Siyo peke yako uliyewahi kuishi huko, kama kweli uliwahi kukaa huko.
Uliyoandika hapa ni kama ni mwenyeji wa huko, au umeolea huko, na pengine kuwa na maslahi binafsi na huko.
Ndiyo, yapo waliyofanikiwa kuyafanya vizuri, mfano mzuri ni elimu yao iko imara zaidi, lakini hilo haliifanyi nchi hiyo iwe "...juu sana kwenye mambo mengi," kama unavyodai
"Raia kujitambua," una maana gani? Umefika kule Baringo ukakuta raia wapo tofauti sana na hawa waliopo Liwale katika kujitambua?
Unachukulia tu kakikundi uliko-'interact' nako hapo ulipofanya vikozi vyako ndiyo ukadhani kuna "seriousness, bidii na uwajibikaji, professionalism", ambayo huku Tanzania haipo mahali popote? Umefanya utafiti ukakupa majibu hayo?
Halafu unachekesha kweli: yaani hata "utembeaji" wa watu unauwekea uzito wai kuonyesha tofauti zilizopo kati ya watu walioko Nairobi na hawa , sijui wa Dar es Salaam au Tanzania yote?
Yaani unataka Tanzania twende Nairobi, tukajifunze kutembea kama wao? Hapo hali zetu ndipo zitakapoonekana kuwa nafuu kidogo kama wao?
Ninachohimiza waTanzania tujitahidi kukifanya kwa bidii zaidi kuliko kitu kingine kwa haraka zaidi, ni kuifanya elimu yetu iwe imara. Elimu yetu inaupungufu sana, na ndio maana, kama huyu 'Executive Sister' ni mTanzania kama inavyoonekana anadai yeye, anadiriki kuandika vitu vya ajabu sana kama alivyoandika hapa. Msingi wake wa elimu ulikuwa duni sana, licha ya kwamba hata hivyo vikozi alivyofanya huko Nairobi inaonyesha havikumsaidia kitu, kutokana kuwa na msingi mbovu tokea mwanzo.