Hakuna Timu ya kuifunga Simba SC, Kituo kinachofuata ni Iringa, Kila timu ishinde mechi zake!

Hakuna Timu ya kuifunga Simba SC, Kituo kinachofuata ni Iringa, Kila timu ishinde mechi zake!

Ligi Kuu ya Tanzania kwa mzunguko huu wa lala salama, hakuna Klabu ya mpira yenye uwezo wa kuifunga Simba SC kutokana ubora wa kikosi.

••Watafanya Nini Sasa Uwezo Hamna

Simba SC imekuwa ikitandaza gozi la ng'ombe vema kabisa kwa viwango vya juu, huku wakipiga pasi za maana zilizothibitishwa na Shirikisho la soka Afrika (CAF) na kusababisha Simba SC kupata matokeo chanya.

Klabu hiyo ya Wekundu wa Msimbazi wao wanachokifanya ni kutiririka tu kwenye mtelemko wa kuzoa pointi tatu kila mchezo, Yanga kachukua kidude 1-0 Uwanja wa Taifa, African Lyon kagaragazwa 3-0 Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Azam FC kachapwa 3-1 Uwanja wa Taifa, klabu ambazo kidogo zilikuwa zikitegemewa kuleta upinzani wa kupata walau sare, kwa mukhadha huo hakuna kwa sasa timu ambayo itaifunga Simba SC kwenye TPL.


••Mwana Kulitaka Mwana Kulipewa

Katika mwendelezo wa kukusanya pointi tatu tatu kila sehemu, kwa sasa kituo kinachofuta ni Ipogolo mkoani Iringa ambapo Lipuli watalazimika kushuka katika eneo lao nakuacha pointi tatu huku safari ya Watakatifu Simba ikiendelea.

Klabu ya Simba imeondoka leo kuelekea mkoani Morogoro ambapo leo jioni watafanya mazoezi kisha kesho asubuhi wataanza safari kuelekea mkoani Iringa ambako Jumanne itakipiga na Wanapaluhengo Lipuli FC.

Niiii Ghazwat kwa niaba ya sembo OKW BOBAN SUNZU Shunie King Ngwaba Sapta Sapta Tui tunawaambia watani zetu Sibonike Mwana Mtoka Pabaya Shadeeya Prince Kunta Kila timu ishinde mechi zake..!View attachment 1030312View attachment 1030313View attachment 1030314

Sent using Jamii Forums mobile app
Hii ya KITUO KINACHOFUATA NI IRINGA ungemalizia kabisa ni kwa sauti ya yule mdada wa mabasi ya Mwendokasi (UDART)
 
Hii ya KITUO KINACHOFUATA NI IRINGA ungemalizia kabisa ni kwa sauti ya yule mdada wa mabasi ya Mwendokasi (UDART)
Naam [emoji23][emoji23][emoji3][emoji3]
 
Leo ni leo Uwanja wa Samora..Lipuli FC dhidi Simba SC, kwa waliojirani wajongee kushuhudia kipute hicho

Kumbuka mechi kuanzia saa kumi jioni.
 
Ni mapumziko Lipuli FC 1-2 Simba SC
 
What a coincidence!!! Refa aliyechezesha Mikia na Lipuli Taifa....kachezesha tena leo Iringa
 
What a coincidence!!! Refa aliyechezesha Mikia na Lipuli Taifa....kachezesha tena leo Iringa
Kwahivyo alipochezesha Taifa na matokeo yakawa droo mkashangilia mlijua Kesho ndo Jana [emoji23] [emoji23]

Soma heading utaelewa mkuu..SimbaNguvuMoja
 
Back
Top Bottom