Hakuna Taifa lililoendelea kwa kujipendekeza na kujidharau

Siko hapa kushindana kuishi ughaibuni. Na wala hakuna sehemu niliyosema ni mimi tu nipo ughaibuni au kuishi au kuwahi kufika huko. Soma uelewe. Hayo umeanzisha mwenyewe. Kuna maelfu ya watanzania ughaibuni. Nakuona weye huna hoja unataka leta ubishi wa kitoto. Hivyo napuuzia ulichoandika. Samahani sana sipo kubishana. Nipo kujenga hoja kwa watu waelewa waliona mawazo ya kujenga.
 
Sasa angalia upuuzi huu. Kenya nayo unaiita "ughaibuni"?

Mimi nimemjibu 'Executive Sister', hapa wewe 'Wilderness Voice' ni kipi kinachokuhusu?

Lakini hata kama ni wewe unayetumia majina mbalimbali humu, ninaridhika kabisa kwamba jibu nililokupa limekuondoa fahamu kabisa na kujiona jinsi ulivyoandika upuuzi katika bandiko lako nililolijibu.

Hili liwe ni fundisho kwako na wenzako, msiwe mnajiandikia tu vitu vya kipuuzi puuzi kudhalilisha taifa lenu (kama kweli nawe ni mTanzania mwenzangu).

Mnaudhi sana.

Utajengaje hoja kwa kulidhalilisha taifa lako, tena kwa mambo ya uongo? Nani atafaidika na hoja za namna hiyo?
 
Wewe uwezi ondoa ufahamu wangu kwa kuandika pasipo kuzingatia hoja. Na kisaikolojia mtu anapom attack mtu kwa maneno anakuwa na upungufu wa hoja. Kikubwa shusha hoja si shambulizi kwa mtu. Leta hoja ipimwe. Simaneno ya mipasho.
Kwa kifupi siko kama unavyofikiri, uwa sibabaiki kwa vijineno. Bali ninamkubali mtu anaejenga hoja nikaona hapa kweli pana hoja. Vijimaneno neno kwangu, uwa napuuza.
Karibu ujenge hoja.
 
Mkuu 'Widerness Voice', nadhani kuna kutoelewana hapa.

Mimi sikujibishana nawe mahali popote.
Hiyo uliyoni'quote' nilikuwa namjibu Executivesister, na wala sio wewe, sasa tatizo limetoka wapi?

Lakini, kama wewe ndiye unafahamika kwa jina lingine la Executivesister; bado sioni kama nilikushambulia binafsi bila ya kuishambulia hoja yako.
Jambo linaloumiza, kama wewe hujui, ni kuidhalilisha nchi yetu, kuidharau, kama Executivesister alivyofanya. Huko sio kujenga hoja, bali ni kutufanya sote tuonekane duni kwa hao unaowasifia, jambo ambao sio kweli kabisa.
Kenya hawatuzidi kiasi cha kuwaona wao ni bora zaidi yetu sisi.
 
Ok, Nimekuelewa ndugu yangu Kalamu 1: Samahani kwa nilipokukosea. Ni binadamu na kunakughafirika. Na Naamini Kenya sio wa kubabaikiwa!
 
Na hao wachina wanasema no hardship that will break you.
Burning spirit ilikuwa mapinduzi makuu ya uchumi kwa kwenda nchi jirani na kuibua ujuzi kutoka huko.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…