Hakuna tija yoyote ya Makundi ya WhatsApp kwa watu uliosoma nao kitambo

Hakuna tija yoyote ya Makundi ya WhatsApp kwa watu uliosoma nao kitambo

Ma-group ya WhatsApp ya watu wa zamani ni poa sana, ukisoma vitu unapata flash back ya nguvu, mnakutana mnachoma nyama na kupunguza stress, wachumba wa zamani una wamega, ni unyama sana unless kama haukusoma mjini
Huwezi kuwa rafiki au kuwajibika Kwa kuwachangia Kwa kila uliyesoma nae
Utakuwa nao baadhi mnaoendana
 
Tulimaliza Form four 2009
Hatuna mawasiliano yoyote baada ya shule
Shuleni hatukuwa marafiki kivile
Sasa mambo yamebadilika, tumekuwa wazazi, tuna majukumu mengine
Mijadala ya magroup haya ni mwalimu Fulani alikuwa anachapa, tulitoroka nk
Ambavyo Kwa Sasa havikusaidii

Suala la michango
Michango haikauki
Tulisoma wote baada ya hapo hatuwasiliani, leo unaona upo Mtwara nipo Musoma nitumie mchango ili iweje
Zaidi ya miaka 15 hujatengeneza circle mpya ya kukuchangia mpaka muweke mikeka ya michango na kutuchoresha sisi makauzu tusiochanga
Mikeka ya michango ya misiba
Usipoonekana kwenye mikeka kinyongo

Mikeka ya michango ni kero
Me siwezi kukosa kumchangia rafiki na jirani yangu Aboubakar akiwa anaona nikamchangia mtu aliyeko Tandahimba kisa nilisoma nae.

Tukiwa in touch nitachanga
Lakini siyo nione jina nianze kukumbuka eti huyu Rehema yule mfupi alikuwa anakaa mbele anaolewa sheria tuchange laki 10000, me sichangi hata 100


Ma groups yote nina mpango wa ku left kama haya ma kero ya mikeka ya michango yataendelea
Mtu ni watu. Jitahidi kuwa karibu na wenzako, usijitenge
 
Nachukia sana wale wanaokuja kwenye facebook na kuweka friend request!!!!! Ahhh jamaa eti tulikuwa mwaka mmoja college au university, so what? Miaka yote tulipokuwa tukisoma hata salamu hatukuwa tukipeana leo tuko nje na majukumu yetu ndio unataka kunijua? No way! Wengine eti tukikaa mtaa mmoja! So what? tulicheza pamoja? No! Kuna chochote tulichokuwa tukifanya pamoja tulipokuwa wadogo? No! Sasa unaniomba friend request ili iwe nini? Tuzungumze nini ilhali hatuna anything in common?
Mi Fb ndo imenishinda kabisa sipogo huko
 
Nina magroup 9 mengine ni magroup ndani ya group...yote school mates....😊😊😊kuanzia la shule ya msingi...
Kati ya yote nalipenda la shule ya msingi...pale tunakua wote tunacheza mtaa mmoja...maisha ya kijamaa kabisa watu wanakumbushia kumbe walikua wana kucrashia ww hujui..si bado mtoto...😄😄😄😄kwa sasa tumekua wakubwa tuna miji yetu na familia zetu..tuna share good memories za miaka zaidi ya 20.....it is amazing...
 
Back
Top Bottom