Hakuna serikali yoyote duniani iliyofanikiwa kuwadharau Raia wake huku ikifanya itakavyo milele ikafanikiwa

Hakuna serikali yoyote duniani iliyofanikiwa kuwadharau Raia wake huku ikifanya itakavyo milele ikafanikiwa

Tambueni kwamba wananchi ndio wenye nchi, kwahiyo wanachokitaka ndio kinachopaswa kuwa kipaumbele, dharau, kiburi, jeuri havijawahi kuacha salama serikali yoyote ile.

Na wala hakuna serikali ilfanikiwa kwa kutegemea vyombo vya dola na watekaji, haijawahi kuwepo, kudharau baadhi ya wastaafu na kupuuza maoni yao ya msingi na kuchukua maoni ya kijinga ya wastaafu wachache wahafidhina ni kujichimbia kaburi.

Msije kusema hatukuwaambia .
Niwajibu wetu kuwakumbusha na kuwaelimisha
 
CCM nimeiunga mkono since , ila issue ya bandari na wanavyowadanganya halaiki wasio na elimu imeniudhi sana.
Mbona Kenya china walitaka bandari wakapewa ardhi wajijengee on a public private partnership basis ila hawakupewa bandari ya taifa .
Tz ndo nchi pekee kumpa mtu bandari fully furnished ni idea nzuri , tutakuwa lini indepedent kwa mwendo huu.
Umaskini na elimu duni ukiongeza uchawa unafanya walio madarakani kuonekana wanajua sana na hawakosei, pathetic state of affairs nchini
 
2025 siyo mbali. Mechi itakuwa DP World dhidi ya wananchi. DP World wamejipanga kumwaga pesa ya kuiteka nchi na kuifanya koloni lao milele.
Wananchi wanaotegemera kufanya maamuzi kwa busara nao bado wanaogelea kwenye ujinga na ushabiki usiokuwa na faida yoyote kwao.

It is not about the date or year...kama wananchi wengi wanadharaulika. Kama rushwa, dhuluma na wizi wa mali ya umma umetamalaki....ni suala la muda.
 
Jamani hii dawa inyopikwa ya bandari tayari imeanza kufanya kazi hata mgonjwa hajainywa. Bado iko chunguni inachemka matapeli wa bandarini matumbo ya kuharisha yamewashika na tegu wanatoka hovyo.
Bandari lazima ishughulikiwe sababu huku mtaani walala hoi wanapata bifhaa kwa ughali sababu matapeli yameisha kata chao huko bandarini kwa hiyo mfanya biashara hana budi ila kuongeza bei ya bidhaa. Anae umia ni mtanzania mtaani.

Mama kazia hapo hapo dawa inaingia.
 
Back
Top Bottom