Hakuna Ubishi Mwabukusi ni Mwanaharakati, Je TLS Yake Iwe ya Kiharakati, Au Asilete Harakati Zake kwenye TLS Yetu, Ibaki Kuwa Profesheno Body?

Mkuu Gulwa, with due respect, hizi za kumuita ntu kwa utambulisho wa eneo analotoka kwa ubara na Uzanzibari, ni ubaguzi!, nimekusamehe kwasababu sio wewe tuu, wengi hawajui, unahitaji sana elumu ya uraia, baada ya Tanganyika na Zanzibar kuungana kuwa Tanzania, uraia ni mmoja tuu, Utanzania, na Watanzania wote wana haki sawa za uraia ndani ya JMT, hakuna Mzanzibari wala Mtanganyika kuna raia mmoja tuu Mtanzania, hivyo kwanza tuache ubaguzi kisha ndipo tujadiliane hayo mengine,
P
 
Wanabodi,
Hii ni makala yangu gazeti la Nipashe la leo
[

Mungu Ibariki Tanzania

Paskali.
"Kwa vile yeye ni Mwanaharakati, namuomba sana, chonde chonde asituletee uana harakati wake kwenye TLS yetu , TLS sio chama cha siasa, sio chama cha ki harakati, TLS ni a Professional Body"! Mathlani angekuwa mlokole, ungeandika asituletee ulokole wake! Uandishi wako unakiharufu cha hasira za kushindwa. Kila mtu anazo pande mbili za maisha na pande hizo ndizo zinazotukutanisha, mfano ninaweza kuwa na rafiki mzuri kwangu kumbe ni jambazi yaani mwema kwangu huku kazini kwake mkatiri. Wapo pia majaji wanahukumu vifo watuhumiwa na huku ni walokole, hata hivyo ulokole wao hawaufanyii ndani ya mahakama. Kwa kifupi komenti yako ni ya hasira na inakolezwa na "asituletee uanaharakati wake"!
 
Kaka PASCO,Uanaharakati wa MWABUKUSI ni upi?.
 
Wewe unaweza kugombea cheo chochote Zanzibar? Wao wana rais wao, serikali yao, bunge lako, bendera yao nk. Acheni unafiki na uchawa
 
Mkuu Hismastersvoice, kwanza asante sana kwa post yako hii, kiukweli wewe ni miongoni mwa wana jf wachache wenye uwezo wa kusoma andiko la mtu na kubaini the motives behind, uwezo huo ni kipaji unaitwa graphology, unasoma andiko la mtu, unajua the moods and emotional status ya mwandishi. You are very right, haswa ukizingatia mimi ni member wa TLS na nilipiga kura.

Kwa vile hii sii mara ya kwanza kwa TLS kuongozwa na mwanaharakati, hatutaki kurudia kosa, hivyo tuna wajibu wa kumsaidia rais wetu Mwabukusi aendeshe TLS yetu ki professional na sio kiharakati.
P
 
Maisha ya nje ya ujuzi ni tofauti na ya ndani ya ujuzi, ni vigumu sana wewe kumkubali mwenye vinasaba vya Chadema hata angekuwa dakitari wa wanyama.
Mbona uwekaji picha ya mtu kwenye bendera ya Tanzania hatujadili pamoja na kuwa la kisheria na katiba tunamjadili mtu Mwabukusi!
 
Kama inabidi tupongezane kwenye majukumu ya job description basi makazini tutatumia muda mwingi kwenye kupongezana kuliko kufanya kazi husika: (karani) "pongezi kwa kupiga photocopy" (cleaner) " pongezi kwa kufagia" (bank teller) "pongezi kwa kudeposit na kutoa hela" nk nk. Ni chawa nation hiyo.
 
Duu swali kifikirishi neno rubber stamp hutumikaje kisheria mfano utakaposema, that organization is just a rubber stamp, this question is related to silent society when deprived the right to know about the where about of their leader's health, what will happen if TLS decides to also keep quite
 
P hofu yako nini au mshikamano wako na wala kwa kamba watafuna na wafujaji wa kodi zetu ni wa viwango vya juu kiwango ganiii?
 
Ni kichekesho mrithi wake kuwa Mwabukusi mwenye elimu za kuungauunga
Basi ni kichekesho pia kama taifa kuwa na viongozi wakuu wenye elimu za kuunga unga!!!
Unalijua hilo la viongozi wakubwa wa serikali yako wenye elimu za kuungaunga!??
 
Mkuu Hismastersvoice , tuko humu pamoja na wewe for more than ten years now, kama unaamini siwakumbali wenye vinasaba na Chadema, then you are very wrong!, japo mimi ni kada wa Chama cha Mapinduzi, mimi sio ile type ya makada matutusa, kuna makada wanaoitwa ma lumpen, kuna ma prolétariat na kuna ma bourgeoisie, mimi niko kwenye kundi la ma proletariat, tunapenda CCM ipate credible opposition, kwa Tanzania, chama chenye kuonyesha hata dalili tuu, ni Chadema, hivyo kuna wana CCM wengi tuu wa type yangu, tunaikubali sana Chadema, na kuna Chadema nawajua, wanaikubali sana CCM.
Mtu anayeichukia Chadema, hawezi kupandisha, posts kama hizi
p.
 
Komenti zako dhidi ya wanachadema zinajieleza, kuuma na kupulizia ni jambo la kawaida. Mimi nilifikia kusema hayo muda mrefu sana na hata wewe mabandiko yako mengi yanaishutumu Chadema, anyway tukubaliane kutokubaliana.
 
Wanasheria wenzako waliliona hilo na kufahamu kuwa yeye ni mwanahatakati na bado wakamchagua so sioni haja ya kumfundisha rais wako ni jinso gani ya kiemdesha taasisi yenu. Angalia body ya wanasheria Kenya ilivyo moto wa kutoea mbali na ikiongozwa na mwanaharakati mwanamke, je hutaki body yenu ichangamke kama ya Kenya? Au nawe ulikuwa machinery ya kuhakikisha Mwabakusi hashindi?
 
Komenti zako dhidi ya wanachadema zinajieleza, kuuma na kupulizia ni jambo la kawaida. Mimi nilifikia kusema hayo muda mrefu sana na hata wewe mabandiko yako mengi yanaishutumu Chadema, anyway tukubaliane kutokubaliana.
Everyone has the right to his opinions, I know myself and what I stand for, I don't have to justify to anybody, ila nimesema humu, kati ya wasifiaji na wakosoaji, nani wanamsaidia zaidi Chadema, usikute sisi wakosoaji ndio tunaisaidia zaidi chadema kuliko hao machawa na manyumbu,ila pia naheshimu mawazo yako
p
 
Mkuu Iki, IKINGO , unapaswa kuuliza maswali ili upatiwe majibu, hiki ulichouliza, sio swali, ni umeuliza jibu!, kuna mtu asiejua kuwa Mwabukusi ni Mwanaharakati?.
P
Mara nyingi msema kweli naye huwa anaitwa Mwanaharakati na mtu mpenda haki pia huitwa mwanaharakati.Na kama ni hivyo basi TLS ni body ambayo iko kiharakati zaidi kwa sababu iko katika mazingila ya kutaka kuona utawala wa sheria ukifuatwa na kuheshimiwa lkn pia kuona haki ikitendeka.
 
Kwa kulijua hilo nimemalizia kwa "anyway tukubaliane kutokubaliana".
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…