Hakuna ubishi, bila biblia, hakuna uislam. Kama ukristo ungedukua na kukopi na kupaste quran, hali ingekuwaje?

Utabisha na kwamba Synagogue zote duniani zimeelekezwa Middle East kama ilivyo misikiti.

Hizo dini zenyewe hamjui kutwa kusambaza chuki.
Mimi Sina chuki na dini yoyote , umeona natoa lugha Kali na mihemko?

Jenga hoja tu utaeleweka, kwanza Sio kweli Lazima Sinagogi lielekezwe Mashariki,

Ni kweli Wayahudi wa kawaida huomba kuelekea Yerusalemu, kama inavyoonyeshwa katika Danieli 6:10, lakini tofauti ni kwamba Wayahudi hawajafanikisha utaratibu wa kudai kwamba kila sinagogi duniani lazima lionyeshe mwelekeo wa Mashariki ya Kati. Mwelekeo huu mara nyingi ni wa kiroho na si wa kimuundo.

Tofauti na misikiti, ambapo mihrab huonyesha mwelekeo wa Makka, hakuna sheria kali inayosema kuwa sinagogi lazima zielekezwe Yerusalemu. Uelekeo ni mazoea yanayopendelewa, lakini si lazima.

Wayahudi huamini maombi yao yanaweza kufika kwa Mungu popote bila kujali uelekeo. Hii inatofautiana na Uislamu, ambapo mwelekeo wa Kibla ni sehemu muhimu ya ibada.

Shida yako moja unapaniki ,haya jibu maswali yangu haya 👇👇👇

1. Ikiwa kila sinagogi limeelekezwa Middle East, je, unaweza kutaja ushahidi wa kihistoria au usanifu wa sinagogi ulimwenguni unaothibitisha hili?

2. Kwa nini maombi ya Wayahudi kama ilivyoonyeshwa kwa Danieli 6:10 yanaweza kufanywa popote, wakati katika Uislamu mwelekeo wa Kibla ni wa lazima kwa sala?

3. Je, uelekeo wa misikiti kuelekea Makka unahusianaje na maana ya kiroho ya ibada, ukilinganisha na Wayahudi ambao wanasisitiza ibada ya moyo bila kuzingatia sana mwelekeo?

4. Kwa nini sinagogi nyingi za kisasa hazifuati kabisa kanuni ya kuelekea Yerusalemu, ikiwa ni muhimu sawa na Kibla kwa Waislamu?

5. Kwa kuwa ibada za Wayahudi zilifanyika katika hekalu la Yerusalemu zamani, je, huoni tofauti kati ya hekalu (ambalo lilikuwa mahali maalum) na sinagogi za sasa ambazo zinaweza kujengwa popote?
 
Fungu lako Ni hili hapa..

Ufunuo wa Yohana 12:7-10, 12
7 Kulikuwa na vita mbinguni; Mikaeli na malaika zake wakapigana na yule joka, yule joka naye akapigana nao pamoja na malaika zake;

8 nao hawakushinda, wala mahali pao hapakuonekana tena mbinguni.

9 Yule joka akatupwa, yule mkubwa, nyoka wa zamani, aitwaye Ibilisi na Shetani, audanganyaye ulimwengu wote; akatupwa hata nchi, na malaika zake wakatupwa pamoja naye.

10 Nikasikia sauti kuu mbinguni, ikisema, Sasa kumekuwa wokovu, na nguvu, na ufalme wa Mungu wetu, na mamlaka ya Kristo wake; kwa maana ametupwa chini mshitaki wa ndugu zetu, yeye awashitakiye mbele za Mungu wetu, mchana na usiku."

12 Kwa hiyo shangilieni, enyi mbingu, nanyi mkaao humo. Ole wa nchi na bahari! Kwa maana yule Ibilisi ameshuka kwenu mwenye ghadhabu nyingi, akijua ya kuwa ana wakati mchache tu.

Andiko Lako nalijua sasa nataka Unijibu maswali yangu machache kabla Sijakujibu Mimi..

  1. Shetani aliasi Baada ya Binadamu Kuumbwa au kabla ya Binadamu Kuumbwa?
  2. Binadamu aliumbwa mbinguni akawekwa Ardhini chini au aliumbwa ardhini akawekwa Kwenye edeni ambayo iko mahali?
  3. Shetani alikuwa na Malaika wake? Maana alikuwa na Nguvu sawa na Mungu?
  4. Baada ya Adamu kufukuzwa Edeni alipelekwa Wapi
  5. Na Shetani alifanya kosa gani akafukuzwa Mbinguni
Ngoja Mimi nijibu

1. Shetani aliasi kabla au baada ya binadamu kuumbwa?

Majibu:
Maandiko hayaonyeshi waziwazi kama Shetani aliasi kabla au baada ya binadamu kuumbwa. Hata hivyo, tukirejelea Mwanzo 3, tunamwona Shetani tayari akiwa ameanguka kwa sababu alijaribu kumdanganya Hawa. Hii inamaanisha uasi wake ulitokea kabla ya tukio hilo.

Katika Ufunuo 12:7-9, tunaona vita mbinguni ambavyo vilisababisha kuangushwa kwa Shetani na malaika zake. Tukio hili linaweza kufasiriwa kuwa lilitokea kabla ya uumbaji wa binadamu, lakini baadhi ya wanatheolojia wanaamini linaweza pia kufungamana na ukamilifu wa kazi ya Kristo duniani.

2. Binadamu aliumbwa mbinguni akawekwa ardhini au aliumbwa ardhini akawekwa Edeni?

Majibu:
Mwanzo 2:7 inasema, “Bwana Mungu akamfanya mtu kwa mavumbi ya ardhi, akampulizia pumzi ya uhai; mtu akawa nafsi hai.” Hii inaonyesha kuwa binadamu aliumbwa ardhini. Baada ya kuumbwa, Mwanzo 2:8 inasema Mungu alipanda bustani huko Edeni na kumweka binadamu ndani yake. Edeni haikuelezwa kama mbinguni, bali kama mahali maalum hapa duniani.

3. Shetani alikuwa na malaika wake? Je, alikuwa na nguvu sawa na Mungu?

Majibu:
Ndiyo, Shetani alikuwa na malaika wake. Ufunuo 12:4 inasema "Mkia wake wakokota theluthi ya nyota za mbinguni, na kuzitupa katika nchi." Nyota hizi zinatafsiriwa na wanatheolojia wengi kuwa ni malaika walioasi pamoja naye.

Hata hivyo, Shetani hakuwa na nguvu sawa na Mungu. Shetani ni kiumbe aliyeumbwa (angalia Ezekieli 28:12-15). Mungu ni Mwenyezi na hana usawa wake (Isaya 45:5). Shetani alijaribu kujiinua juu ya Mungu (Isaya 14:12-15), lakini akashindwa.

4. Baada ya Adamu kufukuzwa Edeni, alipelekwa wapi?

Majibu:
Mwanzo 3:23-24 inasema Adamu alifukuzwa kutoka bustani ya Edeni na kuishi mahali pengine duniani. Haielezwi hasa aliishi wapi, lakini maandiko yanaonyesha aliendelea kuishi duniani, akifanya kazi ya kulima ardhi ambayo ililaaniwa (Mwanzo 3:17-19).

5. Shetani alifanya kosa gani akafukuzwa mbinguni?

Majibu:
Shetani alikosea kwa kuonyesha kiburi na kutaka kuwa kama Mungu. Ezekieli 28:17 inasema, “Moyo wako uliinuka kwa sababu ya uzuri wako, ukaharibu hekima yako kwa sababu ya fahari yako.” Isaya 14:12-14 inaeleza zaidi jinsi Shetani alivyotamani kujiinua juu ya Mungu. Kosa hili la kiburi na uasi ndilo lililomfanya afukuzwe kutoka mbinguni.
 
Kama Yesu dini yake ilikuwa Uyahudi wewe ukristo umeupata wapi?

Yesu alikuwa myahudi wa kabila sio dini

Hivi wewe unazijua core believe za dini ya Uyahudi?
Ili dini yako iwe Uyahudi lazima umkane Yesu

so unataka kusema Yesu alijikana mwenyewe ndio akawa muumini wa dini ya kiyahudi?

Kama Uyahudi ni dini vipi Isaka na Yakobo dini Yao ni ipi?
Maana mtoto wa Yakobo aliyeitwa Yuda na watoto wa Yuda wakaitwa Wayahudi na baadae ndio Kuna watu hilo kabila la wayahudi wakalifanya ndio dini yao

Wakristo na Wayahudi wote mmepotea
Mimi sio Mkristo Mkuu!
Yesu alikuwa Myahudi wa Kabila na Dini na Ndo maana Aliingia Sinagogini na Hekaluni..

Hakuna aliyeruhusiwa Kuingia Hizo sehemu isipokuwa Ni wa kariba yake..
Utakumbuka Hata Yesu wanafunzi walimwita Rabbi..
Rabbi ni Cheo cha Juu sana Cha mwalimu wa Dini ya Kiyahudi
Yaani mwenye Maarifa na Kutafundisha maarifa hayo..

Cheo cha rabbi hakitolewi Hivi hivi mpaka Uonekane umekidhi Vigezo Vinginevyo kama Unajua Dini na Unafata masharti ungeitwa Tu farisayo na Sio Rabbi.

Kama Paulo alikuwa Farisayo ila Hakufikia Level ya Rabbi..

Kuhusu basic Believe za dini ya Kiyahudu nazijua Vizuri sana kwa sababu niliwahi kuwa Myahudi..

Na Nilipita Yeshiva (Shule ya Kiyahudi)

KWa Hiyo ni Tusi sana Kumuuliza Avreich au Kollel au hata ukimkuta Yeshiva bochur kuhusu Basic Za Talmud, Torah Au halakah ni Tusi..

Kuhusu Yakobo na Isaka hawakuwa na Dini bali walikuwa na Muongozo wa kama wao..
Huitaji Dini Unapokuwa Unaongozwa Moja kwa Moja unahitaji dini (Njia) pale ambapo Muongozo umechafuka
 
Wewe ni muongo mkubwa

Ibada za kiyahudi tofauti na waislamu

Wayahudi: Wana ibada kama sherehe za Pasaka, Shabati, na Sikukuu nyingine ambazo ni maalum kwa utamaduni wa Kiyahudi. Katika ibada zao, kuna sheria za kutii Torah na Talmud.

Waislamu: Waislamu wana ibada kama Salah (sala), Hajj (hija), na Zakat (sadaka). Waislamu wana sheria kali za kufunga mwezi wa Ramadhani na sherehe za Kiislamu.
Ibada za Kiyahudi Zinafahana na Za Kiislamu kwa Asilimia 80
 
Kuna maswali nimekuuliza sijui hujayaona ,Mimi nimekuwa muislamu nikauacha ,sasa nataka kurudi ila ukinijibu haya maswali

Usoyaone yakawaidia ukayakurupukia ,

1. Kama Yesu alikuwa Muislamu, kwa nini alizungumza kuhusu utawala wa Mungu na ufalme wa mbinguni, na si kuhusu Uislamu kama unavyojulikana leo?

2. Katika maandiko ya Biblia, Yesu anajiita "Mwana wa Mungu" (Mathayo 16:16, Yohana 10:36), jambo ambalo halifanani na mafundisho ya Uislamu. Je, unaweza kuelezea jinsi Yesu anavyoweza kuwa Muislamu na kusema hivi?

3. Uislamu ulianza karne kadhaa baada ya Yesu kuzaliwa, kwa hivyo, ni vipi Yesu, ambaye alikuwa akifundisha mapenzi ya Mungu, alijua kuhusu dini hii (Uislamu) ambayo haikuwa imeanzishwa bado?

4. Katika Injili, Yesu alifanya ibada katika sinagogi (Mathayo 4:23, Luka 4:16), na si katika msikiti. Je, unaweza kuelezea kwa nini Yesu alifanya ibada katika sinagogi na si katika msikiti, kama Uislamu unavyotaka?

5. Uislamu una mafundisho tofauti na yale Yesu aliyoyafundisha kuhusu wokovu, kufa kwa Yesu, na ufufuo. Je, ni vipi Yesu alikubaliana na mafundisho ya Uislamu kuhusu wokovu na maisha baada ya kifo, kama alikufa msalabani kwa ajili ya dhambi za wanadamu (Yohana 3:16)?

Wala usirudi katika uislam wewe endelea kuwa mgalatia Ili uende Jahanamu

Najibu maswali yako kama ifuatavyo

1) Ufalume wa mbinguni au uzima wa milele
Yohana 17:3
Na uzima wa milele ndio huu, Wakujue wewe, Mungu wa pekee wa kweli, na Yesu Kristo uliyemtuma.

Yesu anasema Ili mtu aende peponi lazima ukubali kuwa Mungu ni mmoja na Yesu ametumwa na huyo Mungu mmoja
Wewe siku ukiliamini hili andiko utakuwa Muislam maana waislam ndivyo tunavyo amini

2) Mungu hana mtoto kwanza Mungu sio Mwanamume Wala sio mwanamke kike na kiume hizo ni sifa za viumbe vilivyoumbwa na Mungu hivyo basi Mungu ndio ameumba kiume na kike

Lakini pia Mungu ana majina mengi kama nyinyi mmeamua kumuita Mungu baba hilo halina shida lakini je! Kwanini nyinyi mnajitoa na kusema kuwa Yesu ni mtoto wa Mungu hilo halikubaliki kama ungesema wewe na Yesu ni watoto wa Mungu tungejua ndio staili yenu ya kumtukuza Mungu
Na Kwa mujibu wa maandiko ipo sehemu Yesu amesema binadamu wote pamoja na yeye ni watoto wa Mungu Kwa Nini nyinyi mlazimishe kuwa Yesu ndio mtoto wa Mungu?

Yohana 20:17
Yesu akamwambia. Usinishike; kwa maana sijapaa kwenda kwa Baba. Lakini enenda kwa ndugu zangu ukawaambie, Ninapaa kwenda kwa Baba yangu naye ni Baba yenu, kwa Mungu wangu naye ni Mungu wenu.

3) Hiyo kusema uislam ameanza kipindi Cha Mtume Muhammad mnaosema ni nyinyi na sijui mmepata wapi maana Quran inasema manabii wote walikuwa waislam

Quran 2:132 -
Na Ibrahim akawausia wanawe, na pia Yaaqub: Enyi wanangu! Hakika Mwenyezi Mungu amekuteulieni Dini hii; basi msife ila nanyi mmekuwa Waislamu, wanyenyekevu.
Quran 2:133 -
Je! Mlikuwapo yalipo mfikia Yaaqub mauti, akawaambia wanawe: Mtamuabudu nani baada yangu? Wakasema: Tutamuabudu Mungu wako na Mungu wa baba zako, Ibrahim na Ismail na Is- hak, Mungu Mmoja tu, na sisi tunasilimu kwake.

Labda utoe ushahidi unasema Ibrahim, Ishmael, Isaka na Yakobo walikuwa dini Yao ukristo au Uyahudi au walikuwa wapagani Ili Quran ionekane imedanganya Kwa kusema kuwa walikuwa waislam

4) Yesu alikuwa anafanya ibada katika sinagogi na kipindi hicho ibada zilikuwa zinafuata Taurati na yeye Yesu alishasema hakuja kuitengua Taurati Taurati sio kitabu Cha ukristo na Wala sio kitabu Cha kabila pekee la kiyahudi Ili watumie wayahudi pekeyao hivyo ilikuwa ni ibada ya kiislam na ndio maana Yesu akisali alikuwa anasujudu na hata yule ibilisi alimwambia imeandikwa msujudie bwana Mungu wako

Mathayo 26:39
Akaendelea mbele kidogo, akaanguka kifulifuli, akaomba, akisema, Baba yangu, ikiwezekana, kikombe hiki kiniepuke; walakini si kama nitakavyo mimi, bali kama utakavyo wewe.

5) Kuhusu uokovu sijui kufa sijui kufufuka hayo maandiko yamewekwa na hao walioandika hizo Injili Kwa sababu Injili iliandikwa Kwa lengo la kuanzishwa ukristo na ndio maana Kuna marekenisho mengi yalifanywa

Na sijui kama unajua kuwa hizo Injili zimeandikwa miaka kati ya 30 Hadi 70 Baada ya Yesu kupaa

Injili ya Luka imeandikwa na mganga wa kienyeji tena alikuwa mpagani

Injili ya Mathayo na matendo inasemekana imeandikwa na Paulo

Injili ya Mariko aliyeandika hajulikani

Injili ya Yohana ndio kabisa hata kuhisi iliandikwa na nani imeshindikana hicho kitabu kiliokotwa Misri miaka 30 Baada ya Yesu kupaa na aliyeandika Hadi Leo hii hajulikani

Hizo Injili zumepewa majina ya wanafunzi wa Yesu Ili kukudanganyeni

Ingia website ya Cambridge university andika Gospel history utakutana na hizi habari

Ila Quran ilishasema Yesu hajusurubiwa
 
Ibada za Kiyahudi Zinafahana na Za Kiislamu kwa Asilimia 80
Kaka hivi mnadhani wote humu hawana exposure na dini ya kiyahudi ?

Ingawa ibada za Kiyahudi na Kiislamu zinafanana katika baadhi ya vipengele kutokana na asili yao ya imani ya Mungu mmoja na urithi wa kihistoria, ila kusema kwamba zinafanana kwa asilimia 80 ni UONGO MKUBWA .

Tofauti zao zipo wazi katika mambo yafuatayo

1. Mfumo wa Ibada:

Kiyahudi: Ibada zao nyingi zinahusisha Torati, Maagizo ya Musa, hekalu au sinagogi, na matendo maalum kama Shabbat.

Kiislamu: Ibada za Kiislamu zinahusisha nguzo tano (sala tano, saumu, zaka, Hija, na shahada).

2. Namna ya Kusali:

Wayahudi husoma maandiko wakiwa wamesimama au wamekaa, lakini hawana mfumo rasmi wa kupiga magoti kama Waislamu.

Waislamu husali kwa kupiga magoti, kurukuu, na kusujudu kwa mwelekeo wa Kaaba.

3. Mwelekeo wa Ibada:

Wayahudi husali wakielekea Yerusalemu.

Waislamu husali wakielekea Makka (Kaaba).

4. Nyakati za Sala:

Waislamu wana sala tano kwa siku.

Wayahudi hawana nyakati maalum za sala kama za Kiislamu, bali wana maombi ya asubuhi, mchana, na jioni.

5. Maandiko:

Kiyahudi: Torati (Vitabu vya Musa), Tanakh.

Kiislamu: Qur’an na Hadithi.

6. Sadaka na Zaka:

Wayahudi wana mifumo ya kutoa sadaka na zaka kulingana na sheria za Torati., Hawa wanatoa 10%

Zaka ni nguzo ya Kiislamu na ni jukumu la kila Mwislamu kutimiza., Hawa wanatoa 2.5%

Nijibu haya maswali kutokana na hoja yako

1. Je, ni vigezo gani maalum unatumia kuamua kuwa ibada za Kiyahudi na Kiislamu zinafanana kwa asilimia 80?

2. Unafikiri ni sahihi kulinganisha ibada kwa kutumia takwimu bila uthibitisho wa msingi wa maandiko?

3. Wayahudi hawasujudu kama Waislamu wanavyofanya – hii unahesabu kuwa ni tofauti au kufanana?

4. Waislamu wana nguzo tano za dini, je, Wayahudi wana mfumo sawa wa ibada?

5. Kwa nini Wayahudi husali kuelekea Yerusalemu, lakini Waislamu husali kuelekea Makka?

6. Shabbat ya Kiyahudi ni ya kila wiki, lakini Waislamu wana Ijumaa kama siku maalum – hii inahesabiwa kama kufanana?

7. Tofauti za maandiko ya Torati na Qur’an zinawezaje kufanikisha mfanano wa asilimia 80?

8. Unafikiria tofauti za matendo ya kiasili na tamaduni katika ibada zinaathiri vipi hoja yako?

9. Je, Wayahudi na Waislamu wanakubaliana juu ya ibada za kafara?

10. Ikiwa Wayahudi wanakataa waziwazi imani ya Mtume Muhammad, je, unaona wanaweza kuwa na ulinganifu mkubwa na Uislamu?
 
Sipo hapa kutetea Doctrine,Mimi nimtu huru ninaye challenge mafundisho mbalimbali,Mimi sifungwi na dhehebu au dini ,na hii kupenda ku challenge ndio kulinifanya nitoke kwenye uislamu maana walikuwa wanakosa majibu

Hoja zako ni nzuri sana na zimekaa kimafundisho haya ya kiyahudi

Hoja kuhusu Mfalme wa Babeli na Tiro zinaweza kuwa za kweli kihistoria, lakini unabii wa Isaya 14 na Ezekieli 28 mara nyingi huchukuliwa kuwa na maana mbili (dual prophecy),zinalenga wafalme wa wakati huo, lakini pia zinaashiria tabia za Shetani. Kulinganisha kiburi cha wafalme hawa na kuanguka kwa Shetani ni dhana inayojadiliwa sana, na msingi wake uko kwenye mifano ya kiroho.

Neno "Lucifer" lina maana ya "nyota ya asubuhi" na lilipewa Shetani baada ya kuanguka kwake kwa sababu ya kiburi (Ezekieli 28:17). Ingawa halihusiani moja kwa moja na mfalme wa Babeli au Tiro, linaelezea hali ya kiroho ya kujiinua juu ya Mungu.

Edeni katika Ezekieli 28:13 inaweza kueleweka kama sehemu halisi au mfano wa neema ya kiroho aliyokuwa nayo Shetani kabla ya anguko lake. Wakati wa Adamu na Hawa, Shetani alikuwa tayari ameanguka na akatumia nafasi hiyo kumshawishi mwanadamu.

Tafsiri ya Biblia inategemea muktadha wa maandiko yote, si sehemu moja tu. Mwelekeo wa maandiko unaonyesha kuwa tabia za kiburi na dhambi zilizoonyeshwa na wafalme wa Babeli na Tiro ni vivuli vya tabia ya Shetani.

Na kwa maelezo yako ndio unazidi kuzalisha maswali mengi kichwani mwangu ,

1. Kama Mfalme wa Babeli na Tiro walikuwa wanajulikana kwa dhambi zao, kwa nini maandiko katika Isaya 14 na Ezekieli 28 yanatumia lugha inayoonyesha zaidi ya wanadamu wa kawaida (k.m., "ulikuwa Edeni" na "uliangushwa kutoka mbinguni")?

2. Je, inawezekanaje "mfalme wa Tiro" aliyeishi duniani kuwa Edeni, wakati maandiko yanaonyesha Edeni kuwa sehemu maalum ya mwanzo wa mwanadamu?

3. Kama Ezekieli 28:13 inamaanisha utawala wa mwanadamu, kwa nini inasisitiza maelezo yasiyo ya kawaida kama vile "uliwekwa jiwe la thamani"? Je, hii haiashirii viwango vya kiroho?

4. Ikiwa Lucifer haimaanishi Shetani, kwa nini tafsiri za kale za Kiebrania, Kilatini, na hata Kikristo zinaeleza neno hilo kama kiburi cha Shetani kabla ya anguko lake?

5. Je, kwa kuwa kiburi na dhambi ya Shetani zilikuwepo kabla ya wanadamu, unaweza kueleza ulinganifu kati ya tabia za Shetani na zile za wafalme wa Babeli na Tiro bila kumhusisha Shetani moja kwa moja?
Vyote hivi pamoja na majibu ya maswali uliyouliza..
Soma Kwa umakini Bila kuweka Upande wowote Soma Na uthibitisho wa Kimaandilo bila Kujiingiza kwenye Doctrine ypyote utanielewa nachosema..

Nimepita na Kulelewa na Kila Dini Najua ninachokisema
 
Wala usirudi katika uislam wewe endelea kuwa mgalatia Ili uende Jahanamu

Najibu maswali yako kama ifuatavyo

1) Ufalume wa mbinguni au uzima wa milele
Yohana 17:3
Na uzima wa milele ndio huu, Wakujue wewe, Mungu wa pekee wa kweli, na Yesu Kristo uliyemtuma.

Yesu anasema Ili mtu aende peponi lazima ukubali kuwa Mungu ni mmoja na Yesu ametumwa na huyo Mungu mmoja
Wewe siku ukiliamini hili andiko utakuwa Muislam maana waislam ndivyo tunavyo amini

2) Mungu hana mtoto kwanza Mungu sio Mwanamume Wala sio mwanamke kike na kiume hizo ni sifa za viumbe vilivyoumbwa na Mungu hivyo basi Mungu ndio ameumba kiume na kike

Lakini pia Mungu ana majina mengi kama nyinyi mmeamua kumuita Mungu baba hilo halina shida lakini je! Kwanini nyinyi mnajitoa na kusema kuwa Yesu ni mtoto wa Mungu hilo halikubaliki kama ungesema wewe na Yesu ni watoto wa Mungu tungejua ndio staili yenu ya kumtukuza Mungu
Na Kwa mujibu wa maandiko ipo sehemu Yesu amesema binadamu wote pamoja na yeye ni watoto wa Mungu Kwa Nini nyinyi mlazimishe kuwa Yesu ndio mtoto wa Mungu?

Yohana 20:17
Yesu akamwambia. Usinishike; kwa maana sijapaa kwenda kwa Baba. Lakini enenda kwa ndugu zangu ukawaambie, Ninapaa kwenda kwa Baba yangu naye ni Baba yenu, kwa Mungu wangu naye ni Mungu wenu.

3) Hiyo kusema uislam ameanza kipindi Cha Mtume Muhammad mnaosema ni nyinyi na sijui mmepata wapi maana Quran inasema manabii wote walikuwa waislam

Quran 2:132 -
Na Ibrahim akawausia wanawe, na pia Yaaqub: Enyi wanangu! Hakika Mwenyezi Mungu amekuteulieni Dini hii; basi msife ila nanyi mmekuwa Waislamu, wanyenyekevu.
Quran 2:133 -
Je! Mlikuwapo yalipo mfikia Yaaqub mauti, akawaambia wanawe: Mtamuabudu nani baada yangu? Wakasema: Tutamuabudu Mungu wako na Mungu wa baba zako, Ibrahim na Ismail na Is- hak, Mungu Mmoja tu, na sisi tunasilimu kwake.

Labda utoe ushahidi unasema Ibrahim, Ishmael, Isaka na Yakobo walikuwa dini Yao ukristo au Uyahudi au walikuwa wapagani Ili Quran ionekane imedanganya Kwa kusema kuwa walikuwa waislam

4) Yesu alikuwa anafanya ibada katika sinagogi na kipindi hicho ibada zilikuwa zinafuata Taurati na yeye Yesu alishasema hakuja kuitengua Taurati Taurati sio kitabu Cha ukristo na Wala sio kitabu Cha kabila pekee la kiyahudi Ili watumie wayahudi pekeyao hivyo ilikuwa ni ibada ya kiislam na ndio maana Yesu akisali alikuwa anasujudu na hata yule ibilisi alimwambia imeandikwa msujudie bwana Mungu wako

Mathayo 26:39
Akaendelea mbele kidogo, akaanguka kifulifuli, akaomba, akisema, Baba yangu, ikiwezekana, kikombe hiki kiniepuke; walakini si kama nitakavyo mimi, bali kama utakavyo wewe.

5) Kuhusu uokovu sijui kufa sijui kufufuka hayo maandiko yamewekwa na hao walioandika hizo Injili Kwa sababu Injili iliandikwa Kwa lengo la kuanzishwa ukristo na ndio maana Kuna marekenisho mengi yalifanywa

Na sijui kama unajua kuwa hizo Injili zimeandikwa miaka kati ya 30 Hadi 70 Baada ya Yesu kupaa

Injili ya Luka imeandikwa na mganga wa kienyeji tena alikuwa mpagani

Injili ya Mathayo na matendo inasemekana imeandikwa na Paulo

Injili ya Mariko aliyeandika hajulikani

Injili ya Yohana ndio kabisa hata kuhisi iliandikwa na nani imeshindikana hicho kitabu kiliokotwa Misri miaka 30 Baada ya Yesu kupaa na aliyeandika Hadi Leo hii hajulikani

Hizo Injili zumepewa majina ya wanafunzi wa Yesu Ili kukudanganyeni

Ingia website ya Cambridge university andika Gospel history utakutana na hizi habari

Ila Quran ilishasema Yesu hajusurubiwa
Ndugu Mimi huko siwezi kurudi maana hoja zangu umezijibu juu juu tu ,

Kwanza ndio unazidi kuzalisha maswali mengi zaidi ,

Kupanua Hoja na Kukanusha

Nitapanga hoja na kuzikanusha moja baada ya nyingine, kisha nitatengeneza maswali ya kumchallange kutokana na mada hii.

Hoja 1: Uzima wa milele unapatikana kwa kumtambua Mungu mmoja na Yesu kama mjumbe wake (Yohana 17:3).

Yohana 17:3 haisemi kuwa Yesu ni mjumbe tu wa Mungu kama inavyodaiwa. Yesu alitumia neno "kujua" kwa maana ya uhusiano wa karibu na wa kiroho kati ya mwanadamu na Mungu kupitia kwake. Hii ni tofauti kabisa na maana inayotolewa katika Uislamu. Zaidi ya hayo, Yohana 14:6 Yesu alisema, "Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi." Hii inaonyesha nafasi ya kipekee ya Yesu kama njia pekee ya uzima wa milele.

Hoja 2: Mungu hana mtoto, na watu wote ni watoto wa Mungu.

Yesu alijitaja kama Mwana wa Mungu kwa maana ya kipekee (Yohana 10:30), akithibitisha uhusiano wake wa kiungu na Baba. Lugha ya Biblia kuhusu "Mwana wa Mungu" haimaanishi uzazi wa kibinadamu, bali inaonyesha nafasi ya kipekee ya Yesu katika utatu mtakatifu. Wakati Yohana 20:17 inataja "Baba yangu na Baba yenu," Yesu hakumaanisha usawa baina yake na wanadamu, bali alitofautisha uhusiano wake wa kiungu.

Hoja 3: Uislamu ulianza na manabii wote wa zamani.

Quran inadai kuwa manabii wote walikuwa Waislamu, lakini historia ya Biblia inaonyesha kwamba Wayahudi waliabudu kwa mujibu wa Agano la Kale, si kwa kufuata Qur’an. Hakuna ushahidi wa kihistoria au wa maandiko unaoonyesha kuwa Ibrahim, Isaka, au Yakobo walikuwa Waislamu kwa maana inayotolewa na Uislamu. Uislamu kama dini ya Muhammad ulianza karne ya 7 BK, wakati Uyahudi na Ukristo vimekuwepo karne nyingi kabla yake.

Hoja 4: Yesu alisali kwa kusujudu na kufuata Taurati.

Yesu hakufundisha sheria za Taurati pekee bali alikamilisha maana yake (Mathayo 5:17). Kusujudu kwake katika Mathayo 26:39 ni ishara ya unyenyekevu, si ibada ya Kiislamu. Yesu alifundisha kwamba uhusiano na Mungu unapatikana kupitia imani kwake, si kufuata sheria ya Taurati tu (Yohana 6:29).

Hoja 5: Injili zimepotoshwa na hazina uthibitisho.

Kuna ushahidi wa kihistoria kwamba Injili ziliandikwa na watu waliokuwa karibu na Yesu au walioshuhudia matukio yake. Ingawa ziliandikwa kati ya miaka 30-70 baada ya Yesu, maandishi hayo yaliendelezwa kwa mdomo kabla ya kuandikwa. Ushahidi wa maandiko ya kale, kama vile manuskripti za Dead Sea Scrolls, unaonyesha uthabiti wa maandiko ya Biblia. Tuhuma dhidi ya Injili hazina uthibitisho wa kitaalamu bali ni maoni yasiyo na msingi.

Nina maswali kwako

1. Yohana 17:3 inasema kumjua Yesu ni sehemu ya uzima wa milele, je, hili linafanana na imani ya Kiislamu ambayo inamwona Yesu kama nabii wa kawaida?

2. Ikiwa manabii wote walikuwa Waislamu, kwa nini hakuna ushahidi wa kihistoria wa maandiko yao yanayosema hivyo kabla ya Qur’an?

3. Je, unakubaliana kuwa Ibrahim, Isaka, na Yakobo walikuwa Wayahudi kwa mujibu wa Biblia, si Waislamu?

4. Mathayo 26:39 inaonyesha Yesu akisali kwa Baba yake. Kwa nini unadhani Yesu alifundisha Mungu kama Baba wa pekee wa wanafunzi wake?

5. Umewezaje kuhitimisha kuwa Injili zimepotoshwa wakati ushahidi wa kihistoria wa maandiko ya kale unaonyesha uthabiti wake?

6. Yesu alisema alikuja kukamilisha Taurati (Mathayo 5:17). Kwa nini unadai alikuwa mfuasi wa Taurati bila mabadiliko?

7. Ikiwa Yesu alisujudu kwa Mungu, je, hili linathibitisha kuwa alikuwa Muislamu au ni ishara ya unyenyekevu wake kama mwana wa Mungu?

8. Kwa nini Qur’an inadai Yesu hajisulubiwa, wakati ushahidi wa kihistoria wa Kirumi unathibitisha kifo chake msalabani?

9. Je, unakubaliana kwamba imani ya Kikristo kuhusu Yesu inategemea maandiko ya kale yaliyoandikwa karne nyingi kabla ya Uislamu?

10. Ikiwa Injili ziliandikwa na watu waliomshuhudia Yesu, kwa nini unakubali Qur’an iliyoandikwa karne kadhaa baadaye bila mashahidi wa moja kwa moja?
 
Ngoja Mimi nijibu

1. Shetani aliasi kabla au baada ya binadamu kuumbwa?

Majibu:
Maandiko hayaonyeshi waziwazi kama Shetani aliasi kabla au baada ya binadamu kuumbwa. Hata hivyo, tukirejelea Mwanzo 3, tunamwona Shetani tayari akiwa ameanguka kwa sababu alijaribu kumdanganya Hawa. Hii inamaanisha uasi wake ulitokea kabla ya tukio hilo.

Katika Ufunuo 12:7-9, tunaona vita mbinguni ambavyo vilisababisha kuangushwa kwa Shetani na malaika zake. Tukio hili linaweza kufasiriwa kuwa lilitokea kabla ya uumbaji wa binadamu, lakini baadhi ya wanatheolojia wanaamini linaweza pia kufungamana na ukamilifu wa kazi ya Kristo duniani.
Unazidi kukuza maswali ila niache kuyauliza maana Mengine hutaweza kuyajibu..

Tuseme Aliasi Kabla ya Kuumbwa kwa Ulimwengu Ile Ole ya Ufunuo Alikuwa anaambiwa nani?

Tuseme aliasi baada ya Kuumbwa kwa Ulimwengu Kwanini Alipelekwa Edeni? Na Mbona akiwa Edeni hakuwa na malaika wake?

2. Binadamu aliumbwa mbinguni akawekwa ardhini au aliumbwa ardhini akawekwa Edeni?

Majibu:
Mwanzo 2:7 inasema, “Bwana Mungu akamfanya mtu kwa mavumbi ya ardhi, akampulizia pumzi ya uhai; mtu akawa nafsi hai.” Hii inaonyesha kuwa binadamu aliumbwa ardhini. Baada ya kuumbwa, Mwanzo 2:8 inasema Mungu alipanda bustani huko Edeni na kumweka binadamu ndani yake. Edeni haikuelezwa kama mbinguni, bali kama mahali maalum hapa duniani.
Katika andiko Lako hata Lile la 1:26-29 halionyeshi Mungu aliumba mtu akiwa wapi..

Alimuumba Mbinguni akamuweka Kwenye Bustanj au alimuumba Ardhinj akamuweka Kwenye Bustani ambayo Inawezekana Iko mbinguni..

3. Shetani alikuwa na malaika wake? Je, alikuwa na nguvu sawa na Mungu?

Majibu:
Ndiyo, Shetani alikuwa na malaika wake. Ufunuo 12:4 inasema "Mkia wake wakokota theluthi ya nyota za mbinguni, na kuzitupa katika nchi." Nyota hizi zinatafsiriwa na wanatheolojia wengi kuwa ni malaika walioasi pamoja naye.
ufunuo 12:4 imasema Mkia wake ulikokota Nyota na Kuzitupa..
ila ukienda mbele Inasema kuhusu Vita Kati ya Mikael na Malaika wake na Shetani na malaika wake....
Sasa Waliokokotwa na Kutupwa Kuna wengine walibaki??

Hata hivyo, Shetani hakuwa na nguvu sawa na Mungu. Shetani ni kiumbe aliyeumbwa (angalia Ezekieli 28:12-15). Mungu ni Mwenyezi na hana usawa wake (Isaya 45:5). Shetani alijaribu kujiinua juu ya Mungu (Isaya 14:12-15), lakini akashindwa.
mimi Nakuomba Usitumie Ezekiel na Isaya kama Refference ya Shetani haipo Hivyo.Mkuu..Hiyo Ni Dogma Ni Doctrine ambayo haina Uhalisia wala Ukweli
4. Baada ya Adamu kufukuzwa Edeni, alipelekwa wapi?

Majibu:
Mwanzo 3:23-24 inasema Adamu alifukuzwa kutoka bustani ya Edeni na kuishi mahali pengine duniani. Haielezwi hasa aliishi wapi, lakini maandiko yanaonyesha aliendelea kuishi duniani, akifanya kazi ya kulima ardhi ambayo ililaaniwa (Mwanzo 3:17-19).
vizuri
5. Shetani alifanya kosa gani akafukuzwa mbinguni?

Majibu:
Shetani alikosea kwa kuonyesha kiburi na kutaka kuwa kama Mungu. Ezekieli 28:17 inasema, “Moyo wako uliinuka kwa sababu ya uzuri wako, ukaharibu hekima yako kwa sababu ya fahari yako.” Isaya 14:12-14 inaeleza zaidi jinsi Shetani alivyotamani kujiinua juu ya Mungu. Kosa hili la kiburi na uasi ndilo lililomfanya afukuzwe kutoka mbinguni.
Please Usitumie Isaya na Ezekiel Kujibu hoja ya Uasi wa Shetanj mimi Kama mwanatheolojia Nimekataa na Nimekuonuesha Ushahidi wa Kina na Kihistoria kuwa Hayo mafungu ama aya Hazihusiani na Shetani..

Maswali uliyojibu Ni mawili tu ni la kwanza na La 4 Mengine Hujajibu ila Umeweka siasa
 
Mimi Sina chuki na dini yoyote , umeona natoa lugha Kali na mihemko?

Jenga hoja tu utaeleweka, kwanza Sio kweli Lazima Sinagogi lielekezwe Mashariki,

Ni kweli Wayahudi wa kawaida huomba kuelekea Yerusalemu, kama inavyoonyeshwa katika Danieli 6:10, lakini tofauti ni kwamba Wayahudi hawajafanikisha utaratibu wa kudai kwamba kila sinagogi duniani lazima lionyeshe mwelekeo wa Mashariki ya Kati. Mwelekeo huu mara nyingi ni wa kiroho na si wa kimuundo.

Tofauti na misikiti, ambapo mihrab huonyesha mwelekeo wa Makka, hakuna sheria kali inayosema kuwa sinagogi lazima zielekezwe Yerusalemu. Uelekeo ni mazoea yanayopendelewa, lakini si lazima.

Wayahudi huamini maombi yao yanaweza kufika kwa Mungu popote bila kujali uelekeo. Hii inatofautiana na Uislamu, ambapo mwelekeo wa Kibla ni sehemu muhimu ya ibada.

Shida yako moja unapaniki ,haya jibu maswali yangu haya 👇👇👇

1. Ikiwa kila sinagogi limeelekezwa Middle East, je, unaweza kutaja ushahidi wa kihistoria au usanifu wa sinagogi ulimwenguni unaothibitisha hili?

2. Kwa nini maombi ya Wayahudi kama ilivyoonyeshwa kwa Danieli 6:10 yanaweza kufanywa popote, wakati katika Uislamu mwelekeo wa Kibla ni wa lazima kwa sala?

3. Je, uelekeo wa misikiti kuelekea Makka unahusianaje na maana ya kiroho ya ibada, ukilinganisha na Wayahudi ambao wanasisitiza ibada ya moyo bila kuzingatia sana mwelekeo?

4. Kwa nini sinagogi nyingi za kisasa hazifuati kabisa kanuni ya kuelekea Yerusalemu, ikiwa ni muhimu sawa na Kibla kwa Waislamu?

5. Kwa kuwa ibada za Wayahudi zilifanyika katika hekalu la Yerusalemu zamani, je, huoni tofauti kati ya hekalu (ambalo lilikuwa mahali maalum) na sinagogi za sasa ambazo zinaweza kujengwa popote?
Mambo ya dini sio fani yangu na sio sehemu ya migogoro yangu; bora nikatafute ugomvi na ‘bi tozo’ na machawa wake.

Hayo mambo ya dini inabidi ukajifunze mwenyewe, siku nikiwa mood nitakutwanga tena kwa sababu hujui.

Msingi wa Jews kuelekeza Synagogues zao Middle East ni kufuata ‘Solomon Temple’ unajua historia yake, hadi kuwa sehemu tukufu kwao. Hata baada ya kuvunjwa na waliojaribu kwenda kuijenga tena asili yao ni watu wa wapi

Wewe dini unaijua kwa biblia, lakini huijui kwa historia wala biblical archeology.

Uwa sipendi hii mijadala lakini nakerekwa
kuona mnatengeneza matabaka ya kujigawa bila ya uelewa mpana wa dini zaidi ya akili mnazolishwa na vitabu vyenu.

Hata misingi ya vitabu vyenyewe hamvijul
na mauaji yaliyo husika kufuta version zingine zozote ambazo tofauti na za clerics walizochagua (salaleh) nina uhakika hayo mambo uyajui; sikia tu unyama wake.

👋 acheni kuchukiana kwa mambo ambayo msiyoyaelewa kwa kina.

Si muamini tu kila mtu anachotaka kwani lazima mchukiane.
 
Unasema mambo ya dini huyajui ,Bado Tena unayaongelea ,ili mradi tu yaani
 
Ishu ni kuwa ukiristu umekuwepo miaka 600 kabla ya Islam. Ila Hawa jamaa wanakuambia uislam ulianza tangu kuumbwa kwa ulimwengu
Uislam umeanzishwa na Muhammad baada ya kupokea alichodai kuwa ni Qur'an. Maana ya uislam ni 'kujisalimisha' au 'kusilimu'. Kwa mujibu wa Uislam ni kuwa Mungu yuko mbali na mwanadamu hivyo maneno yake akapitisha kama 'wahyi' kwa Muhammad. Ulimwengu uliumbwa lini na Muhammad alizaliwa lini?
 
Kaka hivi mnadhani wote humu hawana exposure na dini ya kiyahudi ?

Ingawa ibada za Kiyahudi na Kiislamu zinafanana katika baadhi ya vipengele kutokana na asili yao ya imani ya Mungu mmoja na urithi wa kihistoria, ila kusema kwamba zinafanana kwa asilimia 80 ni UONGO MKUBWA .

Tofauti zao zipo wazi katika mambo yafuatayo

1. Mfumo wa Ibada:

Kiyahudi: Ibada zao nyingi zinahusisha Torati, Maagizo ya Musa, hekalu au sinagogi, na matendo maalum kama Shabbat.

Kiislamu: Ibada za Kiislamu zinahusisha nguzo tano (sala tano, saumu, zaka, Hija, na shahada).

2. Namna ya Kusali:

Wayahudi husoma maandiko wakiwa wamesimama au wamekaa, lakini hawana mfumo rasmi wa kupiga magoti kama Waislamu.

Waislamu husali kwa kupiga magoti, kurukuu, na kusujudu kwa mwelekeo wa Kaaba.

3. Mwelekeo wa Ibada:

Wayahudi husali wakielekea Yerusalemu.

Waislamu husali wakielekea Makka (Kaaba).

4. Nyakati za Sala:

Waislamu wana sala tano kwa siku.

Wayahudi hawana nyakati maalum za sala kama za Kiislamu, bali wana maombi ya asubuhi, mchana, na jioni.

5. Maandiko:

Kiyahudi: Torati (Vitabu vya Musa), Tanakh.

Kiislamu: Qur’an na Hadithi.

6. Sadaka na Zaka:

Wayahudi wana mifumo ya kutoa sadaka na zaka kulingana na sheria za Torati., Hawa wanatoa 10%

Zaka ni nguzo ya Kiislamu na ni jukumu la kila Mwislamu kutimiza., Hawa wanatoa 2.5%

Nijibu haya maswali kutokana na hoja yako

1. Je, ni vigezo gani maalum unatumia kuamua kuwa ibada za Kiyahudi na Kiislamu zinafanana kwa asilimia 80?

2. Unafikiri ni sahihi kulinganisha ibada kwa kutumia takwimu bila uthibitisho wa msingi wa maandiko?

3. Wayahudi hawasujudu kama Waislamu wanavyofanya – hii unahesabu kuwa ni tofauti au kufanana?

4. Waislamu wana nguzo tano za dini, je, Wayahudi wana mfumo sawa wa ibada?

5. Kwa nini Wayahudi husali kuelekea Yerusalemu, lakini Waislamu husali kuelekea Makka?

6. Shabbat ya Kiyahudi ni ya kila wiki, lakini Waislamu wana Ijumaa kama siku maalum – hii inahesabiwa kama kufanana?

7. Tofauti za maandiko ya Torati na Qur’an zinawezaje kufanikisha mfanano wa asilimia 80?

8. Unafikiria tofauti za matendo ya kiasili na tamaduni katika ibada zinaathiri vipi hoja yako?

9. Je, Wayahudi na Waislamu wanakubaliana juu ya ibada za kafara?

10. Ikiwa Wayahudi wanakataa waziwazi imani ya Mtume Muhammad, je, unaona wanaweza kuwa na ulinganifu mkubwa na Uislamu?
Samahani Ulichokitana sio Ibada ya sala ulichotaja hapo Ni Dini Kwa Ujumla..Sio Kila Mda tubishe kwa Kuyumia Neno Uongo unaweza ukabisha kwa kusema sina exposure au sijui

Ni kweli kwamba Kidini wanatofautina baadhi ya Mifumo ..
Pole sana mkuu Nasikitika Kwamba sina jibu jingine zaidi ya hilo.. linaweza kuwa gumu kwako lakini kwa bahati mbaya ndo ukweli wenyewe....

HIVI NI BAADHI YA VITU AMBAVYO HUFANYIKA KWA WAISLAMU LAKINI HUFANYIKA /VILIFANYIKA KATIKA JUDAISM

  • Hadithi/Sunna (kutunza hadithi kwa ajili ya kutafsiri Quran na maelezo Ya Mtume kama sunna)Hii ilifanywa na wayahudi mpaka sasa kwa kutumia Vyanzo vingine tofauti na Biblia kama Talmud,Rabbinic Narrative, Aggadah na Halakhah hizo ni sawa na sunna kwa wayahudi kama wanavyoita Waislamu na watu husoma pia ili kujua sunna hizo...

  • Adhana kwa waislamu ni sawa na shofar katika Judaism japo shofar hutumia Sauti ya Pembe ikipulizwa na Waislamu hutumua sauti Ya kughani Maneno Ya shahada na muito kwa waislamu kwa swala...na pia Kuna Ghani tunaita Shema yisrael adonai..
Hata maneno ya Adhana Hizi Huwa Yanafanana maana Yake Kiswahili Kwa Wayahudi..Nitakutumia Na video hapa chini..

שְׁמַע יִשְׂרָאֵל ה' אֱלֹהֵינוּ ה' אֶחָד

Shema Yisrael, Adonai Eloheinu, Adonai Echad.

kiswahili

Sikiza, Ee Israeli; Bwana, Mungu wetu, Bwana ndiye mmoja.
(Inatoka kwenye Kumbukumbu la Torati 6:4)

Kwa waislamu nafikiri Maana zake zinajulikana ni Hilo.jil9 neno Lililoandikwa hapo Juu Kuwa Mungu Ni mmoja..

Mfano wa shemai yisrael kwa matamshi ziko Video 2 za adhana au Shema Yisrael

Shemai hii akiitamka Mwanajeshi kabla ya Kuingia Vitani..

Hii Hapa Ikitamkwa Karibia na Msikiti wa Al Aqsa..

  • Wudhu-Kabla ya kuswali Waislamu hufanya huchukua Wudhu (ablution) ili Kujitakasa lakini hilo jambo pia hufanyika kwa Judaism kwa hatua zinazofanana na huitwa Netilat Yadayim

  • Kuoga janaba - Waislam wanapotokwa na manii au mtu mpya anaposilimu au mwanamke anapotoka hedhi huoga ili kujitakasa na Huita koga hilo kama "Kuoga janaba" au ghusl na njia ya kuoga hupatikana katika Sharia za kiislamu yaani Fiqhi sasa chakushangaza ni kwamba hatua za kuoga huko Jinsi ya kuoga na nani anapaswa kuoga Zote hufanana na "Tevilah" kogo la janaba kwa Kiyahudi sema Kwa wayahudi mara Nyingi hifanywa katika sehemu maalumu iitwayo Mikveh au kwa Wakristo wanaita Birika .. Na hiyo ipo kwenye sheria za utakazo za kiyahudi yaani Niddah

  • Swala Wayahudi husali mara Tatu kwa siku na cha kufurahisha ni kwamba wana hatua za kuswali zinazofanana kwa 88% sawa kabisa na Swala zinazofanywa na Waislamu Kusimama,Kuinama kusujudu na hata kutaja mungu mkubwa ..kabla ya kuanza kuswali wayahudi husema "Shema Yisrael Adonai Eloheinu Adonai Echad" (Sikia O Israel: Bwana Mungu wetu, Bwana ni Mmoja). Na huwa kama kitangulizi pia kabla ya swala.. Vivyo hivyo na kwa waislam kitangulizi cha swala huwa na maneno hayo hayo ambayo huitwa Iqaama baada ya Allah akbar hufuata Shahada ambayo maneno hayo ni sawa kabisa na hayo ya wayahudi..

  • Swala za wayahudi huwa ni Tatu
    • Shacharit (Hufanyika alfajiri kabla ya jua kutoka)
    • Mincha (husaliwa katikati ya siku Lakini jua likiwa limetoka utosini kuelekea magharibi)
    • Ma'ariv Au Magharib (Husaliwa jua likianza kuzama na giza likianza kuingia.....
    • sasa hivyo vyote ni sawa kama wanavyosali Dhehebu la kiislamu la shiha mara tatu kwa siku na Muongozo huo wa shala japo kwa Sunni husali mara tano Yaani Fajir,Adhuhuri,Alasiri,Magharib na Insha...japo Kwenye Quran Imeandikwa Swala Ziswaliwa kwa Nyakati Tatu..
  • Kuhusu vyakula Huku wana Kosher huku wana halal Na Ndo maana Narudia Tena Uislamu ni Modified and updated Version ya Christian na Judaism..
Kama utakuwa una jambo ambalo ni Jipya limeanza kwenye uislam niko Tayri kujifunza pia..Ila Mambo Yote Ya Uislamu yana. CHANZO KWENYE UYAHUDI

Ila kwa swala angalia Hapa Huyu Mtu anavyoswali mpaka mwishoni anavyotoa Salamu Ni process zile zile za Sala ya Kiislamu sema Kuna Baadhi ya Modofication tu waislmu wamefanya..

Nasubiria Challenge but Nikisemacho ni Kweli
 
Fungu lako Ni hili hapa..

Ufunuo wa Yohana 12:7-10, 12
7 Kulikuwa na vita mbinguni; Mikaeli na malaika zake wakapigana na yule joka, yule joka naye akapigana nao pamoja na malaika zake;

8 nao hawakushinda, wala mahali pao hapakuonekana tena mbinguni.

9 Yule joka akatupwa, yule mkubwa, nyoka wa zamani, aitwaye Ibilisi na Shetani, audanganyaye ulimwengu wote; akatupwa hata nchi, na malaika zake wakatupwa pamoja naye.

10 Nikasikia sauti kuu mbinguni, ikisema, Sasa kumekuwa wokovu, na nguvu, na ufalme wa Mungu wetu, na mamlaka ya Kristo wake; kwa maana ametupwa chini mshitaki wa ndugu zetu, yeye awashitakiye mbele za Mungu wetu, mchana na usiku."

12 Kwa hiyo shangilieni, enyi mbingu, nanyi mkaao humo. Ole wa nchi na bahari! Kwa maana yule Ibilisi ameshuka kwenu mwenye ghadhabu nyingi, akijua ya kuwa ana wakati mchache tu.

Andiko Lako nalijua sasa nataka Unijibu maswali yangu machache kabla Sijakujibu Mimi..

  1. Shetani aliasi Baada ya Binadamu Kuumbwa au kabla ya Binadamu Kuumbwa?
  2. Binadamu aliumbwa mbinguni akawekwa Ardhini chini au aliumbwa ardhini akawekwa Kwenye edeni ambayo iko mahali?
  3. Shetani alikuwa na Malaika wake? Maana alikuwa na Nguvu sawa na Mungu?
  4. Baada ya Adamu kufukuzwa Edeni alipelekwa Wapi
  5. Na Shetani alifanya kosa gani akafukuzwa Mbinguni

Lengo la kukuonesha fungu hilo ni kujibu ile hoja yako ya kuwa shetani hayuko duniani. Na uzuri umeweka hapa mafungu haya. Fungu la 12 linathibitisha pasipo na shaka mahali shetani alipo kwa sasa.

Naomba unijibu kama mpaka hapa tuko na uelewa wa pamoja kuhusu mahali alipo shetani.
 
Nijibu haya maswali kutokana na hoja yako

1. Je, ni vigezo gani maalum unatumia kuamua kuwa ibada za Kiyahudi na Kiislamu zinafanana kwa asilimia 80?
Vyote soma Post iliyopita hapo Post no 275 Nimekupostia
2. Unafikiri ni sahihi kulinganisha ibada kwa kutumia takwimu bila uthibitisho wa msingi wa maandiko?
SOma #275
3. Wayahudi hawasujudu kama Waislamu wanavyofanya – hii unahesabu kuwa ni tofauti au kufanana?
kweli Una thubutu kusema wayahudi hawasujudu?
kweli Huijui dini Ya Kiyahudi Vizuri
4. Waislamu wana nguzo tano za dini, je, Wayahudi wana mfumo sawa wa ibada?
hizo waislamu wanazoziita Nguzo wayahudi wanazifata zote..
Kasoro shahada ya Mohamadi Rasull
5. Kwa nini Wayahudi husali kuelekea Yerusalemu, lakini Waislamu husali kuelekea Makka?
Walibadilishiwa Ila Zaman walikuwa wakiswali kuelekea Msikiti mtakatifu na Ipo Kimaandiko walikuwa Na Qibra Ya Yerusalem..

Al Baqara aya 142..

"WAPUMBAVU miongoni mwa watu watasema: Nini kilicho wageuza kutoka kibla chao walicho kuwa wakikielekea? Sema: Mashariki na Magharibi ni ya Mwenyezi Mungu; Yeye humwongoa amtakaye kwenye njia iliyo nyooka."

6. Shabbat ya Kiyahudi ni ya kila wiki, lakini Waislamu wana Ijumaa kama siku maalum – hii inahesabiwa kama kufanana?
Hapana!
Shabati ni waislamu wanayo na aunaweza ukaisoma Vizuri pia na wale walio ihalifu walipewa nini..
Ila waislamu wakaamrishwa Siku yao Mpya..

Suratul Jumua aya ya 9

"Enyi mlio amini! Ikiadhiniwa Sala siku ya Ijumaa, nendeni upesi kwenye dhikri ya Mwenyezi Mungu, na wacheni biashara. Hayo ni bora kwenu, lau kama mnajua."

7. Tofauti za maandiko ya Torati na Qur’an zinawezaje kufanikisha mfanano wa asilimia 80?
Kuna tifauti kubwa kati ya Dini na maandiko na Ibada..

8. Unafikiria tofauti za matendo ya kiasili na tamaduni katika ibada zinaathiri vipi hoja yako?

Hazina Athari
9. Je, Wayahudi na Waislamu wanakubaliana juu ya ibada za kafara?
Ndyo wanakubaliana Wote kuhusu Ibada za Kafara na Wote Wana Sherehe za Kuchinja

10. Ikiwa Wayahudi wanakataa waziwazi imani ya Mtume Muhammad, je, unaona wanaweza kuwa na ulinganifu mkubwa na Uislamu?
Kukataa Na Kuwa na Mfanano ni Vitu viwili tofauti
 
Samahani Ulichokitana sio Ibada ya sala ulichotaja hapo Ni Dini Kwa Ujumla..Sio Kila Mda tubishe kwa Kuyumia Neno Uongo unaweza ukabisha kwa kusema sina exposure au sijui

Ni kweli kwamba Kidini wanatofautina baadhi ya Mifumo ..
Pole sana mkuu Nasikitika Kwamba sina jibu jingine zaidi ya hilo.. linaweza kuwa gumu kwako lakini kwa bahati mbaya ndo ukweli wenyewe....

HIVI NI BAADHI YA VITU AMBAVYO HUFANYIKA KWA WAISLAMU LAKINI HUFANYIKA /VILIFANYIKA KATIKA JUDAISM

  • Hadithi/Sunna (kutunza hadithi kwa ajili ya kutafsiri Quran na maelezo Ya Mtume kama sunna)Hii ilifanywa na wayahudi mpaka sasa kwa kutumia Vyanzo vingine tofauti na Biblia kama Talmud,Rabbinic Narrative, Aggadah na Halakhah hizo ni sawa na sunna kwa wayahudi kama wanavyoita Waislamu na watu husoma pia ili kujua sunna hizo...

  • Adhana kwa waislamu ni sawa na shofar katika Judaism japo shofar hutumia Sauti ya Pembe ikipulizwa na Waislamu hutumua sauti Ya kughani Maneno Ya shahada na muito kwa waislamu kwa swala...na pia Kuna Ghani tunaita Shema yisrael adonai..
Hata maneno ya Adhana Hizi Huwa Yanafanana maana Yake Kiswahili Kwa Wayahudi..Nitakutumia Na video hapa chini..

שְׁמַע יִשְׂרָאֵל ה' אֱלֹהֵינוּ ה' אֶחָד

Shema Yisrael, Adonai Eloheinu, Adonai Echad.

kiswahili

Sikiza, Ee Israeli; Bwana, Mungu wetu, Bwana ndiye mmoja.
(Inatoka kwenye Kumbukumbu la Torati 6:4)

Kwa waislamu nafikiri Maana zake zinajulikana ni Hilo.jil9 neno Lililoandikwa hapo Juu Kuwa Mungu Ni mmoja..

Mfano wa shemai yisrael kwa matamshi ziko Video 2 za adhana au Shema Yisrael

Shemai hii akiitamka Mwanajeshi kabla ya Kuingia Vitani..
View attachment 3173668

Hii Hapa Ikitamkwa Karibia na Msikiti wa Al Aqsa..

View attachment 3173667

  • Wudhu-Kabla ya kuswali Waislamu hufanya huchukua Wudhu (ablution) ili Kujitakasa lakini hilo jambo pia hufanyika kwa Judaism kwa hatua zinazofanana na huitwa Netilat Yadayim

  • Kuoga janaba - Waislam wanapotokwa na manii au mtu mpya anaposilimu au mwanamke anapotoka hedhi huoga ili kujitakasa na Huita koga hilo kama "Kuoga janaba" au ghusl na njia ya kuoga hupatikana katika Sharia za kiislamu yaani Fiqhi sasa chakushangaza ni kwamba hatua za kuoga huko Jinsi ya kuoga na nani anapaswa kuoga Zote hufanana na "Tevilah" kogo la janaba kwa Kiyahudi sema Kwa wayahudi mara Nyingi hifanywa katika sehemu maalumu iitwayo Mikveh au kwa Wakristo wanaita Birika .. Na hiyo ipo kwenye sheria za utakazo za kiyahudi yaani Niddah

  • Swala Wayahudi husali mara Tatu kwa siku na cha kufurahisha ni kwamba wana hatua za kuswali zinazofanana kwa 88% sawa kabisa na Swala zinazofanywa na Waislamu Kusimama,Kuinama kusujudu na hata kutaja mungu mkubwa ..kabla ya kuanza kuswali wayahudi husema "Shema Yisrael Adonai Eloheinu Adonai Echad" (Sikia O Israel: Bwana Mungu wetu, Bwana ni Mmoja). Na huwa kama kitangulizi pia kabla ya swala.. Vivyo hivyo na kwa waislam kitangulizi cha swala huwa na maneno hayo hayo ambayo huitwa Iqaama baada ya Allah akbar hufuata Shahada ambayo maneno hayo ni sawa kabisa na hayo ya wayahudi..

  • Swala za wayahudi huwa ni Tatu
    • Shacharit (Hufanyika alfajiri kabla ya jua kutoka)
    • Mincha (husaliwa katikati ya siku Lakini jua likiwa limetoka utosini kuelekea magharibi)
    • Ma'ariv Au Magharib (Husaliwa jua likianza kuzama na giza likianza kuingia.....
    • sasa hivyo vyote ni sawa kama wanavyosali Dhehebu la kiislamu la shiha mara tatu kwa siku na Muongozo huo wa shala japo kwa Sunni husali mara tano Yaani Fajir,Adhuhuri,Alasiri,Magharib na Insha...japo Kwenye Quran Imeandikwa Swala Ziswaliwa kwa Nyakati Tatu..
  • Kuhusu vyakula Huku wana Kosher huku wana halal Na Ndo maana Narudia Tena Uislamu ni Modified and updated Version ya Christian na Judaism..
Kama utakuwa una jambo ambalo ni Jipya limeanza kwenye uislam niko Tayri kujifunza pia..Ila Mambo Yote Ya Uislamu yana. CHANZO KWENYE UYAHUDI

Ila kwa swala angalia Hapa Huyu Mtu anavyoswali mpaka mwishoni anavyotoa Salamu Ni process zile zile za Sala ya Kiislamu sema Kuna Baadhi ya Modofication tu waislmu wamefanya..
View attachment 3173675

Nasubiria Challenge but Nikisemacho ni Kweli
Nilichosema ni Dini kwa Ujumla ndio ,ipo tofauti kabisa na Uislamu ,

Ulichofanya wewe umedokoa visehemu vinayoshabihana tu

1. Hadithi/Sunna kwa Waislamu na Talmud kwa Wayahudi

Hadithi za Waislamu (Sunna) zinahusiana na maisha ya Mtume Muhammad na zinaelezea mifano ya kimaisha. Talmud ni kifasihi cha sheria na maelezo ya mafundisho ya Kiyahudi. Ingawa kuna vifungu vya dini ya Kiyahudi vinavyofanana na Sunna, Talmud ni zaidi ya maelezo ya kisheria, siyo kama Sunna, ambayo ni mfano wa maisha ya kimaisha ya Mtume.

2. Adhana na Shofar

Adhana ni wito wa kusali katika Uislamu na hutumika kila siku katika ibada ya Waislamu, ikitumia maneno maalum ya kiimani. Shofar ni kifaa kinachotumika katika matukio maalum ya kiroho kwa Wayahudi, kama ishara ya kuamsha waisraeli kwa ajili ya sherehe au majanga. Ingawa kuna sauti zinazoitwa "wito" katika dini hizi mbili, Adhana ni sehemu ya ibada ya kila siku, wakati Shofar hutumika kama alama ya kiroho au ishara.

3. Wudhu na Netilat Yadayim

Wudhu ni hatua muhimu katika ibada ya Waislamu kabla ya kusali, na inahusisha kusafisha mwili kwa ajili ya ibada. Netilat Yadayim ni utamaduni wa Wayahudi wa kusafisha mikono kabla ya kula chakula. Ingawa kuna hatua zinazofanana katika kusafisha mikono, Wudhu ni sehemu ya ibada ya kila siku ya Waislamu, wakati Netilat Yadayim inahusiana zaidi na tamaduni za kila siku.

4. Kuoga Janaba na Tevilah

Kuoga Janaba ni hatua ya kujitakasa kwa Waislamu baada ya hali fulani kama vile kutoka hedhi, au kwa mtu aliyekutana na manii. Tevilah ni ibada ya kujitakasa kwa Wayahudi, ambapo hutumika kuoga katika sehemu maalum iitwayo Mikveh. Ingawa kuna mfanano katika muktadha wa kujitakasa, Kuoga Janaba linatokea kama sehemu ya ibada ya kila siku, wakati Tevilah linahusiana na matukio maalum ya kidini.

5. Swala za Waislamu na Swala za Wayahudi

Swala ya Waislamu ni ibada ya moja kwa moja kwa Mwenyezi Mungu na inafanyika mara tano kwa siku. Swala za Wayahudi pia ni sehemu ya ibada, lakini ni kidogo tofauti na Swala ya Waislamu, kwani zinaelekezwa kwa kuzingatia sheria za kimila na matukio maalum ya kidini. Swala za Wayahudi hufanyika mara tatu kwa siku, na katika baadhi ya maeneo, zinafanana na hatua za Swala za Waislamu, kama vile kusimama, kuinama, na kusujudu.

6. Kosher na Halal

Vyakula vya Kosher kwa Wayahudi na Halal kwa Waislamu vina sheria maalum zinazohusiana na ulaji wa chakula. Kosher inahusiana na sheria za Kiyahudi, wakati Halal ni sheria za kidini za Uislamu. Ingawa vyakula vyote vinapaswa kufuatwa kwa umakini, sheria za Kosher na Halal zinatofautiana kimsingi katika utekelezaji wa maadili na miongozo ya kidini.

Na maswali machache kwako

1. Je, Talmud ni kifasihi cha sheria tu au pia ni sehemu ya ibada katika Kiyahudi kama Sunna inavyokuwa kwa Waislamu?

2. Je, Adhana na Shofar ni sawa katika muktadha wa ibada au ni alama za kiroho zinazotumika katika muktadha tofauti?

3. Je, Netilat Yadayim ni tamaduni au ni sehemu ya ibada ya kidini kama Wudhu unavyokuwa katika Uislamu?

4. Je, Kuoga Janaba ni sehemu ya ibada ya kila siku au ni hatua ya kujitakasa inayoambatana na matukio maalum?

5. Je, sheria za Kosher na Halal zinatofautiana zaidi katika utekelezaji wa ibada au katika muktadha wa ulaji wa chakula wa kila siku?
 
Lengo la kukuonesha fungu hilo ni kujibu ile hoja yako ya kuwa shetani hayuko duniani. Na uzuri umeweka hapa mafungu haya. Fungu la 12 linathibitisha pasipo na shaka mahali shetani alipo kwa sasa.

Naomba unijibu kama mpaka hapa tuko na uelewa wa pamoja kuhusu mahali alipo shetani.
Shetani Sijui Aliko kwa Kweli mpaka Sasa Hivi na Sidhani kama Tuna Uelewa wa Pamoja kuhusu Hilo!
Kama Ukikubali Kuwa Mbinguni Na Duniani ni zehemu Moja bhasi sawa..
Ila Usisahu kwenye Kitabu cha Ayoubu Pia tuamkuta Shetani akiwa ni muhudhuriaji wa Vikao vya Mungu sasa Sjui Vikao hufanyika Duniani ama lah
 
Vyote soma Post iliyopita hapo Post no 275 Nimekupostia

SOma #275

kweli Una thubutu kusema wayahudi hawasujudu?
kweli Huijui dini Ya Kiyahudi Vizuri

hizo waislamu wanazoziita Nguzo wayahudi wanazifata zote..
Kasoro shahada ya Mohamadi Rasull

Walibadilishiwa Ila Zaman walikuwa wakiswali kuelekea Msikiti mtakatifu na Ipo Kimaandiko walikuwa Na Qibra Ya Yerusalem..

Al Baqara aya 142..

"WAPUMBAVU miongoni mwa watu watasema: Nini kilicho wageuza kutoka kibla chao walicho kuwa wakikielekea? Sema: Mashariki na Magharibi ni ya Mwenyezi Mungu; Yeye humwongoa amtakaye kwenye njia iliyo nyooka."

Hapana!
Shabati ni waislamu wanayo na aunaweza ukaisoma Vizuri pia na wale walio ihalifu walipewa nini..
Ila waislamu wakaamrishwa Siku yao Mpya..

Suratul Jumua aya ya 9

"Enyi mlio amini! Ikiadhiniwa Sala siku ya Ijumaa, nendeni upesi kwenye dhikri ya Mwenyezi Mungu, na wacheni biashara. Hayo ni bora kwenu, lau kama mnajua."

Kuna tifauti kubwa kati ya Dini na maandiko na Ibada..

Hazina Athari

Ndyo wanakubaliana Wote kuhusu Ibada za Kafara na Wote Wana Sherehe za Kuchinja

Kukataa Na Kuwa na Mfanano ni Vitu viwili tofauti
Unasema kwa Waislamu Shabbat ni ijumaaa au nimesoma vibaya?

Shabat ni siku ya mapumziko kwa Wayahudi, inayoanza Ijumaa jioni hadi Jumamosi jioni, wakati Ijumaa kwa Waislamu ni siku ya ibada na kukusanyika kwa sala ya Jumaa. Qur'an inasisitiza kuwa Ijumaa sio Shabat.

Je, unaweza kuthibitisha kwa maandiko ya Qur'an, Hadithi, au Biblia kuwa Ijumaa ni Shabat kwa Waislamu kama ilivyo kwa Wayahudi, licha ya Qur'an kusema wazi kuwa Shabat ni tofauti na Ijumaa (Surah Al-Jumu’ah aya 9)?

Nguzo za Uislamu na Mifumo ya Kidini ya Wayahudi
Uislamu na Uyahudi zina mifumo inayofanana katika ibada za zaka, swala, na sheria za kusafisha. Hata hivyo, Uislamu ina nguzo za kipekee kama Shahada ya Muhammad.

Je, unaweza kuelezea jinsi nguzo za Uislamu zinavyofanana na ibada za Wayahudi, isipokuwa Shahada ya Muhammad?

Qibla ya Waislamu na Wayahudi
Waislamu walikuwa wanageukia Yerusalemu kabla ya mabadiliko ya Qibla kuelekea Makkah, kama ilivyoelezwa katika Surah Al-Baqara aya 142.

Kwa mujibu wa Qur'an, ni nini kilicholeta mabadiliko ya Qibla kutoka Yerusalemu kwenda Makkah?

Sherehe za Kafara na Ibada za Uthibitisho
Sherehe za kafara ni muhimu katika dini zote mbili, lakini Waislamu na Wayahudi wana utaratibu tofauti wa kufuata kafara katika sherehe zao.

Je, unaweza kuelezea tofauti kati ya sherehe za kafara za Waislamu na Wayahudi?

Tofauti kati ya Dini na Ibada katika Uislamu na Uyahudi
Dini inahusisha mafundisho na imani, wakati ibada ni utekelezaji wa imani. Qur'an na Biblia zinatoa mifano ya utofauti kati ya dini na ibada.

Je, kuna mifano ya maandiko ya Qur'an na Biblia yanayoonyesha utofauti kati ya dini na ibada?
 
Shetani Sijui Aliko kwa Kweli mpaka Sasa Hivi na Sidhani kama Tuna Uelewa wa Pamoja kuhusu Hilo!
Kama Ukikubali Kuwa Mbinguni Na Duniani ni zehemu Moja bhasi sawa..
Ila Usisahu kwenye Kitabu cha Ayoubu Pia tuamkuta Shetani akiwa ni muhudhuriaji wa Vikao vya Mungu sasa Sjui Vikao hufanyika Duniani ama lah

Nakuomba urejee ule mstari wa 12, ili kujua ni wapi alipo.
 
Nilichosema ni Dini kwa Ujumla ndio ,ipo tofauti kabisa na Uislamu ,
Halafu Rudi Kasome Mimi Nilisema Dini au Nilisema Ibada..
Na ndo maana Nilikuuliza mara Mbili Unajua Tofauti ya Dini na Ibada..
Ulichofanya wewe umedokoa visehemu vinayoshabihana tu
sijadokoa Nilivyovitoa Ndo Msingi hasa wa Dini Hizi mbili yoyote asiye swali kati ya Dini Hizi mbili Huesabika Kuwa hafanyi Ibada..
yoyote asiyesoma Talmud na Hadithi huhesabika Ni mtu asiyejua Dini..Yoyote asiyefanya wudhu na Netilat hana Utukufu..

mwanzoni Nilikuambia Kuwa Unapoingia kwenye Mijadala Jitahidi Usitafute Kushinda Lengo Liwe ni Kuelimika Ila kama Ukitafuta Kushinda Utatoka Kappa Katika kuelewa baadhi ya Vitu..

mimi Huwa naingia Kwenye Mijadala lengo ni Kupata Elimu nisiyo nayo..

viko Vitu vingi sana Nimeweka Vichache kwa sababu ya Ugumu wa Kuviandika Vyote na Najua Pia nikiandika Viti vingi hitaweza kusoma..
1. Hadithi/Sunna kwa Waislamu na Talmud kwa Wayahudi

Hadithi za Waislamu (Sunna) zinahusiana na maisha ya Mtume Muhammad na zinaelezea mifano ya kimaisha. Talmud ni kifasihi cha sheria na maelezo ya mafundisho ya Kiyahudi. Ingawa kuna vifungu vya dini ya Kiyahudi vinavyofanana na Sunna, Talmud ni zaidi ya maelezo ya kisheria, siyo kama Sunna, ambayo ni mfano wa maisha ya kimaisha ya Mtume.
kuna Hadithi halafu Kuna Sunna..
Kama kweli wewe Ni Ulikuwa Mwislamu utaweza Kutofautisha Kati ya Hadithi na Sunna..

Na Sikuweka Talmud peke yake soma Ili.Kuelewa Sio Kusoma Ili kujibu Hoja Zangu uonekane kwanmba umeweza kuziwekea Pingamizi..
2. Adhana na Shofar

Adhana ni wito wa kusali katika Uislamu na hutumika kila siku katika ibada ya Waislamu, ikitumia maneno maalum ya kiimani. Shofar ni kifaa kinachotumika katika matukio maalum ya kiroho kwa Wayahudi, kama ishara ya kuamsha waisraeli kwa ajili ya sherehe au majanga. Ingawa kuna sauti zinazoitwa "wito" katika dini hizi mbili, Adhana ni sehemu ya ibada ya kila siku, wakati Shofar hutumika kama alama ya kiroho au ishara.
kumbuka Sijaweka Shofar peke yake Nimekuwekea Mpaka Shema Yisrael!
Eleza Kuhusu Hiyo ambayo Nimekuwekea Mpaka Video..
Na kwa bahati nzuri nimeweka mpaka Maneno ya Imani na Nimeonyesha yanatoka kitabu gani..

hapa ndo naamini Unasoma Ili upate njia ya kujibu..
Na Ningependa Usome zaidi Kuhusu Shofar Inaonekana Huna Elimu nayo kabisa..

3. Wudhu na Netilat Yadayim

Wudhu ni hatua muhimu katika ibada ya Waislamu kabla ya kusali, na inahusisha kusafisha mwili kwa ajili ya ibada. Netilat Yadayim ni utamaduni wa Wayahudi wa kusafisha mikono kabla ya kula chakula. Ingawa kuna hatua zinazofanana katika kusafisha mikono, Wudhu ni sehemu ya ibada ya kila siku ya Waislamu, wakati Netilat Yadayim inahusiana zaidi na tamaduni za kila siku.
Wudhu sio Kusali tu Mkuu..
wudhu hata Ukiataka Kula unatakiwa utie Udhu..
kulingana na Maandiko kabla hujachangia Hoja Ijue kwanza hoja
4. Kuoga Janaba na Tevilah

Kuoga Janaba ni hatua ya kujitakasa kwa Waislamu baada ya hali fulani kama vile kutoka hedhi, au kwa mtu aliyekutana na manii. Tevilah ni ibada ya kujitakasa kwa Wayahudi, ambapo hutumika kuoga katika sehemu maalum iitwayo Mikveh. Ingawa kuna mfanano katika muktadha wa kujitakasa, Kuoga Janaba linatokea kama sehemu ya ibada ya kila siku, wakati Tevilah linahusiana na matukio maalum ya kidini.
Kuoga Janaba ni ibada ya Kila siku 🤣🤣🤣

kaka Jitahidi Usome Ndo kitu pekee Kitakuokoa
maana Ninaamini hata Unachokiandika Hukujui vizuri ..

5. Swala za Waislamu na Swala za Wayahudi

Swala ya Waislamu ni ibada ya moja kwa moja kwa Mwenyezi Mungu na inafanyika mara tano kwa siku. Swala za Wayahudi pia ni sehemu ya ibada, lakini ni kidogo tofauti na Swala ya Waislamu, kwani zinaelekezwa kwa kuzingatia sheria za kimila na matukio maalum ya kidini. Swala za Wayahudi hufanyika mara tatu kwa siku, na katika baadhi ya maeneo, zinafanana na hatua za Swala za Waislamu, kama vile kusimama, kuinama, na kusujudu.
ILa mwanzoni ulisema Kuwa Swala ya wayahudi hakuna Kusujudu 🤣🤣

Mi naona Najenga Hoja na Mtu asiye Jua hata Anazungumza kuhusu Nini
6. Kosher na Halal

Vyakula vya Kosher kwa Wayahudi na Halal kwa Waislamu vina sheria maalum zinazohusiana na ulaji wa chakula. Kosher inahusiana na sheria za Kiyahudi, wakati Halal ni sheria za kidini za Uislamu. Ingawa vyakula vyote vinapaswa kufuatwa kwa umakini, sheria za Kosher na Halal zinatofautiana kimsingi katika utekelezaji wa maadili na miongozo ya kidini.
Sheria ya Kosher na Sheria za Halal hazitofautiani hata Kidogo zote zina Msingi wa Kutoka kwenye Mambo ya Walawi 7 😁😁
Na maswali machache kwako

1. Je, Talmud ni kifasihi cha sheria tu au pia ni sehemu ya ibada katika Kiyahudi kama Sunna inavyokuwa kwa Waislamu?
Sunna Sio Ibada sunna Ni Sehemu ya Fasihi na Ni chanzo cha Sheria ya Fiqhi za Kiislamu kama Ilivyo Halakha na Agaddah kwa Talmud
2. Je, Adhana na Shofar ni sawa katika muktadha wa ibada au ni alama za kiroho zinazotumika katika muktadha tofauti?
Kasome kuhusu Shema Yisrael na Shofar Vizuri utajijibu swali hilo
3. Je, Netilat Yadayim ni tamaduni au ni sehemu ya ibada ya kidini kama Wudhu unavyokuwa katika Uislamu?

4. Je, Kuoga Janaba ni sehemu ya ibada ya kila siku au ni hatua ya kujitakasa inayoambatana na matukio maalum?

5. Je, sheria za Kosher na Halal zinatofautiana zaidi katika utekelezaji wa ibada au katika muktadha wa ulaji wa chakula wa kila siku?
Itoshe Kusema Kasome Dini Moja moja kabla ya Kuja hadharani na kuichambua Dini Hiyo..

Kuhusu Uyahudi Ndugu yangu Huuujui na Kuhusu uislamu Pia Huujui

Naomba Niwasilishe Kalamu
 
Back
Top Bottom