Maelezo kuhusu kupandishwa kwake:
Ibn Haatim amesimulia kwamba Ibn 'Abbaas رضي الله عنهما amesema: "Kabla ya Allaah Kumpandisha 'Iysaa mbinguni, 'Iysaa alikwenda kwa Maswahaba zake kumi na mbili katika nyumba. Alipofika, nywele zake zilikuwa zikichuruzika maji akasema:"Kuna miongoni mwenu ambao watanikufuru mara kumi na mbili baada ya kuniamini". Kisha atasema: "Nani atakayejitolea abadilishwe umbo lake liwe kama langu ili auliwe badala yangu na atakuwa pamoja na mimi Peponi?" Mmoja wao aliye mdogo kuliko wote alijitolea lakini 'Iysaa akamuambia akae chini. Kisha 'Iysaa akauliza tena atakayejitolea na kila mara ilikuwa ni huyo huyo kijana mdogo aliyejitolea lakini 'Iysaa akamuambia akae chini. Kisha tena kijana huyo akajitolea tena na mwisho 'Iysaa akasema : "wewe utakuwa ni huyo mtu". Akafananishwa na 'Iysaa na 'Iysaa akapandishwa mbinguni akipaa juu katika uwazi (uliofunuka juu ya sakafu ya nyumba). Mayahudi walipokuja kumtafuta 'Iysaa wakamuona huyo kijana (wakidhani kuwa ni 'Iysaa) wakamuua (kwa kumsulubu) Baadhi ya maswahaba wakamkufuru mara kumi na mbili baada ya kumuamini. Kisha wakajigawa katika makundi matatu. Kundi la mwanzo Al-Ya'aqubiyyah (Jacobites) wamesema: "Allah Amebakia na sisi Alivyojaalia kisha akapanda juu". Kundi la pili An-Nasturiyyah (Nestorians) wamesema: 'Mtoto wa Mungu alikuwa na sisi alivyojaaliwa kisha Allaah Akampandisha mbinguni. Kundi la tatu Waislamu wakasema: "Mja na Mjumbe wa Allaah amebakia na sisi Alivyomjaalia Allaah, kisha Allaah Akamchukua Kwake". Makundi mawili yaliyokufuru wakaungana dhidi ya Waislamu na wakawua. Tokea ilivyotokea hivyo, Uislamu ukafunikwa, hadi Allaah Alipomleta Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم " [Usimulizi huu una isnaad sahihi inayofikia hadi kwa 'Ibn 'Abbas na An-Nasaiy amesimulia kutoka kwa Abu Kurayb ambaye amepokea kutoka kwa Abu Mu'aawiya – Ibnu Kathiyr: 3-28-29]
Baada ya kupata maelezo yote hayo, Muislamu inampasa ayaamini maneno ya Allaah سبحانه وتعالى na Mtume Wake صلى الله عليه وآله وسلم kuhusu kupandishwa Nabii 'Iysaa ('alayhis-salaam) na ajitoe na shaka yoyote nyingine ili aokoke na upotofu uliowapoteza wengi.
Na kama inawashangaza wengi kupandishwa kwake na baadhi yao wenye kutumia akili zao juu ya dini badala ya kufuata Qur-aan na Sunnah, wanapaswa wakumbuke kuwa kwa Allaah سبحانه وتعالى hilo si kubwa, kama Alivyomleta duniani kwa kuzaliwa na mama yake bila kuingiliwa na mwanamume,