Hakuna tena sababu ya kukaa kwenye mahusiano kwa miaka 5 halafu mwanaume anakwambia anataka kuoa mwanamke mwingine!

Hakuna tena sababu ya kukaa kwenye mahusiano kwa miaka 5 halafu mwanaume anakwambia anataka kuoa mwanamke mwingine!

Magical power

JF-Expert Member
Joined
Sep 27, 2022
Posts
2,158
Reaction score
5,626
Hakuna tena sababu ya kukaa kwenye mahusiano kwa miaka 5 halafu mwanaume anakwambia anataka kuoa mwanamke mwingine!

Dalili zote za mwanaume ambaye anakutumia zinaanza kuonekana ndani ya miezi 3 ya mahusiano. Shida inakuja tu kuwa, baada ya miezi 3 ya mahusiano, wanawake wengi ni vigumu kuona ukweli. Kwa mfano, kama mwanaume wako mwanzoni alikuwa na mawasiliano mazuri – ni kawaida kwa mwanaume kupunguza mawasiliano baada ya miezi 3 ya kwanza. Labda mwanzoni alikuwa anakupigia simu mara tatu kwa siku, lakini baada ya miezi mitatu anaweza kupiga mara moja au hata kukaa siku mbili BILA ya kukupigia tena!

Hii ni kawaida na haina shida. Lakini kama mwanaume hana mapenzi ya kweli, ataweza kukaa wiki bila kukupigia simu. Mwingine unakuta kuonana inakuwa mpaka umembeleze sana, yaani lazima umsihi mwanaume aje kukuona, au ukimpigia simu anatafuta sababu za kukata na hakupigii tena. Kuna uwezekano kuwa tayari umeachwa.

Wanawake wengi wanapokutana na hali kama hii, wanaendelea kulazimisha. Unakuta mapenzi yanakuwa ya upande mmoja. Hii ni kwa sababu mwanamke anajiuliza, “Sasa nikiamua kuondoka, nikipata mwingine atakuwa hivi pia?” Hali ya kulala na kuendelea na wanaume wengi inaweza kukufanya uvumilie, bila kujua kuwa hata ukimvumilia miaka 10, kama amekusudia kukuacha, ataondoka tu!

“EPUKA KUDANGANYWA, ACHA KUPOTEZA MUDA.”


MWISHO
 
Mahusiano yakizidi miezi 6 hapo hamna kitu kabisa then punguzeni tamaa na kutuuliza una mpango gani na mimi
 
Back
Top Bottom