Hakuna Taifa lililoendelea kwa kujipendekeza na kujidharau

Hakuna Taifa lililoendelea kwa kujipendekeza na kujidharau

Nikuhakikishie kuwa hamtaweza kumzuia mama kufanya kazi ngumu ya kulinyoosha taifa na kurudisha umoja ndani ya nchi mlio iharibu.

Kitendo cha kurudisha uhusiano wetu na majirani zetu kimewaumiza maana mnajua kuwa sasa mama anaanza kufagia maovu yaliyofanywa na mtangulizi wake.
Tulifikishwa pale tulipofika kutokana style ya uongozi uliopita. Awamu ya 4 ilifanya hayo yote anayofanya mama lakini tulipata nn? Hii nchi utadhani ina laana.

Sent from my SM-A730F using JamiiForums mobile app
 
Mtoa mada anahitaji kujifunza namna ya kutuma ujumbe kwa haraka kuliko kuandika makala ndefu ambayo mtu kama mimi ningetuma ujumbe huo huo kwa paragraph moja tu yenye sentesi zisozidi sita.

Ila alichosema ni ukweli kabisa; kuishi vizuri na jirani yako siyo lazima umlambe miguu yake, ni kuishi kwa kuheshimiana. Magufuli alikuwa expert sana wa kujua jinsi ya kuishi na majirani. Kenyatta alipofanya mambo mazuri kwa Tanzania na yeye alijibu kwa kufanya mambo mazuri kwa Kenya, na wakati Kenyata alipozuia ndege za Tanzania zisiingie Kenya, naye pia akazuia za Kenya zisiingie Tanzania, na wakati balozi wa Kenya alipofanya vizuri kwenye majukumu yake Magufuli alimsifia hadharani.

Siyo kwamba kuishi na jirani ni lazima ujiweke chini kwa kila kitu; hao wanaomshauri huyu mama, yaani timu Msoga itamuangusha huko mbeleni akianza kukumbana na stagnation pressure. Sera za Kikwete za "nikienda nje narudi na kibaba" kila matu anafurahi ni sera za kipuuzi sana zisizokuwa na vision kwa nchi.
 
Hakuna nchi inayoongoza kwa kujifanya iko chini kama Marekani. Sasa hivi ukiwasoma wamarekani mara zote wanaonesha kama nchi yako inaenda kupitwa na China au inazidiwa na China kwa baadhi ya mambo.
Revisit your source of information.
====
Unatilia mashaka uwezo wa wataalamu wako! Vijana wanabuni vifaa/mitambo ya/vya kusaidia jamii, wasimamizi wa mmasuala ya technologies wanawadhibiti kutoendeleza teknolojia hizo kwa sababu za kifitina na uchoyo!

Hivi kifaa chakugundua kuwa kuna mtu kaingia na simu bila mtu huyu kupitishwa kwenye scana zenye mionzi hatarishi sehemu fulani ambapo haparuhusiwi kuingia na simu kina ubaya gani?

Hivi kiantena kidogo kabisa cha kukuza mawimbi ya simu ambacho unaweza kutembea nacho popote ambapo kunashida ya mtandao kina shida gani?

Lakini tafiti zinazohusisha madodoso ndizo zina pewa kipaumbele! Unaenda kufanya udodosaji eti " unakubali ndege yupi tumtumie kuwinda nyoka na panya kati ya tai, mwewe,na bundi". Halafu eti tulete wataalamu wa nje watusaidie kupiga hatua.

Halafu mnasema tutafurukuta kate 4th revolution in the technological sphere!
===
Hivi serikali imetenga kiasi gani rasmi kwa ajili ya maendeleo ya kiteknolojia katika pato lake kitaifa!?
 
Tanzania ndo Taifa pekee hasa kwa miaka ya sasa ambapo kuanzia viongozi wake na wananchi ujidharau na kusifia mataifa mengine kwa kujipendekeza.

Wakati wa Baba wa Taifa haya mambo hayakuwepo. Hatukubembeleza mtu au Taifa. Hata Jomo Kenyatta enzi hizo alionja shubiri za Nyerere. Si mara ya kwanza Tanzania kuwa na vita ya maneno na ya kiuchumi na Kenya.

Rais Kamuzu Banda pia aliwahi onja joto ya jiwe. Nakumbuka mashuleni hadi tuliimba. "Banda wa malawi katuvalia ngozi simba, kututishia watanzania hatujali...hatujalii. Watanzania tulisimama wamoja. Banda kwa mkwara tu akafyata mkia. Lakini bado Tanzania tulibaki imara (Kwa sauti ya Msechu)

Viwanda viliendelea, tulisoma bure kuanzia chekechea au vidudu hadi chuo kikuu. Tulisafirishwa bure kwa wale wa boarding. Tulipewa daftari na kalamu shuleni. Kulikuwa pia na magari ya shule. Maduka ya serikali na mabasi ya serikali kila mkoa. Kulikuwa na viwanda mikoa mingi. Mabus ya wafanyakazi. Kulikuwa na bustani au park zilitunzwa vizuri. Watu tulienda kupumzika mandhari nzuri na familia. Miji ilipangiliwa. Barabara nyingi zilikuwa na miti pembeni. Leo hakuna kitu. Sijui vilienda wapi.

Pamoja na kiburi chetu hakuna kubembeleza. Tulifunga balozi hadi za uingereza na kukataa misaada yao. Ujerumani Mashariki nao tukawagomea. Israel na wengineo lkn bado Tanzania tulieshimika duniani.

Leo tumekuja na siasa za kubembeleza. Kujipendekeza, kusifia wengine. Leo Watanzania tunaona Wakenya kama ndo wakombozi wa uchumi wetu. Miungu wetu. Leo tunawapa rukhsa waingie mbungani kwetu. Wawe huru. Wawekeze kila sehemu. Ni vizuri. Lakini tunaijua vema Kenya? Nani alivunja umoja wa Afrika mashariki? Nani alidhurumu mali za umoja huo? Nani alitumiwa na majasusi kuvunja huo umoja?

Eti leo economic democracy yetu ni kujiona sisi wajinga ila mataifa mengine ni wajanja. Kazi yetu ni ziara za kusaini mikataba tunayopewa kusaini. Hata hatuna muda wakufikiria. Kisa hatutaki hudhi mtu.

Naomba ziara zingine watanzania tuwe tuna taarifiwa kabla ili tujue nini kinaenda fanyika na pia kama ni mikataba ijadiliwe kwanza bungeni na watanzania tuelewe.

Mtamsema sana vibaya Mwl. Nyerere lakini hatabaki kuwa mdiplomasia wa hali ya juu. Alikuwa mbabe lkn bado aliheshimika na mataifa makubwa.

Mtamsema vibaya na kumtukana Magufuli lkn nchi nyingi zilimtambua kuwa alisimama kwa masilahi mapana ya Tanzania. Hata Mkapa hakuwa na siasa za kubembeleza mataifa ya nje.

Angalia marekani, Uchina, Uingereza, Ujerumani na mataifa mengine wapi wanasera za kubembeleza na kusifia mataifa mengine. USA ilifikia sehemu kuweka vikwazo katika biashara na nchina japo USA inamtegemea China kwa biashara. Kikubwa ni kuangalia maslahi mapana ya nchi.

Eti leo tunasifia wakenya wanademokrasia zaidi ya Tanzania. Ni vizuri. Watanzania wanabaki kujidharau. Wanajiona wao si kitu. Kweli katika kukua tunaona mengi. Kujipendejeza sio kusifiwa ni kuzidi kudharaulika tu. Magufuli alikuwa mkorofi na mbabe. Lakini Tanzania iliheshimika. Hakuongea kiingereza lkn hotuba zake zilifatiliwa dunia nzima kusikia nini atasema. UN wenyewe walikubali kuwa alikuwa mtu aliependa Taifa lake na Afrika.

Korea kaskazini aijipendekezi lkn Marekani wanaogopa na kuheshimu Korea kaskazini. Duniani hapa mataifa makubwa yenye nguvu yote yalitumia ubabe.

Hata ukoloni ulifanyika kwa ubabe ili watawala wapate watakacho. Hata katika Biblia watawala hakuna alie kuwa lele mama. Hakuna alie jipendekeza na kusifia wengine.

Haya twendelee na kusifia, kubembeleza na kujipendekeza tuone hayo maendeleo. Hii awamu ya (-6<+4) imenikumbusha mbali hesabu za mlinganyo na magazijuto.

Hongera Rais wetu Samia Suluhu Hassan. Nakupenda ila kuwa makini na washauri wako. Hasa huyo ambae wakati wake nchi ilimshinda. Hata alipoulizwa kwanini Tanzania ni masikini wakati ina kila kitu. Alijibu hata yeye hajui na anashangaa kwanini Tanzania ni masikini. Ulikiri mwenyewe hotuba yako ya Bungeni kuwa anakushauri sana pamoja na yule bwana aliesema ataendeleza majengo alojenga babake lakini hakashindwa akabakiza majungu tu kule kwetu minazini.

Baba yake alikuwa na aakili kubwa. Ange kuwepo kule minazini kungekuwa dubai ndogo. Tusisingizie Muungano. Tunapotezwa tu. Yule baharia aliijenga nchi yetu ya minazini wakati huo huo wa muungano. Hata Dar wakati huo haikujengwa kama baharia alivyo ijenga minazini. Leo tunabaki lalamikia muungano badala ya kujikita kuijenga nchi yetu.

Yangu macho. Twendelee kujipendekeza. Kusifia na kuona sisi hatuwezi jenga uchumi wetu isipokuwa wawekezaji. China ilikuwa sawa na Tanzania miaka ya nyuma. Leo ni Taifa kubwa. Je, walitumia sera ya kujipendekeza na kusifia wengine na kujidharau?

Wachina walifanya kazi hawakutegemea wawekezaji uchwara kama Kenya. Walisomesha vijana wao nje, wakaiba tekinolojia toka mataifa makubwa. Wakaunda tekinolojia yeo. Rushwa ikapigwa vita ni kunyongwa tu. Taifa likasimama.

Watanzani leo hatuna scholarship kwa ajili ya Watanzania pekee kama yalivyo mataifa mengine. Mfano Afrika Kusini, Nigeria, Ethiopia na mengineyo hasa kwenda kusoma nje. Nashangaa balozi zetu hazina ubunifu.

Viongozi wengi tulionao leo walipelekwa kusoma nje na serikali. Leo wamekuwa wabinafsi.

Tanzania tu vijana wanaakili kwenye ubunifu na sayansi. Tuwatumie hawa. Tuwajari. Nchi imebaki majungu. Nchi imekuwa siasa kila kitu. Tunajenga shortcut ya maisha.

Viongozi tuwe na maono. Maendeleo hayaji kwa kujipendekeza. Watu watapata machungu ya maisha ila baadae wataenjoy. Nchi zote upitia huko. Ndo tutaona maendeleo ya kweli.

Karibu tena Ikulu kwa remote control. Nawe waziri wa mambo ya nje ulikuwa katibu Mkuu wa wizara ya mambo ya nje wakati wa team Msoga. Uliishia kutuletea Bush, Obama na hatukuona tija. Tulipata neti za mbu pekee.

Rais na baraza na taasisi waliishia kwenda nje. Nakuomba ubadilike. Mshauri vizuri mama. Najua anashaurika na akitulia ni kiongozi na Rais mzuri.
umeandika vema nadhani kuna cha kujifunza hapo, kazi iendeleee.
 
Ni kweli familia ya Kenyatta wanamiliki ardhi kubwa
Wakenya wameendelea nini ? Wana uchumi wa kati sawa nasi. Uchumi wao unatawaliwa na wachache. Ardhi inamilikiwa na wachache. Huku familia ya Kenyatta ikimiliki asilimia karibu 70 ya hyo nchi.
Nyerere hakuwa kuitetemekea. Na kunawakati alifunga mipaka. Eti Kenya wameendelea. Hujui Kenya.
, lakini sio 70%. Hata 5% haifiki. Gdp (per capita) Kenya wako juu- $4500+, nafasi ya21, wakati Tz ni $2700 nafasi ya 32 barani Africa. Ukiambiwa wameendelea kuliko sisi, ndio maana yake hatakama hutaki.
 
Baada ya kifo cha King JPM, EU walisema"Sasa Tanzania taa imezima ghafla"
TUTAMKUMBUKA.
Kujipendekeza, kujidharau, kujishusha hadhi ni hatari kubwa zaidi kuliko hatari yenyewe.
Ndiyo maana JPM alikuwa akituambia kuwa sisi si maskini, hivyo tunapaswa kujiamini na kutembea kifua mbele.
 
Siku zote lazima ujifunze kwa waliotangulia. Kenya walishatangulia. Lazima tuangalie njia walizopita.
OOooh, Kenya walishatangulia?

Tangulia kwenda wapi?

Wewe unaona Kenya wameendelea? Kwa akili za tope namna hii tutapata shida sana.
 
Kenya wako juu- $4500+
Wacha uongo. Ingekuwa tarakimu ndiyo hizo, asingekuwa kwenye Lower Middle Income, kama ilivyo Tanzania. Tofauti ya namba hizo kati ya Tanzania na Kenya sio kubwa kiasi hicho.

Pamoja na uongo huo, unashindwa kujua kwamba hata kama ingekuwa ni tarakimu hizo, mtu wa kawaida Kenya hana hela hiyo. Ni matajiri wachache, tena wengi wao watu wa nje ya nchi ndio wanaogawana sehemu kubwa ya utajiri huo. Lakini kwa kuwa kichwa chako kimejaa tope, basi unafikiri maskini pale Uasin Gishu naye ana pato hilo!
 
anacho jaribu kuwakilisha muandishi ni kwamba tusiwe tegemezi. tujikwamue kwa jituhada zetu
Sijapata kusikia taifa lolote lililoendelezwa na watu wengine wenyeji wao wekiwepowepo tu kama masanamu.

Sasa tunawalilia hata wakenya waje watuendeleze?

Kama hii sio laana, sijui tuiite kitu gani.

Mama ziara yake hii ya kwanza kajijengea sura mbaya kabisa. Natumaini yafuatayo atakayoyafanya yataziba kidogo aibu hii aliyoliletea taifa hili.
 
Mkuu Hongera kwa post ndefu nimesoma yote kwa umakini. Mimi binafsi nimeishi sana Kenya na kuna baadhi ya kozi nimesoma huko, Kenya wako juu sana kwenye mambo mengi, raia kujitambua,seriousness, bidii na uwajibikaji, professionalism, mfano wengi wanaofundisha lugha ya kiswahili nchi za Ulaya ni wa Kenya kwa sababu wao wanachukulia lugha ya kiswahili kama lugha ya biashara wakati sisi watu wamelala wanalalamika, ukienda Nairobi leo hii ukiangalia utembeaji wa watu tuu utangundua kwamba tunatakiwa tujifunze kutoka kwao,shule nyingi za binafsi Tanzania wakenya wamejaa na Tanzania hatutaki kujifunza chochote kutoka kwao kwa sababu ya kuamini kuwa kujifunza kutoka kwa mtu ni kujipendekeza. Tulichowazidi wakenya ni ukarimu na Ukubwa wa eneo la nchi vingine wametuzidi sana.
 
Mtahangaika sana mwaka huu, mwisho wa zamaumefika na mwisho wa chato pia
 
Mtamsema vibaya na kumtukana Magufuli lkn nchi nyingi zilimtambua kuwa alisimama kwa masilahi mapana ya Tanzania. Hata Mkapa hakuwa na siasa za kubembeleza mataifa ya nje.

Magufuli alikuwa mkorofi na mbabe. Lakini Tanzania iliheshimika. Hakuongea kiingereza lkn hotuba zake zilifatiliwa dunia nzima kusikia nini atasema. UN wenyewe walikubali kuwa alikuwa mtu aliependa Taifa lake na Afrika.
Nimezipenda hizo aya.
Apumzike kwa amani hayati Dr John Pombe Magufuli
 
Hivi nchi kuingia makubaliano ya kibiashara au uwekezaji na nchi nyingine ni kujidharau?!!!

Mtoa mada unaelewa kwa dhati kuhusiana na uwekezaji na biashara katika nyanja za kimataifa? Je, unajua rais anapokuwa ziarani na kusaini makubaliano fulani, kinachosainiwa ni roadmap tu au MoU kukaribisha / kuondoa vizingiti vya kibiashara na uwekezaji baina ya hayo mataifa?.

Na pindi muwekezaji anapokuja kuwekeza mkataba halisi wa biashara husika hujadiliwa na wataalamu wa wizara na kwa kuzingatia sera na sheria za nchi ndipo baadae husainiwa na waziri mhusika wa wizara na siyo Rais.

Kulingana na sheria za nchi yetu kuna mikataba ya kiwango fulani haiwezi kuingiwa na wizara hadi iwasilishwe na kupate kibali cha baraza la mawaziri.
 
OOooh, Kenya walishatangulia?

Tangulia kwenda wapi?

Wewe unaona Kenya wameendelea? Kwa akili za tope namna hii tutapata shida sana.

Watanzania tuwe makini sana, tukisha anza kujidharau/kukosa kujiamini TUMEKWISHA, maadui/washindani wetu wakisha nusa weakness yetu ya kutojiamini watatu chezea sana sana - walisha sema wana kitengo maalum cha ujasusi wa kiuchumi,watatuma watu wa kuchunguza baadhi ya Watanzania ambao ni: wabunge, wanasiasa Viongozi wenye ushawishi Serikalini pia na washauri wa karibu wa Madam President yaani wale wote wenye element ya usaliti watatafutwa na kuingizwa kwenye kundi la kufanya lobbing ya hali ya juu ya kumpotosha mama wa watu - sijasema kwamba mama Samia hawezi kufanya mahamuzi on her own, far from it.

Kwa bahati nzuri madam President aliwahi kutamuka mwenyewe kwamba atatilia maanani baadhi ya maoni ya walala hoi na kuyafanyia kazi, basi tunamshauri kwa nia njema kwamba "tusiende mbio, mbio kukimbilia mlio, kumbe tunako kimbilia kuna kilio, tutapatwa na ajali/hatari DUNIA itatushangaa!!" tuwe wakweli hapa - hakuna Mtanzania mwenye uchungu wa kweli wa Taifa hili inataka kurudi tena kwenye zama za uongozi wa awamu ya nne - hakuna.

Magufuli wa watu pamoja na mapungufu yake ya hapa na pale kama binadamu wote tulivyo lakini alikuwa anasema/anasisitiza kila siku kwamba jamani eeh WATANZANIA tutembee kifua MBELE i.e tujiamini,maadui zake walimchukia lakini wali admire ujasiri wake wa kujali maslahi ya Taifa letu ya kulazimisha wawekezaji wote uwekeze kwenye enviroment ya win win situation ambayo haina element ya unyonyaji,wizi na ufisadi.

Kama ni suala la kujifunza mambo kwa nini tusiende kujifunza kwenye Mataifa yaliyo piga astronomical maendeleo in a record time tangu wapate uhuru - mfano mzuri ni: China, Malaysia, Korea Kusini na India - kuna nini cha kujifunza kwenye mataifa ambayo GDP yao haizidi sana ya Tanzania na wao bado wapo kwenye bracket ya mataifa yenye uchumi wa kati kama sisi - wangesema walao South Africa na Misri watu wange elewa kwamba hao at least uchumi wao umepaa, we can learn something worthwhile therefrom.
 
Ni kweli familia ya Kenyatta wanamiliki ardhi kubwa

, lakini sio 70%. Hata 5% haifiki. Gdp (per capita) Kenya wako juu- $4500+, nafasi ya21, wakati Tz ni $2700 nafasi ya 32 barani Africa. Ukiambiwa wameendelea kuliko sisi, ndio maana yake hatakama hutaki.
So hiyo kwako ndo kuendelea, Marekani inakipato cha juu kuliko Scandinavia. Lakini Marekani kuna maskini wa kutupwa. Unapoongelea uchumi ni kitu kipana. Na Scandinavian countries zinaongoza kwa huduma za kijamii na uwezi kuta umasikini kama uliopo Marekani japo Marekani inakipato kikubwa.
Jiulize ni kwann wamerekani wengi wanahamia Canada na scandinavia countries japo uchumi ni mkubwa. Vivyo vivyo life style ya maisha kwa Africa mashariki baina ya Kenya na Tanzania.
Rudi kafanye utafiti wako.
 
Mkuu Hongera kwa post ndefu nimesoma yote kwa umakini. Mimi binafsi nimeishi sana Kenya na kuna baadhi ya kozi nimesoma huko, Kenya wako juu sana kwenye mambo mengi, raia kujitambua,seriousness, bidii na uwajibikaji, professionalism, mfano wengi wanaofundisha lugha ya kiswahili nchi za Ulaya ni wa Kenya kwa sababu wao wanachukulia lugha ya kiswahili kama lugha ya biashara wakati sisi watu wamelala wanalalamika, ukienda Nairobi leo hii ukiangalia utembeaji wa watu tuu utangundua kwamba tunatakiwa tujifunze kutoka kwao,shule nyingi za binafsi Tanzania wakenya wamejaa na Tanzania hatutaki kujifunza chochote kutoka kwao kwa sababu ya kuamini kuwa kujifunza kutoka kwa mtu ni kujipendekeza. Tulichowazidi wakenya ni ukarimu na Ukubwa wa eneo la nchi vingine wametuzidi sana.
Siyo peke yako uliyewahi kuishi huko, kama kweli uliwahi kukaa huko.

Uliyoandika hapa ni kama ni mwenyeji wa huko, au umeolea huko, na pengine kuwa na maslahi binafsi na huko.

Ndiyo, yapo waliyofanikiwa kuyafanya vizuri, mfano mzuri ni elimu yao iko imara zaidi, lakini hilo haliifanyi nchi hiyo iwe "...juu sana kwenye mambo mengi," kama unavyodai
"Raia kujitambua," una maana gani? Umefika kule Baringo ukakuta raia wapo tofauti sana na hawa waliopo Liwale katika kujitambua?
Unachukulia tu kakikundi uliko-'interact' nako hapo ulipofanya vikozi vyako ndiyo ukadhani kuna "seriousness, bidii na uwajibikaji, professionalism", ambayo huku Tanzania haipo mahali popote? Umefanya utafiti ukakupa majibu hayo?

Halafu unachekesha kweli: yaani hata "utembeaji" wa watu unauwekea uzito wai kuonyesha tofauti zilizopo kati ya watu walioko Nairobi na hawa , sijui wa Dar es Salaam au Tanzania yote?
Yaani unataka Tanzania twende Nairobi, tukajifunze kutembea kama wao? Hapo hali zetu ndipo zitakapoonekana kuwa nafuu kidogo kama wao?

Ninachohimiza waTanzania tujitahidi kukifanya kwa bidii zaidi kuliko kitu kingine kwa haraka zaidi, ni kuifanya elimu yetu iwe imara. Elimu yetu inaupungufu sana, na ndio maana, kama huyu 'Executive Sister' ni mTanzania kama inavyoonekana anadai yeye, anadiriki kuandika vitu vya ajabu sana kama alivyoandika hapa. Msingi wake wa elimu ulikuwa duni sana, licha ya kwamba hata hivyo vikozi alivyofanya huko Nairobi inaonyesha havikumsaidia kitu, kutokana kuwa na msingi mbovu tokea mwanzo.
 
Back
Top Bottom