Hakuna Ubishi Mwabukusi ni Mwanaharakati, Je TLS Yake Iwe ya Kiharakati, Au Asilete Harakati Zake kwenye TLS Yetu, Ibaki Kuwa Profesheno Body?

Kumbe kutafuta haki kwa njia ya maandamano ya umma siyo uprofesheno?
 
Badala ya kumshutumu legal expert wetu Paskali aache bange, nadhani ingekuwa busara kumuuliza jinsi anavyouelewa uanaharakati.
 
Mtajuana wenyewe mliomchagua uzuri niliwapa tahadhari mapema.

Hata hivyo amesema hana Mpango wa kupinga Kila kitu Cha Serikali ila atahakikisha amri za mahakama zinaheshimiwa.
Ukizingatia nguvu iliyotumika ili kujaribu kumzuia asigombee wala kushinda, unajua kabisa kuna watu kazi wanayo kufuatia ushindi wake.
 
Kila nchi duniani ina ‘Law Society’ na zote mission statement zao zinafanana.

Kama kawaida yetu hii law society ya Tanzania ishajipa majukumu wasio nayo kwa sheria za mamlaka ya Tanzania.

Ningekuwa serikali kama kuna sheria inaitambua TLS kama advisory body na hii repeal tu hiyo sheria kwa sababu taasisi imegeuka ya siasa.
 
Ni aibu kwa TLS kuongozwa na mwanasheria wa kiwango cha Mwabukusi. Amejawa na ego na jazba vitu ambavyo havifanani na hadhi ya kiongozi wa wanasheria.

Huwa mnajiita wanasheria wasomi, maana yake mnayo haiba ya kisomi. Mwabukusi hana hiyo haiba pia ni mweupe tu katika masuala mapana ya kisheria ( maoni ya mwanasheria mwenye kuongoza taasisi fulani kubwa).

Tatizo ni uwepo wa kundi kubwa la wanasheria vijana ambao huu ni wakati wao, watoto wa instagram na facebook wanaanza kujaa kwenye masuala ya sheria.
 
Je, uana harakati ni dhambi, ni kosa?
Uana harakati ni dhana inayorejelea juhudi na shughuli zinazofanywa na mtu au kundi la watu kwa lengo la kuleta mabadiliko katika jamii. Hii inaweza kujumuisha kupigania haki za kijamii, kisiasa, kiuchumi, au mazingira. Wanaharakati wanajitolea muda wao, rasilimali zao, na mara nyingi hata maisha yao ili kuboresha hali ya maisha ya watu wengine au kupambana na ukosefu wa haki au unyanyasaji wa aina yoyote.

Vipengele vya uana harakati ni pamoja na:

  1. Kufahamu na Kuchambua Tatizo: Wanaharakati huanza kwa kuelewa tatizo fulani katika jamii, kuchambua sababu zake, na kutafuta njia za kulitatua.Je, Mwabukusi akifanya hilo ni kosa?
  2. Kujenga Uhamasishaji: Wanaharakati wanajitahidi kuwahamasisha na kuwaelimisha watu kuhusu tatizo na umuhimu wa kuchukua hatua. Hii inaweza kufanyika kupitia kampeni za habari, mikutano ya hadhara, au mitandao ya kijamii.Je, Mwabukusi akifanya hilo ni kosa?
  3. Kutetea Mabadiliko: Wanaharakati hutumia njia mbalimbali kutetea mabadiliko, kama vile maandamano ya amani, maandiko ya sera, kushiriki katika majadiliano ya umma, au kuwasilisha maoni yao kwa watoa maamuzi.Je, Mwabukusi akifanya hilo ni kosa?
  4. Kushirikiana na Wengine: Wanaharakati mara nyingi hushirikiana na mashirika mengine, serikali, na watu binafsi wenye malengo yanayofanana ili kuongeza nguvu na ushawishi wa harakati zao.Je, Mwabukusi akifanya hilo ni kosa?
  5. Kuvumilia na Kuendelea Kupambana: Uana harakati mara nyingi hukutana na vikwazo na upinzani, lakini wanaharakati wa kweli huvumilia na kuendelea kupambana kwa ajili ya malengo yao.Je, Mwabukusi akifanya hilo ni kosa?
  6. Kutekeleza na Kusimamia Miradi: Wanaharakati pia wanaweza kuanzisha na kusimamia miradi inayolenga kutatua tatizo waliloliona, kama vile kutoa elimu, huduma za afya, au kuanzisha mipango ya maendeleo ya jamii.Je, Mwabukusi akifanya hilo ni kosa?
Kwa ujumla, uana harakati ni shughuli zinazohusisha kujitoa kwa dhati kwa ajili ya kuleta mabadiliko chanya katika jamii na kuhakikisha haki na usawa kwa wote.
by the way, kaka Pascal Mayalla asante kwa andiko zuri na ujumbe fikirishi.
 
UWT mlishindwa kutoa Rais wa TLS?
 
Wanaiharibu taasisi yao wenyewe kutoka kuwa professional body ya ushauri, kulinda maslahi yao wanasheria na kuwa neutral kwenye kukosoa maamuzi ya mahakama wanapoona haki aijatendeka.

Sasa professional body inapoingiza siasa ni wazi inakosa sifa ya kuonekana impartial kwenye ushauri. Matokeo yake hata wakitoa ushauri ambao ni sound kwa serikali, kwakuwa washaingiza siasa chances are hautopokelewa.
 
Harold Sungusia nimemsikiliza mara chache akihojiwa lakini siku zote ana substance kichwani mwake.

Ni kichekesho mrithi wake kuwa Mwabukusi mwenye elimu za kuungauunga na asiye na utulivu wa kuongea mbele ya camera.

Hii ni aibu ya wanasheria wote waliopiga kura.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…