Hakuna Ubishi Mwabukusi ni Mwanaharakati, Je TLS Yake Iwe ya Kiharakati, Au Asilete Harakati Zake kwenye TLS Yetu, Ibaki Kuwa Profesheno Body?

Yes, inawezekana ni kweli Mwanaharakati ndio kila kitu, lakini jee umemsikia mwenye nchi yake, anataka TLS ya aina gani?. Hebu msikilize kwa makini,
View: https://youtu.be/fZ7MWhPeykohalafu mshauri Mwabukusi
P
Katiba inasema sisi.....na sio mimi...... Hivyo mama kesha jichanganya. TLS ina malengo yake na kubwa ni kuona utawala wa sheria unatamalaki. Na hapa tunaongelea sheria bora, ni wazi kutakua na minyukano ya hapa na pale hasa ukichukulia bunge letu. Mama anataka aungwe mkono vinginevyo......
Uana harakati ukifanya kazi ndani ya sheria kuna tatizo gani? Nyerere na wenzake wikua wanaharakati. TLS inahaki ya kwenda kiharakati kwenye masuala muhimu.
 
Paskali hebu tusaidie Sisi tusiojua sheri, nimemuona na kumsikia Mwabukusi akisisitiza kuhusu section four; hebu tujuze kwa maswali haya:
1. Section 4 ina uharakati au haina?
2. Nini maana ya uwanaharakati?/
3. Dai la katiba mpya TLS wafanye nini kuepuka uwanaharakati.?
4. Kama itatokea kiongozi anakataa kutekeleza Jambo la kiheria TLS wanawajibu gani?
5. Young lawyers watafanye Bila kwenda field ili kuwa professional?

Kindly, I submit for replies
 
Harakati ni activism, mwana harakati ni activist
P
Mwanaharakati ni "activist" kwa kiingereza..

"Activist" inatoka kwenye Neno mzizi "active" lenye maana ya "kitu au mtu au jambo au mawazo yaliyo hai.."

The opposite
ya neno "active" ni neno "inactive" lenye maana ya "kitu au mtu au jambo au mawazo yasiyo hai, yaliyolala au kufa kabisa"

Kwa hiyo na kwa ufafanuzi huo it's very clear kuwa, dhana nzima ya andishi lako ni kumtaka Adv. Boniface Mwabukusi na TLS anayoingoza iwe "INACTIVE" ili maharamia ya CCM ndani ya serikali na jamii yaendelee na uharamia wao wa miaka yote kunajisi sheria na Katiba na kunajisi utawala bora unaozingatia sheria na katia, au siyo ndugu Pascal Mayalla?

Kwa upotofu wako huu, usingependa TLS ambayo kimsingi ndiyo taasisi kiungo cha sheria kati ya wananchi, serikali (executive), mahakama (judiciary) na Bunge (Legislature) kwa kuendelea kuwa "INACTIVE" katika maswala yote ya kisheria hata kama sheria zinahalifiwa, au siyo ndugu Pascal Mayalla?

Hebu fikiria tena na ujiulize, kuwa, kwa akili na ufahamu wako unadhani umekaa na kufikiri vizuri kabla ya kushika kalamu yako na kutoa ushauri huu mbaya kabisa..?

Nyie wana CCM futeni hayo mawazo yenu na dhana zenu potofu hizo kwa zimepitwa na wakati na Sasa jamii kuwa ya Watanganganyika inajielewa na kujitambua..

Haiwezekani tena kuishi kwa kuendelea kuwa - manipulate watu..!!

Pascal Mayalla hapa kwa sehemu kubwa zaidi ya 90% umechemka, unapiga propaganda zilezile mfu za miaka yote za ki - CCM bila kujua kuwa majira na nyakati zimeshabadilika..

Na hapa ni aidha hujui au unapotosha ukweli wa mambo kwa makusudi na kwa faida zako binafsi..

It's shame kuwa hili linafanywa na mwandishi wa habari au mwanasheria wewe mtu ambaye ulipaswa kusimamia haki na ukweli daima kwa manufaa ya jamii nzima..
 
Ninachoelewa mimi ni kwamba wanasheria wana uelewa mkubwa sana wa mambo kuliko raia wa kawaida kama mwabukusi hafai kiwango hicho ilikuaje wakamchagua kwa wingi wa kura namna Ile!?

Kwa kuwa chama hiki ni professional body iweje tuwe na wasiwasi kwamba mwabukusi ataipelekesha si wote ni wanasheria hawa!? Mimi nadhani ndio wataonyesha umwamba wao wa kumdhibiti kisheria.
 
Layman unawapangia mawakili , watu waliosoma HGL na HKL na wana Division 1.7 form 4 na division 1. 3 form Six na chuo kasoma miaka 4 na Law School mwaka 1 kwamba hawana akili kumchagua Mwabukusi?

Ninyi CWT mchagueni MATRAVOLTA awe raisi wenu.
Hao wanasheria ni malayman pia, usitishwe na zile suti zao nyeusi na kola nyeupe wanazozivaa pale mahakama kuu wengine ni wa viwango vya Notary Public.
 
Kuwa na elimu ni kitu kimoja kujua kuishi na watu na kuweza kujichanganya ni suala jingine tofauti kabisa.
Yeah kuna watu wanachanganya mambo wanadhani mtu mwenye vyeti vikubwa ndio anaweza akafit kila mahali.
Watu wangapi tunawaona ni Maprofesa na hawana cha maana walicholeta zaidi ya kuishia kuwa machawa tu
 
We paskali ni mwanasheria?? Mbona unachangiaga pumba sana kwenye mambo ya kisheria??
Ukijititizama kweli mwabukusi anaweza kukusikiliza wewe? Harakati ni bidii zaziada kufanikisha mambo sasa Aaache harakati alale tuu ofisini? TLS ni "bodi profesheno" huo uprofesheno ndio harakati za kutetea Sheria/wanasheria/wadau zisifanyike?
Waliomchagua wamemkubali alivyo wewe Leo unataka awe utakavyo wewe kivipi? Kwaniwewe kunanini hasa au umeifanyiaga hii nchi Nini cha maana?? zaidi ya kutangaza sabasaba unakipi?
 
Ushawahi kumuona akipambana mahakamani 😄
Wanasheria kuwa mwanaharakati hiyo ni kawaida....labda paskali yeye hautaki uhanarakati

Ova
 
Kwani mwanaharakati hawezi kuwa proffesional na vaisi vesa
 
Kwani mwanaharakati hawezi kuwa proffesional na vaisi vesa
Professional bodies zina ongozwa na professionals na zina deal na professionalism, activism zina ongozwa na ma activists na zina deal as pressure groups.
P
 
Professional bodies zina ongozwa na professionals na zina deal na professionalism, activism zina ongozwa na ma activists na zina deal as pressure groups.
P
Professionalism na activism sio brands ambazo hazichangamani, mfano gongo na chai. Unaweza ukawa activist kwenye proffesion yako, kama vile baadhi yenu mnavyochangaya taaluma zenu na uchawa
 
Kupongeza mtu anayefanya kazi iliyo kwenye majukumu yake ya kila siku (job description), mfano kukusanya kodi na kuzipeleka kwenye shughuli za maendeleo ni uchawa!

Hata wewe haupongezwi kwa kuamka na kwenda kufanya majukumu yako ya kila siku!

Pongezi zinafaa pale mtu anapofanya jambo la ziada, mfano kuweza kupambana na wakati mgumu (crisis) kama Covid, vita, ukame, nk au kufanya jambo ambalo watu hawakutegemea (kujenga reli, nk).

Pongezi na asante za kila siku na kwa kila jambo ni uchawa...inasababisha pongezi zisiwe na nguvu tena!!!
 
Ukiwa kama mwanasheria mtanganyika ukapanua mdomo kupongeza Mzanzibari anayeuza mali za Tanganyika, bandari, airports, misitu, madini nk, huku akijaza wazanzibari wenzie kwenye ajira za watanganyika, unastahili kuitwa chawa mwenye njaa kama jina lako, anayekaa kwenye nywele chafu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…