Hakuna Rais wa Tanzania aliyewahi kumteua Joseph Sinde Warioba kuwa Jaji wa Mahakama yoyote hapa nchini, awe mkweli asipotoshe

Pia aliwahi kuwa jaji katika Mahakama ya Haki ya Afrika Mashariki, na mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba ya Tanzania tangu mwaka 2012.

Alihitimu kutoka Chuo Kikuu cha Afrika Mashariki jijini Dar es Salaam, Tanzania mnamo 1966. Kuanzia 1966 hadi 1968, aliwahi kuwa wakili wa serikali jijini Dar es salaam, na kutoka 1968 hadi 1970, kama wakili wa Halmashauri ya Jiji. Mnamo mwaka wa 1970, alihitimu kutoka Chuo cha Hague cha Sheria ya Kimataifa. Kuanzia 1976 hadi 1983, aliwahi kuwa Wakili Mkuu wa Tanzania. Kuanzia 1983 hadi kuchaguliwa kwake kama waziri mkuu, alihudumu kama waziri wa haki.

Kufuatia umiliki wake kama waziri mkuu, aliwahi kuwa jaji wa Hamburg, Korti ya kimataifa ya makao yake makuu ya Ujerumani ya Sheria ya Bahari kutoka 1996 hadi 1999. Zaidi ya hayo, mnamo 1996, Rais Benjamin Mkapa alimteua kama mwenyekiti wa Tume ya Rais Dhidi ya Serikali Rushwa, inajulikana zaidi kama Tume ya Warioba.

Warioba alichaguliwa kuongoza Kundi la Waangalizi wa Jumuiya ya Madola katika uchaguzi wa Aprili 2007 wa Nigeria. Alitoa tathmini chanya ya uchaguzi huo, akiona ni ya maendeleo huku akisema pia kwamba kuna makosa.

Warioba aliteuliwa mnamo Novemba 2016 na Rais wa Tanzania John Magufuli kama Kansela wa Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine cha Morogoro, Tanzania.
 
Kuwa UVCCM haimaanishi kwamba usiwe na akili.
"Warioba served as a judge on the Hamburg, Germany-based International Tribunal for the Law of the Sea from 1996 to 1999".
Unajaribu kuifuta hiyo record?? Bwege wewe
Bado hujasema, na hujajibu mada, kwenye hizo taasisi unaenda na hadhi yako, yeye hakwenda na ujaji
 
Bado hujajibu hoja, huko unaenda na hadhi yako
 
Ka chawa 😂😂
 
Zaidi zaidi aliwahi kukaa katika Baraza linaloshughulika na utatuzi wa migogoro ya bahari.
Mnamo 1985, alikua Waziri Mkuu na, wakati huo huo, Makamu wa Pili wa Rais hadi 1990. Baada ya muda wake kama waziri mkuu, aliteuliwa kuwa jaji katika Mahakama ya Kimataifa ya Sheria ya Bahari yenye makao yake makuu mjini Hamburg. (ITLOS) kwa muda wa miaka mitatu 1996-1999.

Hadi wewe Shule ngumu msongo mkali wa mawazo sababu ya ugumu wa maisha yako unaanza kuandika mashudu?
 
Soma hapa chini wasifu wa Judge Warioba....ujue alipataje ujaji.....hii ipo kwenye VPO website.

Itapendeza na utakuwa na manufaa kwa mabosi wako ikiwa utakuwa unajiongeza badala ya kukurupuka....siyo kwamba ukiwa chawa basi ndiyo uache kutumia akili walau kidogo, hao mnaowafanyia uchawa wataendelea kuwadharau sana ikiwa mtajitoa akili kwa kiwango hichi.


Elimu, Elimu, Elimu.......!
 
Jibuni maswali yake ya msingi kwanza, ndo tujue kama ni jaji ama sio.
Acheni uvivu vijana....information zipo kwenye finger tips zenu....just google, soma utajua!

 
Jibuni maswali yake ya msingi kwanza, ndo tujue kama ni jaji ama sio.
Jibu hilo hapo:

Mnamo 1985, alikua Waziri Mkuu na, wakati huo huo, Makamu wa Pili wa Rais hadi 1990. Baada ya muda wake kama waziri mkuu, aliteuliwa kuwa jaji katika Mahakama ya Kimataifa ya Sheria ya Bahari yenye makao yake makuu mjini Hamburg. (ITLOS).

Uliza swali lingine
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…