Hakuna Ubishi Mwabukusi ni Mwanaharakati, Je TLS Yake Iwe ya Kiharakati, Au Asilete Harakati Zake kwenye TLS Yetu, Ibaki Kuwa Profesheno Body?

Mtoa mada mteuliwa akili yake hapo inawaza maandamano yatokee ili akahamasishe,anawaza kupayuka kuhusu bandari utafikiri hajasoma kuhusu investments au Contracts.TLS wanajukumu la kuishauri Serikali kuhusu mambo yanayohusu sheria lakini tambueni hayo ni maoni Serikali si lazima wafuate sababu mnachukua mikakati ya upinzani huko mnataka kuilisha Serikali mnataka katiba mpya halafu mnashindwa kueleza hii iliyopo ina shida gani,Katiba ni ya wananchi siyo ya CDM mnawaburuza wananchi Wadai katiba mpya wakati hata hawajui inaongelea nini.TLS angalieni katiba ya chama chenu inasemaje na heshimuni utawala uliopo kama maoni au ushuari fikisheni kwa njia zinazoendana na taaluma zenu sio kutuletea maneno ya chuki na ya kuhatarisha amani iliyopo.
 
Hivi kuwa ni mwanaharakati/activist ni dhambi na imeandikwa wapi kwamba activist hawatakiwi humu duniani? Je wao activist -Ni Nephilims/Giants walio sababisha gharika kuu ma Mungu kuwatokomeza ? Nchi ni yetu sote na moja kama ilivyo kwa Mungu na Dada yake Amara, sasa ugomvi wa nini ? Kama Mungu na Dada yake wana shirikiana, kwa nini sisi tuwakatae akina Mwabukusi na rafki zake?
 
Kwa hiyo ilifaa wampigie kura nani?Elimu na uweledi/ufanisi ni vitu viwili tofauti.
Unaweza ukawa na mavyeti makubwa ila kwenye output ya kazi ikawa zero
 
Paschal alitaka TLS iwe chini ya CCM
 
Kwani wao ni wabunge hadi wazipitishe?

maoni kuhusu Mswaada wa Sheria ya uchaguzi na Tume ya Uchaguzi umeona ccm imechukua hata moja?

Wewe usidhani ccm wao ni wajinga wachukue maoni yatakayo waondosha madarakani.
Hakuna aliyesema waipitishe, ni waipitie. Soma vizuri. TLS wanaweza kuipitia muswada wa sheria na kwa elimu yao wakaelimisha umma uzuri na ubaya wa sheria inayotaka kupitishwa.
 
Pascal hujui hata maana ya harakati. Unasemaje harakati vs professional ikiwa hujaelezea harakati ni nini na professional ni nini.
P anajichanganya sana, ni hofu yao kuwa hawataweza tena kuitumia TLS kwa itikadi zao za kisisasa. Chama changu kina hofu siku zote chaguzi kuu zinapokaribia, wanapenda kada mwenzetu ndiye awe bosi hapo TLS.
 
Layman unawapangia mawakili , watu waliosoma HGL na HKL na wana Division 1.7 form 4 na division 1. 3 form Six na chuo kasoma miaka 4 na Law School mwaka 1 kwamba hawana akili kumchagua Mwabukusi?

Ninyi CWT mchagueni MATRAVOLTA awe raisi wenu.
 
Mzee Mpoki, Jenerali Ulimwengu, Tenga, hiyo ni kaliba ya wanasheria maarufu na wenye mantiki vichwani mwao, kukubali kuongozwa na Mwabukusi ni doa kwenye taaluma nzima ya sheria.
Kwamba DAS aliyekuwa anaiba mafuta ya Gari za serikali ndio ingelikuwa sahihi?
Kwamba kuongozwa na Mwanaume wakili ambaye analelewa na mke wake ambaye ni mbunge na naibu waziri ndio ingekuwa sahihi?
 
Mwanaharakati ndio kila kitu mkuu!.. Sasa itatusaidia nini wananchi kuwa na mtu DORMANT PROFESSIONAL.
 
Utasikia wanasema Mimi sikaki siasa
Au Mimi sio mwanaharakati

Wote ni wajinga
Kila mtu ni mwasiasa na ni mwanaharakati kwa kuzaliwa
Siasa au harakati zitategemea mazingira aliyomo

Chama Cha ANC Kuna wakati kilikuwa chama Cha harakati
Baada ya ubaguzi kikabadilika kuwa chama Cha siasa

TLS inaweza kuwa Wanaharakati pia kuwa wanataaluma kulingana na mazingira yalivyo

Kuna kipengele Cha huduma kwa umma si ndo kitawafanya tls automatically wahaharakati ikiwa jamii Ina uhitaji

sijui kama Pasco atanielewa
maana hata huo uwakili amupata kwa kuungaunga
 
Tofautisha kati ya harakati za kisheria(legal activism) na harakati za kisiasa (political activism). Inaonekana unaposema "mwanaharakati" una maana political activist.
Katika historia ya sheria, legal activism ndio iliyosaidia field za constitutionalism, human rights na rule of law ku evolve over time. Sasa hii sio professionalism kwenye uga wa sheria?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…