Hakuna sababu ya msingi ya Diaspora wa Kenya kuwa na haki tofauti na wa Tanzania!

Hakuna sababu ya msingi ya Diaspora wa Kenya kuwa na haki tofauti na wa Tanzania!

Pole sana, sampuli yako mnajifanya mnajua kumbe hamjui, akili yako inawakilisha wapuuzi walioiingiza nchi kwenye mikataba ya ovyo
Nyie ndiyo mmeiingiza nchi kwenye mikataba ya hovyo na sasa mnataka kuiingiza kwenye mkataba wa uraia pacha sababu ya kutanguliza matumbo yenu mbele.
 
Wanaoongiza udiaspora ni Rwanda na South Africa. Rwanda waliuana 50% mwaka 1994 shauri ya ukabila, waliookoka wakaenda refugee nje wakaenda na hela zao. Afrika ya kusini apartheid wazungu walikuwa wanahaki zote kwa hiyo ilikuwa sawa kwa kia Mandela na Thano Benki kuomba uraia wa Tanzania. Baada ya Uhuru mambo yakageuka ikawa haki kwa Wazungu washindwa kuomba uraia wa USA. Kenya tangu Maumau na Mungiki na GEMA ni nchi ya kikabila, watu wanaenda nje kwa msaada w kabila lao na huku wanaacha kabila lao. Uhuru Kenyatta na Raila wana mali nyingi sana nje, of course waliziiba, kwa hiyo kutaka sheria iwe hivyo inaeleweka inabaki tu kujenga hoja Bungeni hasa ukiwa Rais na BBI. Sisi Tanzania hayajatupata hayo labda Karume alipotugomboa utumwa wale waliokuwa wanatumiliki watumwa wakaenda diaspora, nao inaeleweka kutaka uraipacha warejeshewe Watumwa wao Mji Mkongwe. Je tukubali? Labda kwa hila za maridhiano CUF na CHADEMA kwa sababu watoto waona wake zao na nasaba zao tayari walishakimbilia huko.
Karume yupi huyo aliyewakomboa? Watu historia yenu mnaficha mnakubali kusema uwongo sasa hilo kweli ni taifa? Okello ndiye aliyewakomboa kutoka utumwani bwana historia iwekwe wazi na ukweli ujulikane mnaficha nini?
 
Tukiacha ushabiki na kulishwa maneno kama majibu ya maswali yote mawili kwako ni "Ndiyo" basi unatakiwa kuunga mkono dual citizenship kwa wazawa wa Tanzania

1. Je unataka Watanzania wazawa ambao wako nje (Disapora) wapate haki sawa kwenye jumuia ya Africa mashariki kama wenzao wa Kenya na nchi nyingine? Kwa sheria za sasa diaspora wa kenya ana haki nyingi Tanzania kuliko diaspora ambaye ni mzawa wa Tanzania kwasababu diaspora wa Kenya anakuja kama Raia wa Kenya na huyu wa Tanzania anakuja kama mgeni/tourist.

2. Je unataka Watanzania Dispora huko walipo wawe ha haki sawa kama diaspora wa nchi nyingine?.

Hakuna Mtanzania namjua mimi amewahi kukana Uraia. Kukana Uraia ni utaratibu ambao una kuwa na barua ha hati ya kukana au kiapo cha kukana. Sifahamu mtu ambaye amekana Uraia wa Tanzania. Sheria ya Tanzania ndiyo inalazimisha neno Kukana na hii ndiyo kesi iliyopo mahakamani.

Uraia wa huko wanapoishi utawasaidia mambo ya msingi kama
(1) Kupata kazi nzuri
(2) Kupata bima za maisha
(3) Kuweza kusomesha watoto
(4) Kuhakikisha uwekezaji wao unalindwa kisheria.

Ngoja niwape mfano mdogo mimi binafsi mke wangu ambaye hakuwa na Uraia wa USA alikuwa na kuumwa sawa baada ya kumleta kutoka Tanzania. Tulipoenda Hospitali wakasema ni lazima afanyiwe operesheni haraka sana Vipimo tu vilikuwa $30,000 lakini operesheni ilikuwa $235,000. Mimi kwasababu ya bima yangu ambayo nisingeweza kuipata kama nisingekuwa Raia nililipia $3,000 tu na sio $265,000 ambazo ni gharama halisi. Hata Watanzania wenzangu wasingeweza kunisaidia.

Hizi ndiyo sababu kubwa za diaspora kuchukuwa Uraia wa nchi nyingine. Huwezi kukaa sehemu unafanya kazi usaidie familia nyumbani halafu tena kuna haki huna wakati wenzako wa kenya ambao mnashindana kwenye kazi hizo hizo wana haki zote. Hivyo badala ya kulishwa maneno tuwaulize kwanza diaspora ni kwanini wamechukuwa Uraia wa nchi wanazokaa na majibu kwa wanaojua sio ya kibinafsi bali ni ya kifamilia.

Hii ndiyo sababu umeona mabalozi wengi wa Tanzania wanaunga mkono kwasababu wanaelewa maisha halisi ya huku.
Basi diaspora wa tanzania achukue uraia wa kenya ili ale mazuri ya pote
 
Basi diaspora wa tanzania achukue uraia wa kenya ili ale mazuri ya pote
Mnakuwa wagumu wa kuelewa. Mzawa yeyote hatakiwi kuchukuliwa Uraia kwasababu sio huwezi kuhamisha historia makaburi ya mababu na mabibi zake yatakuwa Tanzania milele. Kumpa binadamu mwingine haki ya kuamua mtu akaone au asione makaburi ya ndugu zao ni kitu cha ajabu sana. Unasema Kenya wenzetu hawana utaratibu huu wa kijinga ambao hauna maono yeyote au sababu ya msingi. Mtu aliye zaliwa Kenya ni mkenya tu kwa sheria zao hata aende kuchukuwa Uraia wa nchi nyingine. Passport ni vibali tu sio mtu! kuna passport mpaka fake lakini haina maana ukimpa passport ya Tanzania mzungu wa uingereza ni Mtanzania kuliko mimi mzawa hata kama nipo USA. Mimi natuma pesa kwa ndugu zangu , harusi, shule, naenda kuangalia wagojwa, kuzika, kuangalia makaburi.... nk huyo wa Uingereza anaenda kwao Uingereza hata kama anafanya kazi Tanzania.

Nimetoa pendekezo basi hao diaspora wenye uraia wa nchi nyingine wasiruhusiwe kutuma pesa Tanzania kama kweli hatuwahitaji. Huwezi kusema tumeni pesa lakini hamuwezi kuingia! huu ni unafiki!. Tuamue moja kama hatutaki kuwapa haki za uhuru wa kuingia nchi yao kama wazawa bila masharti ya kibinadamu basi tusichukuwe pesa zao.

kuwe na sharia kama wenzetu ili ugombee au kupiga kura ni lazima uwe nchini kwa miezi sita kabla ya kura.
 
imagine, Israel kuna uraia pacha, lakini ulinzi na usalama upo palepale, marekani kuna uraia pacha, kenya kuna uraia pacha, rwanda kuna uraia pacha, ghana na Nigeria kuna uraia pacha, uingereza kuna uraia pacha, sasa hao wote tujiulize wameathirika na nini na huo uraia pacha ambacho Tanzania tukiuruhusu tutaathirika? kwamba tunaogopa tutakuwa na watu mamluki? kwani sasahivi hapa hakuna mamluki? au marekani au nchi yeyote inahitaji mamluki kukupeleleza kwenye ulimwengu huu ambao mtu anakaa uingereza alafu anadukua simu yako wewe wa manzese? mbona tuna mambo ya zamani sana? au tunaogopa watachukua nini? kwa taarifa yenu uraia pacha una faida nyingi kuliko hasara, kama zipo.
 
Ukweli ni kwamba vita ya uraia pacha kwa diaspora ni sentimental kuliko practical.

Wengi awajakubali uhalisia ya wazo la kufia na kuzikwa huko walipo, fate ya wengi wao.

From personal knowledge kuna familia ina ndugu wengi wako ulaya na miaka 30 wanaishi huko.

Kafa binamu yao wa kwanza huyu hakuwa na mtoto, badala ya kupeleka maiti Tanzania; wazazi wamepanda ndege kwenda kumzika huko ndugu zake wote wa tumbo moja wanaishi huko.

Kafa binamu yao wa pili familia nyingine huyu alikuwa na watoto wametaka mama yao azikwe huko, hata bila ya wao na yeye angezikwa huko huko pia. Bongo kaacha nyumba aliyojenga mumewe alirudi miaka mingi kajirisia kirahisi na huku akiwa keshaoa mke mwingine.

Wengi wa hiyo familia sioni kwenda kuzikwa Tanzania. Yupo mmoja mumewe alikuwa na biashara nzuri tu Tanzania (ni tajiri) amefika miaka 70 mwanae wa kwanza kakulia ulaya ana kazi nzuri baba yake anamwita kurithi biashara. Kamshauri auze hiyo biashara aende kununua nyumba huko halipo kilichobaki atamfundisha property development asiboreke akiwa ulaya. Ila yeye hana mpango wa kurudi kumuacha mkewe ulaya wala hana shida na mali za baba yake.

Nawajua watu wengine wa rika langu baadhi washaanza kupeleka wazazi wao care home baada ya kupata dementia.

Nawajua watu wamejenga Tanzania, watoto zao wote washakuwa wakubwa wanajitegemea, sasa hivi wanawajukuu. Wana uhuru wa kurudi Tanzania wakija holiday wamekaa sana miezi mitatu.

The point hizi diaspora muwe makini ni kweli mnashida ya uraia pacha in practice au sentiments tu; kwa sababu wengi watoto zenu na wajukuu zenu hiyo Tanzania awaijui kabisa na ukweli mchungu wengi wenye watoto na wajukuu waliozaliwa na kukulia ulaya as hiko kizazi kinavyojitambua ni raia wa huko na baba/mama/babu/bibi/mtoto/mjukuu akifa wengi wenu mtazikia huko.

Huo ndio ukweli kwa sasa kwa wale ambao wanatafuta 30 years plus ya kuishi huko, ila bongo ni sentiments tu.
 
Tukiacha ushabiki na kulishwa maneno kama majibu ya maswali yote mawili kwako ni "Ndiyo" basi unatakiwa kuunga mkono dual citizenship kwa wazawa wa Tanzania

1. Je unataka Watanzania wazawa ambao wako nje (Disapora) wapate haki sawa kwenye jumuia ya Africa mashariki kama wenzao wa Kenya na nchi nyingine? Kwa sheria za sasa diaspora wa kenya ana haki nyingi Tanzania kuliko diaspora ambaye ni mzawa wa Tanzania kwasababu diaspora wa Kenya anakuja kama Raia wa Kenya na huyu wa Tanzania anakuja kama mgeni/tourist.

2. Je unataka Watanzania Dispora huko walipo wawe ha haki sawa kama diaspora wa nchi nyingine?.

Hakuna Mtanzania namjua mimi amewahi kukana Uraia. Kukana Uraia ni utaratibu ambao una kuwa na barua ha hati ya kukana au kiapo cha kukana. Sifahamu mtu ambaye amekana Uraia wa Tanzania. Sheria ya Tanzania ndiyo inalazimisha neno Kukana na hii ndiyo kesi iliyopo mahakamani.

Uraia wa huko wanapoishi utawasaidia mambo ya msingi kama
(1) Kupata kazi nzuri
(2) Kupata bima za maisha
(3) Kuweza kusomesha watoto
(4) Kuhakikisha uwekezaji wao unalindwa kisheria.

Ngoja niwape mfano mdogo mimi binafsi mke wangu ambaye hakuwa na Uraia wa USA alikuwa na kuumwa sawa baada ya kumleta kutoka Tanzania. Tulipoenda Hospitali wakasema ni lazima afanyiwe operesheni haraka sana Vipimo tu vilikuwa $30,000 lakini operesheni ilikuwa $235,000. Mimi kwasababu ya bima yangu ambayo nisingeweza kuipata kama nisingekuwa Raia nililipia $3,000 tu na sio $265,000 ambazo ni gharama halisi. Hata Watanzania wenzangu wasingeweza kunisaidia.

Hizi ndiyo sababu kubwa za diaspora kuchukuwa Uraia wa nchi nyingine. Huwezi kukaa sehemu unafanya kazi usaidie familia nyumbani halafu tena kuna haki huna wakati wenzako wa kenya ambao mnashindana kwenye kazi hizo hizo wana haki zote. Hivyo badala ya kulishwa maneno tuwaulize kwanza diaspora ni kwanini wamechukuwa Uraia wa nchi wanazokaa na majibu kwa wanaojua sio ya kibinafsi bali ni ya kifamilia.

Hii ndiyo sababu umeona mabalozi wengi wa Tanzania wanaunga mkono kwasababu wanaelewa maisha halisi ya huku.
Nakuunga mkono, mimi na wife wangu kwanza tulihamia UK, kisha US, mimi nimeendelea kuwa Mtanzania, mwenzangu ni US subject, nilipopata ile ajali, nimetibiwa na support from her!.

Watanzania wengi wanaojilipua, wanajilipua kwasababu ya circumstances na sio kuukana Utanzania wao. Turuhusu dual citizenship!.

Tukiruhusu dual citizenship, diaspora wetu, watafanya mambo makubwa kama diaspora wa India, Nigeria, Ghana na Kenya.
Haya mambo ya diaspora tumeyaongea sana humu

P
 
Kama kuna mtu atakupa jibu sahihi kwenye maswali yako ya msingi unipigie simu +1 000-123-7654

Watanzania wengi sana wanaamini kuwa mtanzania anayefanya kazi nje ya nchi ama ana hela nyingi sana au ni mtu fulani ...................; kuna neno la kiswahili nimeshindwa kulipata lakini linafanana na Betrayer wa nchi.

Wanasahau kuwa mtu huyo ana ndugu zake na hata wazazi wake huko huko Tanzania ambao huenda wanamtegema yeye kwa kiasi kikubwa sana. Mtanzania huyo hataweza kupata haki huko Kenya kama Mtanzania tofauti na ambavyo Mkenya mwenye hadhi kama yeye huko ughaibuni waliko akiingia Tanzania atapewa hadhi kama Mkenya.
Mkenya akiingia Tanzania ni hiyo hiyo sawa na Mchina na Mhindi na Mzimbabwe au Mnyarwanda, haijalishi awe diaspora au la. Diaspora ni wasaliti walioenda nje wakaikana Tanzania ili wapewe uraia. Kwa Kenya ni wale waliokimbia mauaji ya MAUMAU na MUNGIKI na Ukabila na mapinuzibya Raila na Captain Ochola. Kwenda na kusoma au hata kuishi nje na kuchuma mali sawa, ukishatosheka rudi nyumbani. Nyerere na Pendo na Slaa na Baregu na Lipumba na Mwinyimvua na Fumbuka wote walikuwa nje wakasoma wakamaliza wakarudi. Kuna waliobaki bado wanakuja nyumbani kusalimia ndugu zao hawajaomba chochote wakanyimwa. Utajisikiaje mtoto wa Mbowe au mke wa Tundu raia wa Marekani awe Mbunge wa Rombo Kusini?
 
Nakuunga mkono, mimi na wife wangu kwanza tulihamia UK, kisha US, mimi nimeendelea kuwa Mtanzania, mwenzangu ni US subject, nilipopata ile ajali, nimetibiwa na support from her!.

Watanzania wengi wanaojilipua, wanajilipua kwasababu ya circumstances na sio kuukana Utanzania wao. Turuhusu dual citizenship!.

Tukiruhusu dual citizenship, diaspora wetu, watafanya mambo makubwa kama diaspora wa India, Nigeria, Ghana na Kenya.
P
Naona muda mwingine huwa unawekwa uchawa pembeni unazungumzia jambo kiuhalisia.
 
Uraia pacha ni sera ya mabeberu kunufaika na sisi moja kwa moja.

Ni agenda ambayo anaipambania sana Bongo Zozo na kafanikiwa kutuchota akili.
 
Naona muda mwingine huwa unawekwa uchawa pembeni unazungumzia jambo kiuhalisia.
Mkuu Nziiri sr , ni vile tuu hunijui, mimi sio chawa na sijawahi kuwa chawa!. Tatizo kwa vile mimi ni kada na kuna watu wanaichukia CCM hadi kukuona ukiwa CCM, wanakuona kama chawa!. Sio kila mwana CCM ni chawa!. Angalia hoja zangu za kugombea uongozi kupitia CCM kama ni hoja za kichawa chawa
View: https://youtu.be/Qr6j25jFGyI?feature=shared
P
 
Back
Top Bottom