasiliimali za kila aina, ikiwemo madini ya thamani kubwa, LAKINI serikali inategemea kwa kiasi kikubwa pato lake kutoka kwenye bia. Nchi inaendeshwa na pombe
Kwahiyo leo ndio akili zinawajia kwamba tatizo siyo mama?

Mbona mlisema magufuli ndio chanzo cha matatizo yenu yote na kwamba baada ya kufa ndio matatizo yenu yameisha?
 
Sasa awamu ya 6 unaiongeleaje wakati ndiyo kwanza inamiezi tu!Awamu ya 6 ni sawa mtoto aliyezaliwa hata kusimama bado.Ajabu awamu hii ya 6 imeweza kuwapandisha madaraja watumishi,wakulima waliokuwa wamekata tamaa kwa uduni wa soko sasa wanaanza kula matunda ya jasho lao tena kama awamu ya 4.Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni.Mama anapambana na mambo yanaonekana kwetu sisi washika jembe na watumishi.
Inshu katiba mpya yenye kutatua changamoto zote hizi. Unaposema watu wamepandishwa madaraja alafu figure inasoma vilevile,Mimi sioni mantiki yeyote ya kufanya hivyo
 
Wanajukwaa nawasalimia Kwa jina la Jamhuri.

Wanandugu kunajambo naomba niwashirikishe tujadiliane.

Kama hakuna nyongeza ya mishahara,hakuna ajira mpya, tozo kama kawaida na mikopo ipo pale pale. Je, kuna kipi kinaendelea Tanganyika? Au Kuna mchezo tunachezewa sisi watanganyika Kwa manufaa ya Wanzanzibari?
Noma... Ngoja tusubiri.
 
Hiz tasilimali wameshagawana wenyw bwashee
Si bure kunakitu tunafichwa kwenye Pato la Taifa,haiwezekani tuwe na rasilimali zote alafu tuwe tunaendesha nchi Kwa kutegemea bia,sigara na mikopo mikubwa plus tozo za miamala alafu mambo yapo vile vile hakuna maboresho ya mishahara wala ajira mpya...!

Kunauwezekano mkubwa watu wachache katika uongozi wananufaika na hii hali uwenda Kuna out source za nchi hii zinapitiliza kwenye mifuko Yao binafsi.

Nguvu kubwa inayotumika kuzuia katiba mpya ndiyo kitu ambacho kinatupa ukakasi wa kuhisi Kuna mambo mabaya yanafanyika kupitia katiba ya zamani.

Kwa hali ya sasa katiba mpya inahitajika Kwa Tanzania hakuna mjadara juu wa hili.
 
Back
Top Bottom