Hakuna Ubaya Wowote kwa Mtu Yoyote, Taasisi Yoyote, Nchi Yoyote Kusaidiwa Pale Inaposhindwa, Muhimu ni Kuwa Makini Tusipigwe. Je DPW Tunapigwa?

Watanzania hawana tatizo na DP world kupewa bandari. Tatizo la watanzania liko kwenye mkataba unaoingiwa kati ya serikali na na DP world!

Mnakomaa sana kukwepa hoja za msingi kwa visingizio vya kipuuzi kabisa. Maswali makuu ya watanzania ni haya;


.- Mkataba unaoingiwa una ukomo gani? DP world wanapewa bandari yetu kwa muda gani?

- Kama tukiamua kuvunja huo mkataba baada ya miaka kadhaa, kuna win-win situation kwa pande zote mbili?

- Bandari ni lango kuu la nchi, je vigezo vya kiusalama vimezingatiwa?

- DP world wanawekeza kiasi gani na mgawanyiko wa mapato utakua vipi? Je, mkataba unatuhakikishia usalama wa gawio letu la hayo mapato?



Badala ya kuwaita watanzania wajinga, hawana elimu, hawataki kukubali kushindwa, hebu jikiteni kwenye kujibu hoja za msingi ili waelewe kama huo mkataba uko na manufaa kwao au La!

Tulipigwa kwenye migodi na watu walewale, tulipigwa kwenye gesi na watu walewale, leo tena watu walewale wanataka kutuingiza kwenye mkataba wa bandari. HATUWAAMINI!
 
Hivyo Watanzania tuache nongwa, tunaposhindwa jambo fulani, tusione aibu kusema tumeshindwa!, tuanze kuomba msaada kwa Watanzania kwanza, tukikosa ndio twende kwa wageni kutafuta msaada kwa uwazi na ushirikishwaji.
Aliyewaambia tumeshindwa ni Nani? Yaani unajenga mifumo ya hovyo, then unajitokeza hadharani na kusema umeshindwa unaomba kusaidiwa, Mzee Paskali hakuna mentality mbaya kama hii ya kutaka kusaidiwa, msaada! Unaambiwa wewe ni mnyonge, then unaambiwa Kwa kuwa wewe ni mnyonge basi unahitaji kusaidiwa! MUNGU atusamehe
 
Tunavyoelekea kwenye Multipolar World order, Tunahitaji zaidi strong locally-owned private sector. Lakini, wamefanya iwengumu sana kwa startups, ngumu sana kwa already established businesses amabazo hazina muelekeo wa chama .
 
Hawawezi kukujibu kamwe! Wanachofanya akina Paskali ni kujipendekeza kama akina Balile Ili nao wawe sehemu ya mgao huu dhalimu
 
P
Yapi maoni yako kuhusu DP World?
Au na wewe umeshalambishwa bahasha?
[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16]
Karibu sana.
Kwanza nilianzia hapa, Watanzania tujifunze kukubali kuna vitu hatuwezi, tunaposhindwa tukubali kusaidiwa au tukomae? Baada ya Bandari ni ATCL na SGR au Tusubirie?

ikaja kuwaomba waheshimiwa wabunge wetu, kwenye kuridhia IGA ya DPW, watangulize mbele maslahi ya taifa Wabunge Wetu, Macho ya Watanzania Wote Leo ni Kwenu!. Maslahi ya Taifa Mbele!. Tuwaogope Kama Ukoma Muflis Hawa!, Kama Huwezi, ni Lazima Usaidiwe Tuu!.

Na baada ya Bunge letu Tukufu kuridhia mkataba huo bila kufanya due diligence yoyote kumhusu Mwarabu wa Dubai na hadhi ya mkataba wenyewe, kwanza nikasisitiza kuunga mkono hoja, Hakuna Ubaya Wowote kwa Mtu Yoyote, Taasisi Yoyote, Nchi Yoyote Kusaidiwa Pale Inaposhindwa, Muhimu ni Kuwa Makini Tusipigwe. Je DPW Tunapigwa?.

Kisha nikahoji uwezo wa Bunge letu na uwezo wa wabunge wetu kujadili jambo kubwa kama hili Bunge letu ni Bunge la ovyo? Bunge linafanya Uhuni? Wabunge Wetu ni Wahuni? Tumshauri Spika naye aanze kuita Watu kwenye Kamati, au waachwe tu? .

Pia nikatoa angalizo la maeneo yenye ukakasi ili HGA iwe imenyooka Japo Bunge Limeridhia, DPW Kuendesha Bandari Zetu, ni Makubaliano Tu, Tukithibisha Kuna Matatizo, Tunarekebisha Mkataba wa HGA, Kazi Nzuri Iendelee! na kesho Jumapili, nitaandika makala kwenye gazeti la Nipashe kuhusu huu mkataba
P
 
Kwenye mpira wakiletwa kina Mayele na Chama na Nabi kila mtu anaelewa....
Kwenye mambo ya uchumi kama bandari wakiletwa wenye uwezo zaidi kusaidia ..makelele Tele...Utasikia kwanini tusifanye wenyewe...
Mbona mpira hamtaki tucheze wenyewe
 
Kwenye mpira wakiletwa kina Mayele na Chama na Nabi kila mtu anaelewa....
Kwenye mambo ya uchumi kama bandari wakiletwa wenye uwezo zaidi kusaidia ..makelele Tele...Utasikia kwanini tusifanye wenyewe...
Mbona mpira hamtaki tucheze wenyewe
Huu ndio Dr Nshala aliuita upumbavu.
 
Ukishindwa unajiuzulu anakuja mwenye uwezo zaidi yako sio unashindwa unaendelea kukaa hapo kwani kwako?
 
Kwenye mpira wakiletwa kina Mayele na Chama na Nabi kila mtu anaelewa....
Kwenye mambo ya uchumi kama bandari wakiletwa wenye uwezo zaidi kusaidia ..makelele Tele...Utasikia kwanini tusifanye wenyewe...
Mbona mpira hamtaki tucheze wenyewe
Huwezi kutoa mifano ya darasa la tatu
 
Kwenye mpira wakiletwa kina Mayele na Chama na Nabi kila mtu anaelewa....
Kwenye mambo ya uchumi kama bandari wakiletwa wenye uwezo zaidi kusaidia ..makelele Tele...Utasikia kwanini tusifanye wenyewe...
Mbona mpira hamtaki tucheze wenyewe
😡
 
Huu mpango wa kumpa Mwarabu wa Dubai kutuendeshea Bandari yetu, ni mpango wenye maslahi makubwa kwa taifa la Tanzania, tuunge mkono ila tuwe makini na huyu Mwarabu wa Dubai maana...!.
Unafiki sikuzote huwa hauna maana unawezaje kuwa makini namtu ambaye ana full power pamoja na control yahali yajuu kutokana namkataba ambao unampa priolity nahaueleweki mwisho wake?!?!?
 
Hapana hatupigwi mkuu. Hatuwezi kusema sisi hapa jamvini tunajua sana kuliko vyombo vyoooote vya dola kama
1. Baraza la mawaziri
2. TISS
3.TPA
4. TAKUKURU
5. BUNGE.
Mimi naona tuache wasiwasi na tuwaamini wanaotuwakilisha basi.
 
Hapana hatupigwi mkuu. Hatuwezi kusema sisi hapa jamvini tunajua sana kuliko vyombo vyoooote vya dola kama
1. Baraza la mawaziri
2. TISS
3.TPA
4. TAKUKURU
5. BUNGE.
Mimi naona tuache wasiwasi na tuwaamini wanaotuwakilisha basi.
Kwani tulivyopigwa kwenye mikataba mingi ya kilaghai huko kwenye madini, hivyo vyombo havikuwepo au wewe ni mtoto mdogo huelewi chochote Wizi kupitia mikataba
 
Wananodi hii Makala ya Nipashe ya leo 11/06/2023
View attachment 2653617View attachment 2653619
Haa🥱
Lakini umejiuliza ni kwanini tumeshindwa?
Kuna vitu sisi Watanzania wenyewe hatuwezi!, na inapotokea kuna vitu hatuwezi, tunapojaribu kuvifanya na tukashindwa, lazima tujikubali hili tumeshindwa, hatuwezi!.
Umejiuliza kwanini hatuwezi? Kwanini tunashindwa?
Swali ni unaposhindwa kuna ubaya wowote kukubali kusaidiwa au tuendelee tuu kujitutumua tukomae tuu mpaka tuweze?
Too much repetition "kushindwa, kushindwa".

Jaribu kuwa aggressive ktk kujenga hoja zako vyema ili uwashawishi wenye akili zao wakuelewe..!

Lakini bado hujibu swali muhimu la chanzo Cha kushindwa kwetu kama nchi nini!

Au unadhani tulizaliwa kushindwa tu? Je, hudhani kuwa kuna sehemu tulikosea na kujilaza kwenye njia ya kushindwa?
Kiukweli kabisa uamuzi wa kulipa kampuni ya Dubai kutuendeshea Bandari yetu ya Dar es Salaam, Dar Port, ni uamuzi sahihi, kwasababu sisi tumeshindwa,
Kwanini tumeshindwa? Mbona makala ni ya kipropaganda zaidi badala ya kufanya deep analysis kama mwandishi kweli wewe??
tena kwa maoni yangu, sio Bandari pekee, hata kuiendesha ATCL kwa faida sisi wenyewe peke yetu hatuwezi, lazima tongie ubia!. Hata tukija kwenye SGR ndio kabisa!, lazima tushirikiane na wajuvi wenye uzoefu, wakati tukijenga uwezo
Please, answer the question!

Kwani unadhani tunashindwa? Tukusaidieje sasa maana hutoi sababu za kushindwa kwetu ili tuzipime Kisha mwenye za tofauti akusaidie?

What's wrong with you dude?
wetu wa ndani.

Kuna vitu Watanzania hatuwezi na tunashindwa sio kwasababu ni vilaza, au hatuna uwezo, tunashindwa kwasababu tuu hatujui kutazama mbali!.
Kutazama mbali wapi? Tumepata uhuru mwaka 1961. Kina nani hawa wasiotazama mbali?
Mfano saa hizi tuko busy kujenga SGR, lakini hatuna mkakati wowote wa kujiandaa kwa mzigo wa kuiendesha hiyo SGR kwa faida ndio tukaja na Bandari ya Bagamoyo.
Still the question is;

Kwanini tumeshindwa kufikiri hivyo? Nani anakwamisha watu kufikiri hayo? What do you think is the problem?

Kama unamtumia akili yako vyema kufikiri na ukajibu swali hili kwa usahihi, basi utaelewa shida iko wapi!!
Kuendesha Reli ya SGR kwa faida sio mchezo!. Wenzetu Kenya yameshawakuta, wanaiendesha SGR yao law hasara.
Una justification ya tuhuma hii? Where is the evidence?
Jee sisi tusubirie SGR yetu ikamilike, tujaribu kuioparate tushindwe ndipo tutafute usaidizi?
Kama tutaendelea na mfumo wa kisheria na kikatiba ambao umezaa mfumo huu mbovu na wa hovyo wa kiutawala, mambo yatakuwa hivihivi bila shaka...!!
au wakati ujenzi unaendelea, tutazame mbali kwa kujenga uwezo wa uendeshaji na maandalizi ya kutafuta mzigo wa kushiba wa kubebwa na SGR?.
How?

Je, ni kwa kuutumia mfumo wa "mfumo wa utawala wa u - Rais wa kifalme?"
Swali kwako ndugu mwandishi wa habari ni lilelile..

Kwanini tunashindwa?

Go back to your desk, think and come out with answers..!!
Kuna ubaya kuwaita watu wenye uwezo wakuendeshee kwa kipindi fulani huku unajenga uwezo wa ndani kuendesha, ukiwa tayari ndipo uendeshe?.
Ukianika sababu za kushindwa kwetu na zikawa beyond our control, tutasema HAKUNA UBAYA WOWOTE...!

Lakini as it is for now, Kuna Kila aina ya ubaya kuiuza bandari yetu Kwa waarabu...!!
ATCL, tushukuru Magufuli kwa kuwa bold kukimbilia kununua midege kwa cash kwa mtindo wa kupiga tanchi, bila kuwa na business plan!.
Unaji - contract mwenyewe!!

Huko juu umeandika nini kuhusu ATCL? Si umesema inajiendesha kwa hasara? Na hapa unashukuru kitu gani?

Kwanza ni kwanini Magufuli anunue ndege yeye Tena Kwa kutumia mfumo huo wa cash?

Hujui kwamba hapa ndipo kilipo chanzo cha matatizo ya nchi yetu kushindwa kipujisimamia?

Yaani kuingia siasa za "mkono wa Rais" kwenye kila eneo na taasisi?

Wewe unafikiri kwanini watu wanasema "Rais katupa hela kujenga choo au barabara au kisima cha Maji au stendi?

Wewe unadhani insposikika hivi ni dhana gani inaingia Kwa watendaji na wasimamizi wa hizo taasisi?

Kama hujui, nitakusaidia kujua:


Watasema; "hela za Rais hizo. Kama anatupa hizi, yeye kachukua ngapi eti? Uamuzi ni ....CHUKUA CHAKO MAPEMA - CCM!!"
Answer the question, why things are like that? What is the problem?
Pale unaposhindwa kitu fulani, hakuna ubaya wowote kuomba msaada kwa wenye uwezo usaidiwe!.
Not that way!

Si kwa kwa viongozi hawa kuuza sovereignty ya nchi ya watu !

But the question still stands: Why things are like that?
Tuliwahi kujaribu kwa ATC, TTCL, Tanesco, Dawasco, tukaja kuvunja mikataba hiyo.
Why?

Mbona unazunguka zunguka tu husemi sababu?

Si Unataka tusaidiwe? Si ulisaidiwa? Sasa what happened ukavunja mikataba tena?

Na sasa Unataka iwe hivyo? Why?
Kuna msemo wa Kiswahili usemao, "Ukitaka kula ni lazima uliwe!", hivyo hata huu mkataba wa Bandari, kwavile tunataka kula, ni lazima tuliwe!. Wazungu wanasema "You can't eat your cake and have it!".
Does it relate with what you've written in your article?
Kuna vitu vingi tuu tunashindwa na tunaomba msaada tunasaidiwa. Jengo la BOT lilipoungua, polisi wetu walishindwa kufanya uchunguzi, tuliomba msaada wa polisi wa Uingereza, The Scotland Yard, wakatusaidia.
Linahusiana vipi na bandari, reli, ATCL nk nk ?
Hakuna uwezo siyo?
Kuna watu wanadhani Scotland Yard, wanazaliwa na uwezo huo!, no!, Scotland Yard wanafanya scouting kuwapata watu wenye uwezo huo!, hapa Tanzania watu hao tunao lakini hatuwatumii!.
Kumbe unajua kuwa no body is born with some skills. Everything is learnt, right?

If you know these, what made us tuwe watu wa kushindwa tu...???
Niliwahi kuuliza WanaJF, je tuisaidie Serikali yetu inaposhindwa au tusubiri ishindwe, tuibeze na kuizomea kuwa haiwezi?.
Ushauri mzuri na muhimu kwa sasa ni mmoja tu brother Pascal Mayalla ili nchi itoke kwenye mkwamo wa tope hili la "kushindwa" ni;

Kutengeneza mfumo mpya wa kiutawala unatengeneza taasisi imara zenye watu walio huru kimawazo na ubunifu Kwa sisi sote kama taifa kukaa chini na kukubaliana namna gani tujitawale na makubaliano haya tuya - document kwenye nyaraka muhimu iitwayo KATIBA MPYA...

Haya mengine yote ni porojo na propaganda za kisiasa tu.

MWISHO:
Narudia tena kusema; Lakini kama mtu unayefikiri vyema, umewahi kujiuliza maswali haya mawili muhimu;

1. Kwanini sisi kama nchi tunashindwa kuendesha baadhi ya mambo yetu likiwemo la bandari linaloleta shida sasa?

2. Kama tulijiuliza, then tulipata sababu ni zipi? Na way forward ili kutoka hapa tulipo ni nini?


Nafikiri kama mwandishi wa habari mahiri, ungeanza kujenga msingi wa makala yako hii kwa kwanza kujibu maswali hayo muhimu...

Lakini nimekusoma mpaka mwisho, naona nawe umetumia uhuru wako wa kutoa maoni Kwa mtindo uleule wa kukwepa kusema ukweli na kuanza kulalama kipropaganda tu kama walivyo wana CCM wengi watafuta vyeo vya uteuzi Kwa sababu mfumo wetu utawala wa nchi umejengwa katika msingi huu mbovu na WA hovyo kabisa...

Na kimsingi hili ndilo tatizo kubwa tulilonalo kama nchi na ndiyo msingi wa matatizo yote. Na Kamwe ishu siyo kuwa Watanzania hawezi kuendesha mambo yao kwa ufanisi na kuleta matokeo...

Bali wamefanywa hivi na mifumo yetu ya hovyo na dhaifu ya kisheria na kikatiba iliyozaa mfumo mbaya na wa hovyo na dhaifu wa utawala wa nchi yote...

SULUHISHO:

NI KATIBA MPYA itakayozaa MFUMO MPYA WA KISIASA na KIUTAWALA katika nchi na kutengeneza TAASISI IMARA..
 
DP WORLD Tumepigwa brother. Hilo Halina ubishi
 
Mkuu Pascal Mayalla kwanza kabisa nikupongeze kwa kujaribu kuidadavua na kuitolea ufafanuzi hoja yako.

Mimi binafsi niseme Tanzania hatujashindwa ila iliyoshindwa ni serilikali inayoongozwa na chama cha mapinduzi(ccm).Hiyo ndiyo iliyoshindwa kuhusu kusimamia sheria na katiba kuhusu masuala la nchi lakini watanzania hawajashindwa!.

Ripoti ya CAG kila mwaka inaonyesha kuna upotevu mkubwa wa mapato hapo bandarini,pamoja na ripoti hiyo lakini hatuoni hatua zikichukuliwa zaidi ya kubadirishwa watendaji na wale walioondolewa kupewa kazi nyingine,sasa hapo tatizo ni watanzania au serikali?

Kama ni kushindwa basi kuna taasisi kibao za serikali zimeshindwa kuonyesha matokeo chanya kutokana na ripoti ya CAG,itakuwa vema na hizo taasisi zikabinafisishwa ili kuleta ufanisi.

Tatizo kubwa la hii nchi ni sheria hazifuatwi na kulindana ndiko kwingi,Rais anapopaswa kuacha sheria ichukue mkondo wake yeye anabaki kucheka cheka tu na walanguzi na mafisadi.

Bunge halitekelezi wajibu wake kama bunge bali limekuwa sehemu ya serikali na kusifia kila upumbavu.

Mahakama kama muhimili unaojitegemea nao umebaki kutekeleza maagizo ya watawala badala utimize wajibu wake.

Hii nchi miimili hii ikitimiza wajibu wake kisheria na kikatiba wala hatuna haja ya kuuza bandari mkuu haya yote yanafanyika kwasababu sheria hazifuatwi na kuna uvunjifu mkubwa wa kikatiba!.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…