Tundu ni mtu wa pekee sana, ana utofauti na hao wengine wagombea, sikuwahi sikia hata mkuu wa nchi kuzunguka kutafuta saini mbali na pale alipopokea lile gimbi. Hivi hakujua mtaani au kijijini mtu mpaka ufuge gimbi lifikie pale linakuwa limebeba maroho yote, hili mtani utalijua kiroho.
Gimbi linaona watu wakizaliwa, wakiroga, wakitambika, wakifa, limeshughudia misiba limesikia watu wakisema na linaongea na ardhi, leo hii mkuu top leader unalishika kwenye kadamnasi, haikuwa nzuri.
Mwalimu Nyerere alipokuwa anapewa zawadi walikuwa wanampokelea. Na akitoka hapo anaenda kwa kiongozi wa mila kusema naye.
Anyways hayatuhusu,
Ya Lissu leo ni makubwa, ni nini kimewalazimisha kushezesha orodha? Suala la kiroho sana hilo.
Je hao wagombea wengine waliopitishwa tu yaani bora liende si ni lazima watakuwa bora liende, tutaona.
Ni nini kilikusudiwa kimtokee, mpaka ikafika tunaona namba za magari kuwa yanamngoja nje tukasikia mengi mengi vile.
Mwisho nguvu zao zikamezwa, Ikawa kimyaaa.
Sitaki kumalizia kuandika kitu ambacho kilishaandikwa, ardhi ni shahidi. We will see.
Mshana Jr hulali ?