Hakuna sababu ya msingi ya Diaspora wa Kenya kuwa na haki tofauti na wa Tanzania!

Msikilize huyo punguwani asiyetaka diaspora kupata Dual citizenship
 

Attachments

  • VID-20230504-WA0001.mp4
    34.4 MB
  • VID-20230501-WA0031.mp4
    14.2 MB
Msikilize huyo punguwani asiyetaka diaspora kupata Dual citizenship
Usalama ni kizingizio tu! Usalama upi ambao diaspora watahatarisha?
Muungano una uhusiano gani na diaspora ? na haki ya uraia!
 


Mbona serikali ya Tanzania inawatambua diaspora zoezi la vitambulisho vya NIDA kwa wakazi ya U.K. kazi kwao.

Wasije Tanzania kuanza kulalamika wanasumbuliwa serikali imewafuata huko huko walipo.
 
Wacha porojo. Kama kuna faida kuwa raia wa Marekani, chukua. Mie napenda wanawake Wazungu blondes, ni hiari yangu nikipata nitaoa. Lakini sasa siwezi tena kudai mke Msukuma eti kwa sababu ni haki ya kuzaliwa. Au nigombee Udiwani kwetu Korogwe hulu nimeamua kuishi kuwa Raia wa London.
 

Tatizo ni ushamba uraia sio sawa na mke. Ukizaliwa Mtanzania wewe hasili yako haitabadilika milele hata ukioa wake mia moja bado utakuwa Mtanzania tu!. Utanzania sio kibali ni uhalisia wa mtu. Mimi ni mix mpare na mchaga niko hapa USA mtu yeyote ambaye anaweza kubadilisha hilo ni mungu pekee sio bunge wala wewe. Ni ujinga kufikiri una uwezo wa kuamua nani awe nani hayo ni maamuzi ya Mungu

Watu hawajali kugombea udiwani bali kwenda kuangalia makaburi ya mababu na mabibi zao bila visa za kijinga jinga. Kumzuia mtu kwenda kuangalia makaburi ya familia ni sawa na kutangaza vita haiwezekani. Hizi ndizo haki ambazo watu wanazungumzia. ujue tu hili sio swala lako au laungu bali la vizazi vijavyo. Je unajua watoto wako, wajukuu zako watatafuta maisha wapi? hata sisi baba zetu wametokea vijijini ndiyo wakaja mijini hawakujua kama watoto wao watakuja kwenda ulaya, nchi nyingine za Africa, Asia au US kutafuta maisha. Leo ni mimi kesho ni wewe. Ni utoto kuweka sheria bila kufikiria mbele
 
Diaspora wa Tanzania ambaye hajakana uraia wa Tanzania si bado mtanzania. Ana haki zote kama mtanzania. Acha upotoshaji.
 
Kama umekuwa raia wa Marekani unapokuja kuangalia makaburi unakuja kama Mmarekani. Kuna waingereza na wajerumani mababu zao walizikwa hapa. Wakija kuona makaburi wanakuja kama wageni. Huwezi kula keki na kubaki nayo.
 
Kama umekuwa raia wa Marekani unapokuja kuangalia makaburi unakuja kama Mmarekani. Kuna waingereza na wajerumani mababu zao walizikwa hapa. Wakija kuona makaburi wanakuja kama wageni. Huwezi kula keki na kubaki nayo.

Uraia ni vibali tu🥲 ! Haya ni makaratasi tu ya passport! Swali ni kwamba Utanzania ni nini hasa?

Ni diaspora wangapi wanatuma pesa Tanzania? Zaidi ya $1B je kwanini basi tusikataze wale ambao wamechukuwa uraia wa nje wasitume pesa? Kuna wazungu wangapi wanatuma pesa za familia zao Tanzania?

Inaelekea kwenye pesa tunataka wazawa watume pesa popote walipo lakini kwenye vibali ndiyo sio Watanzania!

Kama kweli ni uzalendo pendekezeni watu wote wasio Uraia wasiruhusiwe kutuma pesa Tanzania tuone kama bunge litapitisha.
 
Unajenga hoja za kitoto sana.
 
Diaspora wa Tanzania ambaye hajakana uraia wa Tanzania si bado mtanzania. Ana haki zote kama mtanzania. Acha upotoshaji.
Kwani diaspora wakiwa na uraia pacha nyie inawauma nini, mnapinga vitu hamuelewi kabisa, uraia nchi mbili ni fursa, ila roho mbaya zenu mnataka kuzuia fursa za wengine, kuna kesho mwanao anaweza kujikuta anaishi US na kaoa na kuwa raia, kwa uboya wako unaona sawa kumnyang'anya uraia wa alikozaliwa (TZ), kwa taarifa yako watanzania wanaoishi US na nchi zilizoendelea wanatuma pesa kuliko sekta yote ya utalii yote Tanzania, yale magorofa ya mbweni, Bunju, Mbezi etc zile ni pesa zimemwagika kutoka diaspora na ndio mnapatia vibarua na maduka yenu kuuza, mnakataa fursa wakati zinawafaidisha wenyewe, akili ya maharage tupu
 
Ulafi wa nini hapa duniani? Chagua uraia mmoja. Kama uraia pacha ni mzuri basi kuwa raia wa nchi 2,3,4....... Ni kuzuri zaidi.
 
Ulafi wa nini hapa duniani? Chagua uraia mmoja. Kama uraia pacha ni mzuri basi kuwa raia wa nchi 2,3,4....... Ni kuzuri zaidi.
Watu wanachukua uraia kwa sababu ya fursa tuu za kazi na maisha kwa ujumla lakini wengi bado moyo uko nyumbani, watu wanapiga kazi pesa nyingi wanatuma nyumbani kufanya maendeleo na kusaidia jamii zao then leo mnataka kumnyima huyo mtu haki ya kumiliki hata nyumba au ardhi, angalia faida kwa ujumla, nchi kama Mexico ina encourage raia wake hata kuruka ukuta ili wakapige kazi, acheni kulala nyie, kenya mwaka jana wametuma nyumbani zaidi ya trillion 10 nyumbani, pesa nyingi kuliko mauzo yao yote ya nje ambayo wengi wanafikiri ndio uchumi ulipo, wabongo hakuna records nzuri lakini nina uhakika mauzo ya utalii na dhahabu mnazofikiri ndio major exports za Tanzania zimezidiwa na pesa inayotumwa na diaspora
 
Ulafi wa nini hapa duniani? Chagua uraia mmoja. Kama uraia pacha ni mzuri basi kuwa raia wa nchi 2,3,4....... Ni kuzuri zaidi.
In 2022, Kenya's diaspora remittances rose by 8.34% to $4.027 billion. This was an all-time record and a tenfold increase in inflows to Kenya over the last 15 years. The remittances were close to the amount of foreign currency brought in by exports, which was $5.77 billion in the same period.
In February 2022, Kenyans living abroad sent home $321.5 million. Although the value of remittances decreased from the previous month, the amount of money sent increased substantially compared to February 2021.
According to the Central Bank, Kenya is now earning more foreign exchange from diaspora remittances than its major exports, such as coffee, tea, and horticulture.
 
Unajenga hoja za kitoto sana.

Tatizo hamja zoea watu wenye akili kubwa mnapenda bla bla akija mtu na kutoa facts mnatukana au kuwaita majina ! wengine wananielewa vizuri sana! kama hujaelewa ni utoto wako mwaka kesho unaweza kuelewa hoja yangu. search utaona topic zangu za zaidi ya miaka 10. Kuanzia vibali vya taifa, mikopo, mikataba ya madini, mawazo kwa wizara mbalimbali.... mimi ni Platinum Member
 
Sasa remmittances na uraia pacha vinahusiana nini? Hao wanatumia ndugu zao na kuwekeza kwao. Huhitaji urai pacha kufanya hayo. Chagua moja, ulafi wa kutaka uwe raia wa nchi zote hatuutaki.
 
kwa kifupi, tunataka uraia wa nchi mbili, ili diaspora wote warudi hapa bongo kama wabongo na sio wageni. nchi nyingi tu Africa zimeprove kwamba hakuna tatizo linatokea sasa sijui tanzania tunaogopa nini.
 
Hakuna diaspora aliyekatazwa kutuma pesa na kuwekeza nyumbani. Tena mimi ni muumini wa watu kutoka kwenda nje. Leo uchumi wa Lebanon unaokolewa na diaspora. Lakini huhitaji uraia pacha kufanya yote hayo.
 
Sasa remmittances na uraia pacha vinahusiana nini? Hao wanatumia ndugu zao na kuwekeza kwao. Huhitaji urai pacha kufanya hayo. Chagua moja, ulafi wa kutaka uwe raia wa nchi zote hatuutaki.
Pole sana, sampuli yako mnajifanya mnajua kumbe hamjui, akili yako inawakilisha wapuuzi walioiingiza nchi kwenye mikataba ya ovyo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…